Muongozo na vyuo vya kujiunga kwa ngazi ya Ualimu Stashahada

SAKA25

Member
Jul 15, 2021
12
22
UTANGULIZI
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu kwa ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari. Waombaji wa mafunzo haya ni wahitimu wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III). Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.

SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU
Sifa za jumla za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekodari ni wahitimu wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha “Principal Pass” mbili (02) za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari kidato cha I-IV. Aidha kwa waombaji ambao moja ya “Principal Pass”mbili ni somo la Uchumi “Economics”, wanaweza kuomba kozi za fani ambazo ni Michezo (Physical Education and sports), Muziki, Sanaa za Ufundi (Fine Arts), na Sanaa za Maonesho (Theatre and Performing Arts).

AINA YA MAFUNZO NA SIFA
Jedwali lifuatalo linaonesha aina ya mafunzo ya Ualimu, sifa za kujiunga, vyuo vinavyotoa mafunzo hayo na muda wa mafunzo
  1. MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA SEKONDARI
NaAINA YA MAFUNZO SIFA ZA KUJIUNGA CHUOMUDA WA MAFUNZO


1


Stashahada ya Ualimu Sayansi na Hisabati
Ufaulu wa Kidato cha VI kwa kiwango cha Daraja la I-III na alama zisizopungua ‘Principal Pass’ mbili katika masomo ya Tahasusi za Sayansi, Hisabati na TEHAMA kwa kuzingatia Masomo yanayofundishwa katika shule za Sekondari kama ifuatavyo: Basic Mathematics, Biology,Food &nutrition , Geography, Chemistry, Physics, Agricultural Science, Information and Computer Studies (ICS) na Computer Science.Monduli TC, Mandaka TC, Butimba TC, Kleruu TC, Songea TC, Tukuyu TC, Kasulu TC, Mpwapwa TC, Morogoro TC, Korogwe TC, Tabora TC
Miaka 2
2

Stashahada ya Sayansi ya Jamii , Biashara na Lugha
Ufaulu wa Kidato cha VI kwa kiwango cha Daraja la I-III na alama zisizopungua ‘Principal Pass’ mbili kwa kuzingatia masomo yanayofundishwa katika shule za Sekondari Kidato cha I-IV. Masomo yanayofundishwa katika shule za Sekondari kidato cha I-IV ni : Kiswahili, English, History, Geography, Civics, Commerce na Book keeping.Bunda TC,
Mtwara (K) TC,
Marangu TC, Nachingwea TC, Shinyanga TC, Mandaka TC, Mpuguso TC, Dakawa TC, Butimba TC,
Tabora TC,
Morogoro TC, Tarime TC,



Miaka 2
3







Stashahada ya Ualimu Michezo, Muziki, Sanaa za Ufundi na Sanaa za Maonesho
Ufaulu wa Kidato cha VI kwa kiwango cha Daraja la I-III na alama zisizopungua ‘Principal Pass’ mbili pamoja na ufaulu wa masomo yaliyoainishwa katika mtihani wa kidato cha IV kwa kila kozi kama ifuatavyo:
(a) Sanaa za Ufundi: masomo ya Fine Arts , Basic Mathematics, Chemistry, History, Physics, English na Civil Engineering.Butimba TC
Miaka 2
(b) Sanaa za Maonesho: masomo ya English, Literature in English, Kiswahili, Geography na History.Butimba TC
Miaka 2
(c) Muziki: masomo ya ‘Music’ pamoja na masomo ya English, Kiswahili, Physics, Geography, History na Biology.Butimba TC
Miaka 2
(d) Elimu kwa Michezo: masomo ya Physical Education and sports, Languages, na Biology.Butimba TC na Mtwara (K)Miaka 2




  1. MAFUNZO YA UALIMU KAZINI (STASHAHADA ELIMU YA SEKONDARI)

Na.AINA YA MAFUNZOSIFA ZA KUJIUNGACHUOMUDA WA MAFUNZO

1

Stashahada ya Elimu Maalum
Mwalimu kazini aliyepitia mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada au Shahada mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu usiopungua miaka 2; na awe amefaulu masomo ya Sayansi katika mtihani wa Kidato cha SitaPatandi TCMiaka 2

UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI

  • Tangazo hili linawahusu wahitimu wa kidato cha sita waliohitimu kuanzia mwaka 2015 hadi 2021;
  • Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Ualimu vya Serikali wanatakiwa kujisajili na kufanya maombi kupitia tovuti (tcm.moe.go.tz);
  • Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu kwa vyuo visivyo vya Serikali watume maombi yao katika vyuo wanavyotaka kusoma na vyuo husika viwasilishe sifa za waombaji Baraza la Mitihani Tanzania kwa uhakiki;
  • Waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali watachagua tahasusi hadi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi;
  • Waombaji wa nafasi za mafunzo walio kazini wanapaswa kuwa wamehitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada au Shahada;
  • Walimu Kazini watapaswa kuambatisha barua ya ruhusa kutoka kwa waajiri wao;
  • Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu kwa Vyuo vya Ualimu Vya Serikali yatatolewa kupitia “account” aliyotumia mwombaji kuomba mafunzo ya Ualimu kuanzia tarehe 03/08/2021 na katika Vyuo walivyochaguliwa;
  • Barua na fomu za kujiunga na Mafunzo zitatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (moe.go.tz) na Chuo atakachopangiwa mwombaji kwa kutumia anuani yake. Waombaji wote wanashauriwa kuandika anuani kamili, barua pepe na namba ya simu inayopatikana kwa mawasiliano zaidi;
  • Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 01/08/2021;
Tanbihi: Masomo ya Dini hayatatumika kama kigezo cha sifa ya kujiunga na Mafunzo ya Ualimu.


pdf.png
TANGAZO LA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA Y...
 
Back
Top Bottom