gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,305
- 3,327
Nimezunguka vijijini maeneo mengi mikoani hali ya ukame imesababisha madhara makubwa kwa wananchi hasa wakulima na wafugaji.
Ng'ombe wamekufa na wanaendelea kufa ma elfu kwa maelfu kwakukosa malisho kutokana na ukame unaondelea nchini jambo ambalo limesababisha baadhi ya wafugaji kuwa masikini.
Njaa imetamalaki kwa wananchi kutokana na kukosa mavuno kwasababu ya ukosefu wa mvua.
Natambua tatizo hili ni kubwa na haliwezi kuondolewa kwa miti 200 ninayofikiri kujitolea kuipanda kandokando mwa Morogoro road ila naamini inaweza kuwa chachu kwa wengine kuendeleza zoezi hili.
Japo TMA wametangaza mwaka huu kutakua na uhaba wa mvua ila nimefikiri kuanza maandalizi mapema kuanzia mwezi wa pili kama kuchimba mashimo na kuweka mbolea na kisha nitasubiri msimu wa mvua hapo mwezi wa tatu mwaka huu kisha nitaipanda.
Naomba kwa mwenye kufahamu kama sheria ya tan road itanibana ikiwa nitaipanda miti hiii kando kando mwa morogoro road ili iwe kichocheo cha kupanda miti zaidi kwa wasafiri watakao tumia Morogoro road.