Museveni apasua jipu, Tanzania haikumng'oa Idd Amin peke yake!

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,658
15,784
Nimemsikia Rais wa Uganda Ndugu Mseven akiwataja kama Marais wengine watatu pamoja na Nyerere akiwashukuru kwa vita ya ukombozi ya kumng'oa Idd Amin.

Hii ni tofauti na ambavyo tumekuwa tukiaminishwa kuwa Tanzania pekee ndiyo iliyomng'oa nduli.

Sasa ninawekea mashaka vitabu vyetu vya historia. Je huu ndio ukweli?
 
Nimemsikia Rais wa Uganda Ndugu Mseven akiwataja kama Marais wengine watatu pamoja na Nyerere akiwashukuru kwa vita ya ukombozi ya kumng'oa Idd Amin.
Tofauti na ambavyo tumekuwa tukiaminishwa kuwa Tanzania pekee ndiyo iliyomng'oa nduli.
Sasa ninawekea mashaka vitabu vyetu vya historia kwa uongo huu uliotukuka.
Hongera M7 kwa kutuambia ukweli.
Em sema/weka kile ulichosikia Mseveni akisema, na tutajie hao maraisi watatu aliowasema
 
Nimemsikia Rais wa Uganda Ndugu Mseven akiwataja kama Marais wengine watatu pamoja na Nyerere akiwashukuru kwa vita ya ukombozi ya kumng'oa Idd Amin.
Tofauti na ambavyo tumekuwa tukiaminishwa kuwa Tanzania pekee ndiyo iliyomng'oa nduli.
Sasa ninawekea mashaka vitabu vyetu vya historia kwa uongo huu uliotukuka.
Hongera M7 kwa kutuambia ukweli.
Hata hili nalo unataka kutuletea ubishi?
Duniani kote ukweli unajulikana kwamba JWTZ ndio waliomng'oa nduli Amin
Leo Mseven ndo amekwangua ukweli wote kichwani mwako na unataka kutuingiza kwenye mjadala hewa
Yeye mwenyewe hapo alipo anajua fika kwamba TZ ndio iliyompa urais miaka ile ...!!! ndio !!! kama ulikuwa hujui basi chukua hiyo.......!!!
 
Nimemsikia Rais wa Uganda Ndugu Mseven akiwataja kama Marais wengine watatu pamoja na Nyerere akiwashukuru kwa vita ya ukombozi ya kumng'oa Idd Amin.

Hii ni tofauti na ambavyo tumekuwa tukiaminishwa kuwa Tanzania pekee ndiyo iliyomng'oa nduli.

Sasa ninawekea mashaka vitabu vyetu vya historia. Je huu ndio ukweli?
vitabu vyetu havikusema ukweli wote kuhusu amini hata sababu za sisi kuingia vitani hazikusemwa wazi
 
Maadam wewe umesikia embu tutajie hao marais na maelezo mengine,mimi siwezi kumfundisha pia mwanangu nusunusu kama ulivyoleta hapa
Nimemsikia Rais wa Uganda Ndugu Mseven akiwataja kama Marais wengine watatu pamoja na Nyerere akiwashukuru kwa vita ya ukombozi ya kumng'oa Idd Amin.

Hii ni tofauti na ambavyo tumekuwa tukiaminishwa kuwa Tanzania pekee ndiyo iliyomng'oa nduli.

Sasa ninawekea mashaka vitabu vyetu vya historia. Je huu ndio ukweli?
 
ila serikali yetu imeaniacha hoi kumpeleka katika kiwanda cha bakhresa badala ya kumpeleka katika viwanda vilivyo chini ya serikali, nimeshindwa kuelewa imekaaje hii, labda wadau mudadavue
Hatuna kiwanda kikubwa cha serikali tunachoweza kujivunia
 
Nijuavyo mimi ni kuwa vita vya kagera ndivyo vilivyomtoa Idd Amin Dada madarakani mengine hayo siyajui
 
Nichumu Nibebike,

..Tz tulikuwa na washirika wetu ktk vita dhidi ya Iddi Amin.

..Kwa mfano Algeria walitupatia silaha.

..Msumbiji walituma kikosi kilichopigana bega kwa bega na JWTZ.

..pia walikuwepo askari wakimbizi wa Uganda ambao walipigana pamoja na Watanzania. Askari hao ndiyo waliokwenda kuanzisha jeshi jipya la Uganda baada ya Amin kukimbia.

..lakini pamoja na msaada huo, mtu yeyote mwenye uelewa wa masuala ya vita atakueleza kwamba Iddi Amin alipinduliwa na majeshi ya Tanzania.

NB.

..Amini naye alikuwa na washirika wake, mkubwa kuliko wote alikuwa ni Muamar Gaddafi.

..kama tusinge mtwanga Gaddafi ktk mji unaitwa Lukaya huenda historia ingekuwa siyo hii tunayoizungumzia leo.

..lakini wako waTz limbukeni wa historia yetu wanamtukuza na kumlilia Gaddafi.
 
Historia tanzania wameharibu siijui kwanini maana majuzi bungeni wakati wanapanga kuhusiana na kudai ujerumani fidia juu ya maji maji ndipo nikasikia kinjiketile sio kiongozi wa hiyo vita na Pia wakataja sehemu ambazo zilianzia duh nilichoka
 
Back
Top Bottom