Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Video ya mwongoza watalii huyo, ilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita, na kuzua taharuki katika sekta ya Utalii nchini,huku wadau wengi wakitaka asakwe na kukamatwa.
Katika video hiyo, mtalii huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja, anaonekana akisema safari yake nchini Tanzania imekuwa nzuri na watanzania aliokutana nao walikuwa ni watu wenye upendo.
Akizungumza na gazeti hili kwa simu leo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alisema mara baada ya kuona video hiyo kwenye mitandao aliagiza akamatwe mara moja.
“Nilitoa maagizo jana (juzi) usiku atafutwe na akamatwe na taarifa nilizopewa leo ni kuwa ameshakamatwa kwenye gate (lango) la Nabi Serengeti na yuko rumande kule Mugumu”alisema.
Chanzo: Mwananchi