Mungu tusaidie jahazi la CCM linazama mchana kweupe!

Kwa mtut yeyeto anayeshabikia ccm miaka hii lazima atakua na upungufu wa akilia labda uwe mtoto wa mukama au baba milaji
 
Dhambi wanazofanya viongozi wa CCM na ufirauni walioifanyia nchi hii hata shetani angeambiwa afanye hizo dhambi angeogopa, zinatisha, sidhani kama sala yako itasikilizwa na Mungu....

CCM ni sawa na sikio la kufa halisikii dawa, uthibitisho ni kitendo cha mtu ambaye angekinusuru chama wakati huu mgumu kaenda zake Malawi baada ya kurejea toka kwa Maximo

Mbona CCM inanyongwa na viongozi wake wenyewe, tena mchana kweupe. By the way Fisadi na Shetani nani mbaya zaidi? Labda Profesor Safari atanisaidia kwa hili.
 
Kuna wenye uchungu na CCM lakini katika top 10 Dr. Xavery Lwaitama hakosekani.. Ameshasema yeye hajalipia kadi yake ya uanachama CCM mpaka mafisadi waondoke.. Yaani anaomba 2015 CCM ipigwe chini ili mafisadi wote wahame.. Hape ndipo yeye ataenda kuilipia kadi yake..
Kama Mafilifili una uchungu wa kweli baci acha kulipia kadi yako..
 
Na mapinduzi yameanza mwezi huu na CCM itakufa mwezi huu.

Mkuu imeshakufa tayari,liliobaki ni tunasubiri siku maalum ya kuizika hapo 2015,ina maana harufu yote anayotoa marehemu CCM ya kuoza wewe haujajua tu ameshakufa?
 
matukio mengi ya ajabu yametokea mwezi wa tano. Hitler ,osama wote walithibitishwa kufa mwezi mei....... mwaka huu tunasubiria mazishi ya CCM
 
CCM kwaheri na si ya kuonana tena, sisi tumeanza kumshukuru Mungu kwa puputiko hilo la ccm!!!!!!!!!:target:
 
Mungu awasaidieje tena wakati ameshawapenda zaidi?
Ndio maana kasi imeongezeka ya kwenda kwa baba kwa njia ya kifo!!
 
Kauli muhimu sana wakati huu. Tutajivuna tukifanikiwa kuvuka kipindi hiki salama. Kinachotakiwa sasa ni umakini wa hali ya juu ili kufikia na kufanya maamuzi sahihi kwa kila jambo - kadiri inavyowezekana. Pungufu ya hapo, kuogelea kwaweza kuwashinda wengine maana maji ni marefu tulipo; uchumi mbaya, umasikini umezidi, maradhi, na hata ujinga kwa watu wengi na hasa watoto kutojua kusoma na kuandika enzi hiii...kipato cha familia kimeshuka, bei za bidhaa kupanda bila maelezo yakini. mfumuko wa bei nk. Kuna mahala tumekosea na tunahitaji kurekebisha mapema. Jazba haitatufikisha popote, na haina mshiko. Matafakuri yanaweza kutuokoa sasa na hata milele. Mungu aongeze hekima zake kwa wapenda maendeleo wote, kwa ushirikiano TUNAWEZA!!!
 
Kwa mtji wa kukumbatia UFISADI,

CCM sasa kumfia Kikwete mkononi hata kabla ya 2015. Si kipindi kirefu CCM kugeuka kuwa kama TLP. Watch this space na CDM kazi za kisayansi tunaendelea nazo zaidi!!

Twasubiri miujiza ya mwenyezi mungu ili tupate okoka katika lundo la kashfa na tuhuma mitaani na bungeni. Mie leo nimepata taabu kusikiliza mazungumzo ndani ya daladala toka Gongo la Mboto hadi Posta;

njia yote ni kukisema vibaya chama chetu tukipendacho CCM.

Ilikuwa ni kushindana kutoa msururu wa kashfa dhidi ya CCM kana kwamba chama chetu hakijafanya jambo lolote la maana kwa watanzania.

Ilibidi Tazara nishuke katika lile daladala nichukue bodaboda kwani uvumilivu ulikuwa mdogo, wasafiri hawana na neno zuri kwa CCM niipendayo.

Mungu toa nguvu kwa viongozi wetu waamuke na kufanya mageuzi ndani ya CCM ilu mvuto urudi kama enzi za mwalimu.

MUNGU SAIDIA CCM ili WATZ wafunguke warudi tena chamani
 
Kwa makusudi . Kikwete na rafiki yake .. Pinda wanachelewa kutoa uamuzi juu ya hawa mawaziri kujiuzulu ili wasikie wananchi wanavyomwaga ladhi.
 
mwenye macho haambiwi Tazama, mwenye sikio haambiwi sikia..
Nimetizama, nimesikia waheshimiwa wabunge katika kipindi chooote cha awamu hii bungeni...
Serikali yetu imeanikwa ya kutosha, wananchi wengi wamezidi kujua madudu yanayofanywa na viongozi wetu tuliowapa kura zetu..
Ndugu wananchi wezangu, Kwanzia leo mimi sio Mwanachama wa ccm tena, nimechoshwa na hali ya kutetea watu wachache ambao wanaitafuna nchi hii na kuiweka nchi pabaya..
Hichi kitendo cha Rais kusema " Huu ni upepo utapita" ni dharau, na kujiona kuwa yeye ndiye zaidi ya watanzania wote.

Wananchi wenzangu bado tuna miaka mitatu ya kutawaliwa na mtu ambaye hayupo serious na nchi yetu.fikiria tu hapa alipo hata tukimpiga chini kashatufikisha wapi....je, hiyo miaka mitatu nchi itakua wapi?
Serikali ya kiswaiba ndo impact zake hizo wandugu...NO ACCOUNTABILITY..
 
Hitimisho la kikao cha bunge leo limebainisha kuwa ccm inalinda na italinda kile inachodhani kuwa ni "sifa za kikwete" hata ikiwa ni kwa gharama ya kujinyonga. msingi wa hoja yangu upo kwenye ibara ya 8(1) (a), (b), (c) na (d). pia ibara ya 9(a)-(i).
pamoja na ripoti ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali kuweka wazi kuwa mawaziri wametusababishia hasara kubwa iliyotokana na uvunjwaji wa katiba kwenye ibara nilizozitaja hapo juu, bado waziri mkuu Pinda ameendelea kuruka sarakasi huku amevaa taulo, anatuimbia ngonjera tukiwa icu, anatusomea risala tukipiga miayo ya njaa. Anashuhudia mawaziri ambao yeye ni kiranja wao wakihujumu uchumi kwa dhamana tuliyowapa, na kung'ang'ania madaraka hayo, Pinda kajipinda kuwafundisha maprofesor kusoma, kuandika na kuhesabu!!!!!! mchezo mzima ni kutochukua hatua ili aje achukue hatua hizo kikwete iwe kwamba wengine wooooote wabaya including ccm isipokuwa mzuri pekee ashangiliwaye na wazee wa dar kwa kuchelewa kuutatua mgogoro baina ya serikali na madaktari!!!!! na sasa mawaziri wamebainika kututia hasara, wanadai kuwa sahihi kutuibia, na Pinda kajipiiiinda kusoma risala ya kuahirisha bunge, kanakwamba hakuna lililotokea ili hatimaye kikwete akiisha kwisha chelewa kwa kujizungusha aje kushangiliwa na wazee wa dar kwa kumiminiwa misifa kibao! Haya niambieni huo uzuri wa kikwete v/s ccm,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom