GE2025 Musiba: Nitashinda ubunge kwa 98%, sitaruhusu kuibiwa kura

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mwibara kupitia ACT Wazalendo Cyprian Musiba ameahidi kuzilinda kura zote atakazopigiwa na wananchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Musiba amesema hayo Agosti 31, 2025 akizungumza na waandishi wa habari wilayani Bunda akiwaomba wananchi kumpigia kura kwa wingi na kumsaidia kuzilinda.

Soma pia: Musiba: Mimi nilikuwa na ndoto ya kuwasidia wananchi Mwibara lakini naona inapotea

"wananchi nendeni mkanipigie kura mimi nitadhibiti hizo kura kuliko mnavyofikiria" Musiba

Ameongeza kuwa ataweza kudhibiti mianya yoyote ya wizi wa kura kutoka kwa mpinzani wake.

"huyo mpinzani wangu mkuu huyo Mzee hatoniibia kura na nitalinda kura zangu vibaya sana wananchi wenzangu tutalinda kura kwa kushirikiana na nyie".

Aidha amesisitiza mwaka huu atapata ushindi wa kishindo na kihistoria.

"kwa sababu ushindi sio asilimia sabini (70%) mimi nataka nimshinde mpinzani wangu kwa asilimia tisini na nane (98%)" amesema Musiba.
 
Attachments

  • VIDEO- Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mwibara kupitia ACT Wazalendo Cyprian Musiba ameahidi kuzil...mp4
    8.7 MB
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mwibara kupitia ACT Wazalendo Cyprian Musiba ameahidi kuzilinda kura zote atakazopigiwa na wananchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Musiba amesema hayo Agosti 31, 2025 akizungumza na waandishi wa habari wilayani Bunda akiwaomba wananchi kumpigia kura kwa wingi na kumsaidia kuzilinda.

Soma pia: Musiba: Mimi nilikuwa na ndoto ya kuwasidia wananchi Mwibara lakini naona inapotea

"wananchi nendeni mkanipigie kura mimi nitadhibiti hizo kura kuliko mnavyofikiria" Musiba

Ameongeza kuwa ataweza kudhibiti mianya yoyote ya wizi wa kura kutoka kwa mpinzani wake.

"huyo mpinzani wangu mkuu huyo Mzee hatoniibia kura na nitalinda kura zangu vibaya sana wananchi wenzangu tutalinda kura kwa kushirikiana na nyie".

Aidha amesisitiza mwaka huu atapata ushindi wa kishindo na kihistoria.

"kwa sababu ushindi sio asilimia sabini (70%) mimi nataka nimshinde mpinzani wangu kwa asilimia tisini na nane (98%)" amesema Musiba.
keep Dreaming

Tume ya mama, Tume ya CCM, ikutangaze wewe umeshinda nini vile?
 
Msiba bure kabisa kipindi cha Magu alikua anatukana watu leo kajaa kwenye mfumo yuko kwenye chama cha wanamtandao
 
Back
Top Bottom