Number ni 26
JF-Expert Member
- Apr 3, 2019
- 1,478
- 2,836
Once again leo tupeane hints kidogo kuhusu hatima ya maisha yetu. Katika maisha tunayoishi wanadamu hasa vijana, tunakutana na vipengele vingi kiasi kwamba mtu hadi anagonga 40 bricks ngoma bila bila.
Mimi Number ni 26 na wewe kijana mwenzangu ambae upo kwenye 20's, 30's na kidogo wewe wa 40's. Hakikisha unapouanza mwaka wako wa 50 basi uwe na uhakika wa kupata vitu hivi bila wasiwasi ili umalize salama uzee wako na sio uishie kuchukia watu
1. Uwe na afya njema/bora
Huu ndo mtaji wa kuyafikia mengine yote, kama huna afya njema/bora tegemea kuanguka katika mengine.
2. Uhakika wa matibabu bora
Kijana pambana katika kipindi hiki ili unapouanza mwaka wako wa 50 basi uwe na uhakika wa kupata matibabu sahihi na ya uhakika pale utakapoumwa au kupata itilafu itakayoitaji utibiwe
3. Uhakika wa chakula
Kijana kaza sana ili ukiianza hiyo age uwe na uwezo wa kugonga menu yoyote na wakati wowote bila wasiwasi. Na sio ule kile kitakachopatikana, kwakweli utazeeka mapema ndugu
4. Pesa ya dharula
Kijana pambana kuiweka hii pesa iwe ndani au popote pale mradi ukiihitaji hata ngoma 8 usiku shwaaa unaipata hapo hapo. Ukianza sasa hadi unafika 50 hautakuwa na wasiwasi na kitu kinaitwa dharula.
5. Akiba benki
Hii wote tunaijua sina haja ya kuisemea sana, ila nikumbushie tu kuwa ukianza sasa kuweka akiba hata ya buku buku tu katika umri wako huo wa miaka 25, guess utakuwa wapi utakapogonga decades 5
6. Usafiri
Nadhani wote tunajua changamoto za usafiri wetu hasa mijini, sasa fikiria katika umri huo unavyogombea daladala na watoto wanakupiga vikumbo wanawahi siti af hawakupishi, utaishia kusema watoto wa sasa hawana adabu. Kijana hebu jitahidi katika umri huo umiliki chuma, basi hata ukikosa miliki pikipiki yako safi
7. Nyumba
Yes muhimu kumiliki mjengo wako hata wa vyumba viwili tu inatosha. Ujue ni raha sana kuishi kwako ubuguzwi na mtu sijui mambo ya kodi, mara zamu yako usafi . Yani umefika 50 bado umepanga mbona utawaona watu wabaya.
Hizi ni faharasa nimeona niwashirikishe vijana wenzangu maana na me nipo ndani ya hizo. Kama kuna zingine basi jazia hapo
Naomba kuwasilisha, niko pale nimeshika yangu Number ni 26. I'm out