Musa,Hamis,Juma na Rose kua mbunge au rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Musa,Hamis,Juma na Rose kua mbunge au rais

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by raffiki, Oct 17, 2011.

 1. r

  raffiki Senior Member

  #1
  Oct 17, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashawishika kuamini humu great thinkers ni wachache,ila kuna makundi ya watu yanayopigia chapuo watu wao kisiasa. Post zimekua ni za majina ya watu badala ya hoja za kichama au kitaifa.,asubuhi utasikia musa tunamkubali bila hata alilofanya kwa taifa hata chama chake,mchana utasikia siri nzito ya rose, jioni 2015 ni ya Juma...tukiamka kesho Hamis namkubali anakila sifa ya kua kiongozi ameweza anathubutu...jiulize sasa anathubutu nini eti kuongea magazetini na majukwaani wakati umeme taabu,maji shida,kazi hakuna,mikopo wanafunzi wanalia, vijinini kwetu hali ngumu na mengi mnayajua bana...Na tena angalia vizuri wachangiaji wakusupport post hizo za watu ni wale wale utaona Mangi232, mara rafikki1, mara popo sijui popoo. JAMANI maneno ya wazee yanabusara hata kama wanamakosa mkapa,kikwete,butiku na warioba wamesema vijana tufanye kazi tusikazane na mbwembwe za siasa majukwani na fitina za kimaslahi tunaliua taifa letu. Angalia utashia kua masikini siku nzima unakesha una post na kumbe wenzio wanaopost majina yao maana ndio mtaji wao wa maisha wangekua wanadhubutu au kuweza si wangeweza kwingine bila kua viongozi mbona kutwa vijembe na mashindano ya nani mkali na nani anapata publicity kubwa. What's hell is this???. Hata mwalimu alipigania haki na wengine walimsupport sasa sisi kila kijana sasa anataka yeye ndiye awe mpigania haki na hataki kumsupport mwingine...kuna kitu hapo?jiulize.

  Wanaofaa wametulia sana tuu kwa taarifa yenu na wapo humo humo CCM na CDM.

  Tujadilini hoja za taifa bwana na sio majina ya watu banaa kha mnabore sasaa.

  Source:political analyst.
   
 2. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  magreat thinker tupo wa 5 tu humu
   
 3. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Umekosea, ! Great thinker ni wewe tuu.
   
 4. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,159
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Raffiki hapo kwenye red sikubaliani na wewe. Watakaoua taifa sio vijana na hao akina Mkapa, Kikwete etc waliokosa uzalendo kwa taifa lao. Wanagawa maliasili zetu halafu wanajifanya manabii. Upuuzi mtupu.

  Hebu jiulize unawaambie vijana wafanye kazi, ni kazi gani hiyo unayotaka waifanye kwa uchumi wetu huu. Wameua viwanda vyote, mazao yetu hayana soko na hata yenye soko wanunuzi ndio wanaotupangia bei, tena wanayopenda wao, wakileta bidhaa zao weneyewe kama vile pembejeo wao ndio wanaopanga bei. Mkapa, Kikwete na hata Warioba wanataka tufanye kazi....nani huyo tumfanyie kazi ili aendelee kutunyonya. Ni bora vijana wasifanye kazi.

  Waondoke hapa na unafiki wao na wewe mleta mada next time uwe great thinker sio unapost post tu upuuzi na uelewe kuwa si kila mzee ana hekima.
   
 5. r

  raffiki Senior Member

  #5
  Oct 17, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakubaliana na wewe asilimia 50 kwamba ni kweli juhudi za vijana kufanya kazi zimekua zikirudishwa nyuma na baadhi ya watu na viongozi kama ulivyoainisha hapo juu,lakini nikefahamishe ndugu yangu kuwa kila mwanadamu anamapungufu yake,hilo lazima uelewe hatujawa malaika sie bado ni binadamu, pili kuwa kiongozi mfano position ya rais..kuna matatizo au ufujaji wa rasilimali ambao unatokea bila presidential will, na ni mwingi tu so hauwezi kufukuza au kufunga kila siku,,hii najumuisha pia kama kiongozi una ndugu na rafiki ,tuwe wakweli nao wanamatatizo yao sasa leo hii wewe uwe rais na kuna ndugu na jamaa wengi tu wanafanya visivyo hasa kwa dunia ya sasa ya utandawazi utawafunga tuu????tujaribu kuwa realistic ok?? Anyway naweza kukujibu sn niishie hapo pengine umenielewa..nije kwenye asilimia 50 nisizokubaliana na wewe..na hoja yangu hapo ni kuwa je inamaana kama viongozi wetu uliowataja wananamapungufu yao basi na vijana ndio tukae chini kwa kulalamalalama tu tena kwa majina??????tunafuga ugonjwa au tunatibu????na hapo hapo uwe unakua great thinker sio kujibu bila kuchanganua akili yako.
   
 6. THK DJAYZZ

  THK DJAYZZ JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Khaaa...!!! What this ?
   
 7. S

  SIKUOGOPI Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baba Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliondoka Chama Chake CCM. Maana sioni lolote alilofanya Mkapa na Kikwete tena Baada ya Baba Kufa Hawa watoto aliowaacha ndo wamekuwa Majangili wezi na Majambazi wasio na Aibu!

  Ushahidi unadhihirika kwa CCM kuanza kuraruana mara utasikia LOWASA, ROSTAM,CHENGE ni Mafisadi. kesho SITTA,MWAKYEMBE,MWANDOSYA wameandaliwa kuuwawa kwa Sumu! Kwa sababu ya Kutokukubaliana na Uozo wa Chama.

  Jioni utasikia WABUNGE BAADHI WA CCM WAKANUSHA KUPIGA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA RAIS Kikwete. Ukiuliza sababu eti kadharau Mhimili wa Bunge! Kwa Jairo Kurejea Kazini Baada ya Kauli ya PM Pinda Kudharauliwa na Rais.

  Usiku wa Manane MABOMU GONGO LA MBOTO YAMELIPUKA achilia Mbali ya Mbagala Lakini ukifuatilia kwa Baadhi yao wanalalamika Wakiomba Pesa kwa ajili ya Ulipuaji salama hawapewi na Badala yake wakubwa Wanagawana kwa Njia Mbadala bila wadogo kuhusishwa juu ya Matumizi Hayo.

  Asubuhi utaambiwa Tumetumia Mabilioni ya Fedha kwa ajili ya Shughuli za Mwenge, Vikao ,Posho, Magari ya Rais,Ukarabati wa Ikulu, ooh Marufuku wananchi Kuhoji Kazi na Matumizi ya Usalama wa Taifa.

  Mchana Wawekezaji kwenye Migodi wameondoka na Changa wetu ghafla utasikia
  Sekta ya Madini inaliingizia Taifa Fedha za Kigeni nyingi tu ghafla Ooh Wawekezaji wapewe Miaka Mitano kwanza ya Majaribio.

  Alasiri wanafunzi wamegoma Fedha hazitoshi
  ghafla Kawambwa kafika Kutuliza na V8 ya Milioni Mia Mbili na Sabini utasikia akisema Serikali Kwa sasa Haina Pesa! eeh Jamani FFU
  wameanza Kumwaga Maji ya Pilipili ukiuliza Wanafunzi Hawaelewi somo!

  Jioni Waziri Mkuu Mstaafu tena mwenye Heshima anaongea Utumbo utasikia Luningani Vijana Hawawajibiki. Gari anayotumia yeye tu na Posho anayolipwa kama Staafu MWAKA MZIMA anaweza Kulipa Wazee wa EAST AFRICA! Wanaoleta Laana ya Nchi kwa Kuvua Nguo!

  Usiku Yuleyule aliecha Ubunge kwa Siasa Uchwara za CCM anampigia Kampeni Kafumu

  WARIOBA, ACHA KUROPOKA KWA SHIBE YA MUDA! Vijana unaotaka wawajibike ni Akina nani ?. Maana watoto wenu na wajomba zenu tu ndio Mmewapa kuwajibika sisi wengine Mmetuacha eti Hatupo kwenye Mtandao! Anza na Fisadi Ridhiwani kwanza ndipo uendelee na wengine! Kulalama Hatutaacha Maana Ninyi Wazee ni Wasanii na
  mnatufanya sisi ni Mazuzu sana! Siku yenu inakuja tena iko Mapema sana! 2015!
   
 8. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Acha utani! kwahiyo tuwaache mbadilishane mawazo wenyewe watano au? Hata hivyo basi kama mko watano na mmeshindwa kubadilisha waliobakia nina wasiwasi na upeo wenu wa akili! Maana mjinga siku zote hujifunza kwa anayejua na siyo anayejua kujifunza ka asiyejua, hivyo mna kazi kubwa ya kutuonyesha njia tufanane na nyie. Ni watu wachache sana wanaojia kazi ya chumvi, ukiuliza wengine watakuambia ni kukoleza, wengine kuwekw ladha nk. Lakini kazi ya chumvi ni kuharibu au kubadilisha! Kutoa ladha halisi ya kitu husika na kukileta katika ladha ya chunvi, mf ukitaka kujua ladha halisi ya nyama ni uile bila chumvi, vivyohivyo ladha ya wali, maharage nk. Hivyo wali unaokula huwa una ladha ya chumvi na siyo ladha halisi ya wali, mnapaswa Great Thinker watano mnaojitambua mwe kama chumvi mtubadili tuwe na mawazo pevu kama nyie. Kinyume na hapo hapa kitakuwa kijiwe cha kahawa. Ila siamini kama mko watano tu huku!
   
Loading...