Muombe msamaha uliyekosana naye. Tugange yajayo

Magema Jr

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
1,299
1,201
Uzi huu ni mahususi kwa wapendanao, Marafiki, na watu mbalimbali waliokwaruzana kwa namna moja au nyingine, kuombana msamaha, na kuwiana radhi.

Kumbuka jambo la kukoseana au kukwaruzana ni la kawaida sana katika maisha yetu ya kila siku. Lakini kuhifadhi maumivu moyoni huenda isiwe na faida sana katika maisha yetu.

Hivyo ni wakati sahihi sasa, wapendanao na watu wa karibu mbalimbali kuweza kumaliza tofauti zao hapa. Ushauri pia unatolewa buree.

Naanza mimi kuwasamehe wale woote waliowahi kunitoa nduki inbox!!😂😂, pia wale ninaotofautina nao katika mijadala mbalimbali tafadhali mniwie radhi ndugu zangu
 
Nasubiri kusoma misamaha ya waliokoseana..msiandike magazeti tasavali.
hahahaha ,tatzo hapa kila mtu anasubiri aone nani anaanza kuomba msamaha😂😂 bora mods wafunge tu uzi.ova😂😂
 
Kwa jinsi aliyonitendea yule kaka, Mungu anisamehe nimeshindwa kusahau na kumsamehe jamani.!

Mtu anakuua huku anakuchekea na simu anakupigia kabisa anakupigisha story mnacheeeeka, kumbe mkikata tu anaendelea kukukaangia sumu na convo yote za plan unakuja kuoneshwa, hujawahi mkosea chochote maskini, umekuwa rafiki mwema kwake maisha yako yote..!

Nipo tayari kumsamehe hata mtu nlomfumania mara 100 ila siyo yule muuaji baridi..!! Nimewasamehe wooote maishani mwangu kasoro yeye..!!

Ilifikia pahala kama ningepewa bastola nichague kati yake yeye na shetani, ningemchagua yeye..!
 
Noma sana.
 
Back
Top Bottom