Sina uhaklika kama CCM nao wanatoa vibahasha, ila niliwahi kuwa mwandishi kipindi kirefu nyuma na sasa sio mwandishi tena bali mratibu wa waandishi kwenye matukio, vibahasha ni muhimu na kwenye kila shughuli ninayoiratibu, lazima nihakikishe hivi vibahasha vinatembea, kwa lengo moja tuu, sio kuinfluence watakachoripoti, bali kuwafacilitate mobility ya kuweza kuja na hatimaye kurejea watokako.
Sio mara moja wala mbili, wale waandishi wa wa vyombo makini, wakiwemo TBC, ITV, Star TV, Chanel Ten, Daily News, Mwananchi na IPP media, siku zote huwa wanapewa usafiri toka ofosini kwao, na usafiri huo huwasubiri kwenye tukio mpaka wamalize na kuwarudishas news room, hivyo kwao, ka bahasha sio muhimu sana unless wapokee tuu kwajili ya kunywa chai, au wakakae viti virefu baada ya kazi.
Naombeni haka ka bahasha msikatafasiri vibaya, ni ka bahasha ka halali, kama wakuu wengine wote wanapohudhuria vikao, hupewa sitting alowance, wanapukuwa kwenye kazi mpaka time ya chukula, either hupewa lunch alowance au chakula halisi lunch etc.
Kwa msiowajua waandishi, au kazi ya uandishi, kwa waandishi wa ukweli, hii kazi ni wito tuu, au tuseme ni kazi ya kujitolea na waandishi wa bongo, wanafanya kazi katika mazingira magumu sana, ni watu wa kuhurumiwa, hata hivyo vibahasha, si lolote, si chochote!.
Ila pioa lazima nikiri wazi kuwa kufuatia utaratibu wa vibahasha kuwa more formal, kumepelekeas fani hii kuvamiwa na kundi la watu wajulikanao kama makanjanja ambao wao lengo lao ni kuvuta kibahasha tuu. Hawa ndio wanaotuharibia sifa nzuri ya tasnia ya habari. Kosa lao ni kuchangamkia bahasha kwa kujifanya anaandikia mahali fulani, wakati ukweli wa mambo akishakunja bahasha yake na kufakamia chakula na vinywaji, hupotelea gizani, hana aandikacho!.