Muone mtoto wa ajabu anayejua hesabu

NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
10,971
2,000
Inshallah uyo dogo aje kuwa prof. Kabudi wa baadae kulitumikia taifa.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,450
2,000
Waziri wa sayansi technolojia na elimu ya juu kuna mtoto anaitwa Charles Matias anasoma chekechea katika shule ya msingi Nyingwa na kuna video yake inatembea mitandaoni akionyesha uwezo mkubwa sana wa kufanya hesabu kichwani za kikubwa.

Hiki ni kipaji na huyu mtoto ana brain ambayo kwa wataalamu wa kompyuta wanasema ana processor yenye high speed.

mimi napendekeza mtoto huyu afundishwe hesabu tu na kwa uwezo alionao kwenye hesabu akifikisha miaka 12 mpaka 14 atakuwa na uwezo wa kuingia chuo kikuu kuchukua masomo ya hesabu.

kwa trend kama hiyo kipaji chake kinaweza kuwa na faida kubwa kwa taifa letu kwani serikali ikiwekeza kwake atakuja kuitangaza vyema sana nchi yetu.

 

Mzingo

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
2,114
2,000
Afuate utaratibu wa kawaida yasijejirudia ya Bethuel Mbugua wa Kenya. Anajuta.
 

Kaka pembe

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
633
1,000
Tatizo walimu wenye stress watakiua kipaji. Huyo inabidi ajengewe mazingira ya kuamini kuwa duniani somo ni hesabu tu.

Akianza kuingiziwa historia mpya pamoja na historia za zamani, kwisha habari yake.

Needs a special teacher.
 

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
9,780
2,000
Hawa madogo wanaishiaga kusikojulikana, mmenikumbusha yule Jiniazi wa Kenya.

Sasa huyo Waziri mnamuita asaidie nini?
 

Teenager

JF-Expert Member
Jun 28, 2020
1,807
2,000
That's great.
Kuhusu kupelekwa secondary ni bado sana.

Mdogo wangu anafanya zaidi yake ila tofauti ni kwamba mimi namfundisha na walimu wake wanamfundisha.

Hapo kwenye kujifunza mwenyewe bila chanzo ni ngumu kuamini.
Lazima kutakuwa na mtu yupo nyuma yake.
 

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,450
2,000
Afuate utaratibu wa kawaida yasijejirudia ya Bethuel Mbugua wa Kenya. Anajuta.
Shida iliyopo kwenye jamii zetu ni watu kama hawa kuwaacha na kusubiri wao watakuja kuibuka na kitu gani wenyewe.

huyu mtoto ukimfundisha hesabu tu ana uwezo wa kujiunga na chuo kikuu katika umri mdogo sana ambao duniani kote huyo mtoto anakuwa habari.

Uwezo alionao ni dhahiri akiendelezwa vizuri katika somo la hesabu atapata attention ya dunia na hiyo itatangaza nchi yetu sana.

wenzetu watu kama hawa hawaachi na kuwatazama wenyewe wataibuka na nini bali wakiona potential kama hiyo ya mtoto wanatafuta wamuendeleze vipi ili awe faida kwa taifa
 

Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,785
2,000
Quantum physics,quantum computing,Data science,AI hivi vitu ndio habari ya mjini dunia nzima na ndio pesa ilipo achaneni na mathematics. Mathematics haina dili zaidi ya kuwa mwalimu. Angekuwa kijiji nachofundisha ningeanza kumpa misingi ya science bila kufuata mtaala fake wa kuzeeshana.
 
Aug 13, 2020
11
45
Kwa kweli ni kipaji kizuri Sana ambacho Mungu kaweka ndani yake kwa umri wake kwa hesabu hizo za kujumlisha na kutoa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom