Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 10,884
- 18,824
Asili ya fisi huyu kuitwa Musa ni kwa vile siku moja alipojaribu kumkamata mwanamke aliyekuwa amelewa; bibi huyo alimdhani fisi ni mumewe aitwaye Musa, hata akamwita kwa sauti kuu, “Musa Musa! Bwana wangu silewi tena, bwana! Usiniadhibu namna hii, kwanza makucha yako leo makali bwana.” Basi watu walipokwenda kutazama ugomvi huu wa Musa na mkewe wakamkuta yule fisi akijaribu kumvutia yule bibi mlevi maporini. Basi tangu siku hiyo fisi huyo akaitwa Musa.
Basi siku nyingine fisi huyo hupata akalia usiku katika kijiji cha Mikwanga. Wenyeji wa kijiji wakimsikia humjibu kwa maneno haya: “Musa! Musa! Bure wajisumbua, mpenzi wako halewi siku hizi heri uende zako ukamtafute mchumba mwingine.”