Mungu tusaidie jahazi la CCM linazama mchana kweupe!

MAFILILI

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,377
1,194
Twasubiri miujiza ya mwenyezi mungu ili tupate okoka katika lundo la kashfa na tuhuma mitaani na bungeni. Mie leo nimepata taabu kusikiliza mazungumzo ndani ya daladala toka Gongo la Mboto hadi Posta; njia yote ni kukisema vibaya chama chetu tukipendacho CCM. Ilikuwa ni kushindana kutoa msururu wa kashfa dhidi ya CCM kana kwamba chama chetu hakijafanya jambo lolote la maana kwa watanzania. Ilibidi Tazara nishuke katika lile daladala nichukue bodaboda kwani uvumilivu ulikuwa mdogo, wasafiri hawana na neno zuri kwa CCM niipendayo.

Mungu toa nguvu kwa viongozi wetu waamuke na kufanya mageuzi ndani ya CCM ilu mvuto urudi kama enzi za mwalimu.

MUNGU SAIDIA CCM ili WATZ wafunguke warudi tena chamani
 
Sio siku nyingi utaingia mtegoni tu. Hakuna kimbilio kaka na Usitukane mamba kabla hujavuka mto!!!
 
Mungu Saidia hili Janga liondoke haraka...

Every minute gone ndani ya hili jinamizi.., ni Janga la taifa
 
Bora umejionea wenyewe manake huwa huamini jinsi watu walivyochoka na chama chako
 
Watazama kama ilivyo zama Mv. BUKOBA Sorry kwa wale waliopoteza Ndugu na Jamaa!CCM Watakufa Natural Death which i think they deserve.

Myatake: "CCM YOU WILL NOT BE WHAT YOU DREAM BUT YOU WILL GET WHAT YOU DESERVE WHICH IS DEATH"
 
Ni vizuri pia akitoka kwenye mazishi ili kubalance strory pia aenda kwenye Wedding ya Zuma!
 
Twasubiri miujiza ya mwenyezi mungu ili tupate okoka katika lundo la kashfa na tuhuma mitaani na bungeni. Mie leo nimepata taabu kusikiliza mazungumzo ndani ya daladala toka Gongo la Mboto hadi Posta; njia yote ni kukisema vibaya chama chetu tukipendacho CCM. Ilikuwa ni kushindana kutoa msururu wa kashfa dhidi ya CCM kana kwamba chama chetu hakijafanya jambo lolote la maana kwa watanzania. Ilibidi Tazara nishuke katika lile daladala nichukue bodaboda kwani uvumilivu ulikuwa mdogo, wasafiri hawana na neno zuri kwa CCM niipendayo.

Mungu toa nguvu kwa viongozi wetu waamuke na kufanya mageuzi ndani ya CCM ilu mvuto urudi kama enzi za mwalimu.

MUNGU SAIDIA CCM ili WATZ wafunguke warudi tena chamani
Dhambi wanazofanya viongozi wa CCM na ufirauni walioifanyia nchi hii hata shetani angeambiwa afanye hizo dhambi angeogopa, zinatisha, sidhani kama sala yako itasikilizwa na Mungu....

CCM ni sawa na sikio la kufa halisikii dawa, uthibitisho ni kitendo cha mtu ambaye angekinusuru chama wakati huu mgumu kaenda zake Malawi baada ya kurejea toka kwa Maximo
 
MKUUU KWA SARA KILAKITU KINAWEZEKANA BUT MAPENZI YA MUNGU YATIMIe
 
Bye bye CCM!Mimi ningekuwa na uwezo wa kuongeza kitu kizito ili Jahazi lizame vizuri ningefanya hivyo!!!!
 
Hata Farao alikuwa na moyo mugumu kutii maagizo ya Mungu na Serikali ya sasa imefanywa kuwa na miyo migumu ili Inguke
 
Hivi wewe uliyeleta mada hii utafunguka lini? aliyekuambia CCM kama haitakuwepo maisha hayaendi ni nani. Yawezekana nyie ni wale mnaoamini Nyerere hajafa na Raisi wa Africa kusini bado ni Nelson Mandela. Nyerere mwenyewe aliona mbali na kusema kweli kuwa upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM; kwani Nyerere alianzisha chama cha kupeleka watu peponi au kuunganisha watu na kuwaletea maendeleo? Wameshindwa kuongeza nchi wawaachie wengine. Funguka toka usingizini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom