Museveni apasua jipu, Tanzania haikumng'oa Idd Amin peke yake!

Nimemsikia Rais wa Uganda Ndugu Mseven akiwataja kama Marais wengine watatu pamoja na Nyerere akiwashukuru kwa vita ya ukombozi ya kumng'oa Idd Amin.

Hii ni tofauti na ambavyo tumekuwa tukiaminishwa kuwa Tanzania pekee ndiyo iliyomng'oa nduli.

Sasa ninawekea mashaka vitabu vyetu vya historia. Je huu ndio ukweli?
Museveni ni mtu makini inapokuja issue ya Tanzania ya Nyerere. Hana sababu ya kudanganya lolote maana hapotezi kitu.
 
Mbona hiyo kawaida tu, kutumia wenyeji ndiyo mbinu inayotumika na "wajanja" kushinda vita. Wanamgambo wa Uganda (akina Mseven) walikuwa kama 6,000 tu, na waliongozwa na Majeshi yetu
 
Inaonekana ulikua bado hujazaliwa ama hujaifuatilia vizuri hiyo unayoiita historia, wanajeshi wa Uganda walisalimu amri wakaungana na watanzania kumng'oa Iddi Amin hiyo inajulikana tangu zamani labda kama wewe peke yako hukujua
Anajua hadithi za kunywa gahawa
 
Kweli kiswahili kigumu..Kumbe mwandishi ulimaanisha si Tanzania peke yake iliyomg'oa Idd Amin?
 
Nimesema tunafuata itikadi kuu ya kiliberali Toka kwa hao wazungu na huu uliberali unasema serikali siyo mwekezaji wa msingi bali ni msimamizi tu wa uwekezaji huo na uchumi kwa ujumla..uliberali huu huu unasema kwamba tuwe na mfumo wa kisiasa wa vyama vingi na hii tumetoa kwa hao hao waliotuletea hii itikadi. Lazima uwaguse ukiichambua hii itikadi, na hata Kenya au south au hata huko Uganda serikali hizi hazina maslahi wala nia ya kumiliki viwanda bali kuvisimamia vya watu binafsi na ndiyo maana viongozi Wakuu wakisafiri wanaongozana na wafanyabiashara na wawekezaji ili uwekezaji na biashara zifanywe na sekta binafsi huku serikali ikijikita kuhakikisha mazingira sawia ya uwekezaji huo. Ni kuelimishana tu
Kaka unajisumbua kuwaelewesha watu walioazimisha akili zao kwa wanasiasa, akisema mwanasiasa watamuelewa, waambie huko UK wanawabembeleza wawekezaji wasiondoke na viwanda vyao baada ya Brexit, Trump anaweka mpaka mkwara kwa watu binafsi wenye viwanda wasiondoshe viwanda vyao. Huwezi kumuelewesha mtu ambaye kutwa nzima anashinda JF kuangalia nini Magufuli kachemka ili amakandie watu hapa hawajui kabisa foreign affairs, labda hawajui hata nini kinatokea Kenya mpaka Zitto ama Mbowe aandike katika facebook page yake. Aibu kubwa sana....
 
Nimemsikia Rais wa Uganda Ndugu Mseven akiwataja kama Marais wengine watatu pamoja na Nyerere akiwashukuru kwa vita ya ukombozi ya kumng'oa Idd Amin.

Hii ni tofauti na ambavyo tumekuwa tukiaminishwa kuwa Tanzania pekee ndiyo iliyomng'oa nduli.

Sasa ninawekea mashaka vitabu vyetu vya historia. Je huu ndio ukweli?
anawasha kiberiti kwenye ma pipa ya petrol wewe muache tu kama hatukumuweka pale asubiri siku sio nyingi atapata majibu.Uganda bila TZ haipo just fyi
 
mkuu nifafanulie hili azimio la zanzibar, manake sijawahi lisikia, lilikuwa linahusu nini, najua arusha na iringa
Azimio la Zanzibar lilibadilisha maazimio yote ya Azimio la Arusha. Viongozi hawakuruhusiwa kuwa na biashara katika Azimio la Arusha la Zanzibar lilibadilisha watu wakaanza kujinufaisha kwa maslahi yao binafsi. Azimio la Arusha lilikataza Ubepari, Ukabaila Azimio la Zanzibar liliruhusu, Azimio la Arusha lilibinafsisha mashirika binfasi na kuyaweka chini ya serikali, La Zanzibar liliing'anya serikali na kuwapatia watu binafsi kama NBC, TBL, SIGARA n,k. Nadhani hapo nitakua nikuangaza kidogo
 
Azimio la Zanzibar lilibadilisha maazimio yote ya Azimio la Arusha. Viongozi hawakuruhusiwa kuwa na biashara katika Azimio la Arusha la Zanzibar lilibadilisha watu wakaanza kujinufaisha kwa maslahi yao binafsi. Azimio la Arusha lilikataza Ubepari, Ukabaila Azimio la Zanzibar liliruhusu, Azimio la Arusha lilibinafsisha mashirika binfasi na kuyaweka chini ya serikali, La Zanzibar liliing'anya serikali na kuwapatia watu binafsi kama NBC, TBL, SIGARA n,k. Nadhani hapo nitakua nikuangaza kidogo
umenifumbua sana kaka, swali tena lilikuwa mwaka gani hili azimio
 
Wabunge gani?

Akina Msukuma na Jah people au?

Historia tanzania wameharibu siijui kwanini maana majuzi bungeni wakati wanapanga kuhusiana na kudai ujerumani fidia juu ya maji maji ndipo nikasikia kinjiketile sio kiongozi wa hiyo vita na Pia wakataja sehemu ambazo zilianzia duh nilichoka
 
vitabu vyetu havikusema ukweli wote kuhusu amini hata sababu za sisi kuingia vitani hazikusemwa wazi
Sisi kuingia vitani ni kwa sababu
Muamar gadaf aliyekuwa rais wa libya alitoa msaada uende Tanzania kwa masharti : ili kupata msaada ule lazima uambatane na kujengwa msikiti mkubwa msikit huo ulitarajiwa kujengwa kagera lakin bhaada ya mzee kukaa na wazee wenzie wakapinga kujengwa kwa msikiti kwa hiyo sasa idi amin akasema ajengewe msikit pekee baadaa ya msikit kujengwa mzee akachukia kuukosa msaada akaifunga boda ya kagera akamwambia Hamna mtu wa Uganda kuingia Tz idi amin akamwambia sawa huku kwangu kuna watu wako na wenyew hawatoki baada ya hapo idi amin akawa anawanyanyasa sana watanzani waliokuwepo uganda baada ya mzee kuona ivo akaamsha majeshi kumshambia dadaa hapo washamuandaa museven kipind hicho anafany kaz tz baad ya hapo mzee akasema kuwa dadaa anataka kuchukua ardhi ya tz ila sio kwel mzee alitumia hiyo kiki kumweka museven madarakan kwa makubaliano flan.

KUMBUKA VITA ILE ILIKUWA YA KIDINI
 
Idd Amini aling'olewa madarakani na Tanzania na kama wapo wengine hao ni wale waliotoa mchango mdogo sana ukilinganisha na Nguli wa vita hivyo aliyekuwa ni TANZANIA.
 
Nimemsikia Rais wa Uganda Ndugu Mseven akiwataja kama Marais wengine watatu pamoja na Nyerere akiwashukuru kwa vita ya ukombozi ya kumng'oa Idd Amin.

Hii ni tofauti na ambavyo tumekuwa tukiaminishwa kuwa Tanzania pekee ndiyo iliyomng'oa nduli. Sasa ninawekea mashaka vitabu vyetu vya historia. Je huu ndio ukweli?

Museveni anaweza kuwa sahihi. Kumbuka kwamba japo Nyerere hakutaka nchi kama Msumbiji zilizokuwa tayari kutusaidia mstari wa mbele ziende vitani, wananjeshi wa Msumbiji walitumika ndani ya Tanzania kufanya "patrol" wakati wengi wa wanajeshi wetu wako mstari wa mbele. Kwa hiyo Msumbiji ilichangia. Pia ona kwamba vita ilipoanza hatukuwa na silaha wala fedha za kuendela vitani, na nchi kama Uingereza, Ujererumani hata Urusi nadhani, walikataa eidha kuutuzia au kutupa mkopo wa silaha. Nchi iliyotupa silaha hadi tukashinda vita ilikuwa Algeria - ambayo hatukutegemea kabisa. Hata Zahir Ali aliimba kwamba "kile kipindi cha vita wazazi kilikuwa kigumu, katika muda mfupi tu tumeweza kujua, nani kwetu ni rafiki, nani kwetu ni adui". Ukweli ni kwamba bila Algeria huenda Idd Amin angetupiga, hatukuwa na silaha za kutosha wala hela!

Inasemekana walitaka kutudhoofisha katika harakati za ukombozi kusini mwa Afrika, wakajua tusipopewa silaha Idd Amini angetupa kibano kikali, akishirikiana na Gadafi wa Libya. Hivyo inawezekana kabisa Afrika Kusini ilikuwa na mchango katika Tanzania kukataliwa kuuziwa silaha na nchi tajiri kwa ajili ya vita vya Kagera.

Ila Museveni asisahau kwamba kushirikishwa kwa Umoja wa kuikomboa Uganda kuipeleka vita ndani ya Uganda halikuwa suala la sisi kushindwa au kutokuwa na uwezo. Baada ya kumowondoa Idd Amini eneo la Tanzania alilovamia, jeshi la Tanzania liliambiwa lisimame kwanza mpakani kabla ya kuingia Uganda, kwa sababu Nyerere alisema kama tungeingia Uganda bila vikosi vya Uganda ingekuwa uvamizi na katika sheria za kimataifa isingekubalika. Hivyo mkutano wa haraka haraka ulifanyika Moshi nadhani, kina Museveni wakaitwa wakaambiwa waunde umoja wa kuikomboa Uganda ili upigane bega kwa bega na majeshi ya Tanzania ndani ya Uganda. Hiyo ingeondoa shutuma kwamba jeshi la kigeni la Tanzania lilikuwa limevamia Uganda. Ilibidi JWTZ wasubiri na wasimamishe vita mpaka umoja huo wa Uganda uundwe, viongozi wake wachaguliwe ndipo vita ikaendelea kwa awamu ya pili, ambayo ikawa ni kumuondoa Idd Amin. Lakini ukweli ni kwamba jeshi la umoja wa kuikomboa Uganda, kina Museveni, walikuwapo kama ushahidi tu, wala hawakuja na silaha. Vita yote ilipiganwa na JWTZ Tanzania. Museveni, mwanasheria, angefanya nini wakati huo? Alikuwa anapiga domo tu, mbishi kama nini. Sintashangaa mtu kama Paul Kagame kwamba alikuwa katika jeshi la umoja wa kuikomboa Uganda. Lakini kuwapo kwa Kagame haimpi haki Museveni kusema Rwanda ilishiriki kumwondoa Idd Amin. Itakuwa Museveni anazeeka vibaya.

Nyerere alikuwa na busara sana. Hivyo aliiepusha Tanzania na shutuma za Umoja wa Mataifa kuwa tumevamia Uganda kwa akili sana. Kumbuka hawa wenye kura za veto Umoja wa Mataifa ndio waliokataa kutupa au kuuzia silaha za kumpiga Amini.
 
Sio kweli hilo mm na bisha kwa asilimia75% Tanzania ndio iliyo fukuza nduli..n 20% wananchi na 5% hao wengine wapambe
Naukiangalia Idd Amini alikua rafiki kipenzi wa Gaddafi..sababu ya Uislam alimpa marcernalies ambao baadhi yao walitekwa na jeshi la Tz
 
hiyo hotuba aliyoitoa rais mseveni wa uganda kuwa tanzania haikuondoa madarani idd Amin hivyo ni vichekesho kwani idd Amini alipoiangusha serikali ya uganda iliyokuwa chini ya rais obote utawala wa ngazi za juu asilimia kubwa wakikimbilia tanzania wakiongozwa na rais milton obote na aliyekuwa mkuu wa majeshi ,alikuwepo luteni kanali mseven,luteni kanali ojokwu na civ paul mwanga na wengine ambao walikuwa ni walinzi wa wakubwa,katika hali hiyo intelejensia ya idd Amin ilijua wazi kuwa wabaya wake wote wako tanzania pakawepo na chokochoko katika mpaka wetu na uganda wa mara kwa mara hadi kupelekea kuingia vitani awamu kwanza mwaka 1972 lakini vita hivyo ambavyo viliisha ambapo askari wetu wakiigia ndani ya ardhi ya uganda sehemu za mbalala na masaka hatimaye vita hivyo vikamalizika,lakini choko choko hiyo haijuishia hapo kwani hadi mda huo serikali ikawa imeshajua kwamba mpaka wetu na uganda haupo salama jeshi letu likawa tayari muda wote na hatimaye mwaka 1978 oct yakawa yametimia kwa kipindi kile jeshi letu lilikuwa dogo baadhi ya askari wetu walikuwa nje ya nchi kweye nchi ambazo zilikuwa zinadai uhuru kama msumbiji,zimbabwe,Namibia lakini nguvu kubwa ulikuwa msumbiji,‘pindi Amin alivyovamia tanzania jeshi letu likawa na kazi awamu ya kwanza ni kumzuia adui asiedelee kuingia ndani ya ardhi yetu lakini kwa sababu alikuwa amejiandaa kwa uvamizi huo akikamata maeneo ya ardhi yetu hadi mto kagera na akavunja daraja na kujitangazia hapo ndi mwisho wa mpaka wake eneo lote la kyaka,na rais wetu akaitangazia dunia kwa uvamizi huo wa uganda kwenye ardhi yetu,hatimaye makamanda wakakaa na kufanya mipango ya vita ambayo ilikuwa ni ya lazima,mkuu wa majeshi wa mda huo major general twalipo na mabriged commd wote na maafisa wote wa ngazi za juu waliokuwa nje ya jeshi akina brugedia mayunga ambaye alikuwa mkuu wa mkoa singida wote alikaa na kutafakari vita hivyo wakiwemo akimbizi wa kijeshi wa uganda kanali Tito okello,luteni kanali ojokwu,luteni kanali mseveni,piul mwanga,wakati huo jeshi linafanya maandalizi ya kupanua jeshi lake ambapo askari mgambo wote wakiitwa kama sera yetu ilivyowazi kuwa ni jeshi la akiba ,wakachukuliw baadhi ya askari polisi na magereza wote wakapewa training ya mda mfupi na kuelekea vitani,hoja ya mseveni kweli tulikuwa naye vitani lakini hakuwa na kikosi au watu aliowaongoza vitani ila kwenye uwanja wa mapigano alikuwepo kama mwenyeji wa nchi husika na kutupa uhauri,na hilo swala kwamba palikuwa na nchi au marais wanne hiyo inaweza kuwa sawa na hali halisi huwezi ukapigana vita na ukashinda hila msaada,kuna nchi zilijitokeza kutusaudia kijeshi lakini mwl alikataa ila akikubaliana na vifaa japokuwa rais wa msumbiji alipinga mawazo ya mwalimu bado alileta wanajeshi wake kwa nguvu na kuwaomba makamanda mapungufu waliyonayo katika medani ili ayazibe haraka sana makamanda wakamweleza mapungufu hayo na akayafanyia kazi akatuma kikundi cha artilary ambacho kilileta history uganda hadi leo ,na hao walikuja kwa niaba ya tanzania siyo uganda,baada ya idd amini kuondoka madarakani pakaanzishwa mafunzo kwa kuunda jeshi ambalo liliitwa UNLAna chama chama chao UNLF
 
wakati vita imeisha nakuundwa serikali ya mda ambaye akikuwa rais wa muda yusuph Rule akawa rais mda baada muda pakatokea mgogoro ambao rule akaondoshe akaingia godfrey binaisa naye akaondoshwa kisa mseveni alikuwa akitaka madaraka wakati huo alikuwa ameanzisha kundi la uasi ambalo aliita NRA ambalo liliendesha vita vya chini chini hadi ikapelekea mzee obote apinduliwe na mkuu wavmajeshi tito ikello kwa lengo labda mseven atatulia lakini wapi aliendeleza mashambulizi mpaka mzee tito okello naye akakimbia hapo ndo mseveni alipochukua madaraka kwa mara kwanza hadi leo lakini ubavu wa kumtoa idd amin kawatoa hao wengine ambao hawakuwa na jeshi!
 
Nimemsikia Rais wa Uganda Ndugu Mseven akiwataja kama Marais wengine watatu pamoja na Nyerere akiwashukuru kwa vita ya ukombozi ya kumng'oa Idd Amin.

Hii ni tofauti na ambavyo tumekuwa tukiaminishwa kuwa Tanzania pekee ndiyo iliyomng'oa nduli.

Sasa ninawekea mashaka vitabu vyetu vya historia. Je huu ndio ukweli?
Huyo museveni na kikosi cha waganda waliokuwa exile walisaidia kwenye undercover role zaidi....offensive combative role...ilibaki kwa...Tanzania na hususani TPDF
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom