Mungu si Athumani Kasie ameinuka tena.......

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
22,050
40,028
Hellos. ....
Maisha ukiyatizama kama mstari au kama umbo lolote hutayafurahia kwa asilimia zote.... ila ukiyatizama kama maisha ya amoeba ( yule mnyama sijui mdudu tumejifunza form two kwenye biology jinsi anavozaliana ni kwa kujimega au kujigawanya na hata miondoko yake iko iko tuu na hana umbo maalum yaani anabadilika badilika) ukiishi hivi japo si lazima na si marazote hakika utayafurahia maisha kwa asilimia zote hii ni pamoja na wakati wa shida na raha.
Nasema hivi kwa kuwa kama wiki hivi au mbili nilileta uzi wa kuwa kasie yuko katika hali ya huzuni ambapo wanadamu bin wazandiki walichukizwa na furaha yangu na maisha ninayoishi, mafanikio yangu hata kupanga kuniumiza, kuniangusha kuning'oa mahali nilipo na kuhakikisha nadondoka.
Kwa asilimia fulani walifanikiwa maana nilihuzunika kwa kupoteza vitu vyangu muhimu ila kwa sasa nawapa pole... nawaonea huruma na naweza kuwazomea haoooooooooo wajua kwa nini........
Mungu si Athumani wala Khadija nimeinuka tena.......nimefurahi tena nimerudi kwenye hisia zangu na maisha yanasonga mbele. Poleni sana sadists maana mlinizibia riziki kwa kufunga dirisha nililokuwa nikipokelea hela ila kwa Neema za allah yakafunguka madirisha 2 na mlango mkubwa ..... hadi rahaa ashukuriwe na azidi kunibariki aliye juu mweka na mtoa uhai.
Punde si punde utasikia Kasie mwanga yule au babu yake mchawi iweje mambo yamnyookee yeye tuu hahahahahaaa tumieni akili zenu na si nguvuuuu........
Huwezi amini nilipoteza vitu muhimu maishani niliyokuwa navyo kwa sababu ya chuki na maneno ya wanafiki na wazandiki. ......
Hivi niandikavyo niko Johannersburg nina wiki ya pili sasa na nitakaa huku kwa miezi kadhaa japo nitakuwa natoka na kwenda nchi nyingine nyingine kutokana na majukumu yangu mapya ya kazi.
Nimeyafurahia maisha ya huku johannersburg maana watu wake wengi asubuhi wanatembea kuelekea makazini wanaotumia magari binafsi wengi wanaotumia magari ambayo hayatumii mafuta mengi mfano wa engine capacity cc 2000 kushuka chini. Wanaopanda daladala ni wengi na utawaona wamebeba lunch box mkononi wadada kwa wakaka..... Maisha yako poa hapa.....
Meza niliyoipata inatema mawe ya maana na inanipa good time ambayo sijawahi kuiwaza. Nasafiri mara kwa mara kwa gharama za kampuni, nakutana na watu wa maana oooh what a life. Ukizingatia na status yangu ya single for life kiukweli nayafurahia maisha.
Napiga kazi kuliko ilivyo na muda wa ziada nakula maisha......
Kweli Mungu si Athumani wala Khadija.... assnte maulana.....
Nitakuwa mchoro wa fadhila nisipowashukuru walionisababishia nikaondolewa nilipokuwa maana wasinge fanya fitina nisingepata hii nafasi niliyonayo.
Asanteni sana sadists....mmuah
:):):)
Kasie.
 
Kasieeee daaah_.....!!!! Hongera Mkuu,.ila kuna baadhi ya maneno cjayaelewa vzr ktk huu Uzi wako ila nahic kutokana na furaha uliyonayo,.anyway

Enjoy Life.
 
Huko Joberg wamejaa wahuni tu hasa Hilbrow , njoo huku cape town ule good time!!!
 
Kasie, hongera bhana ila ulituacha njia panda na yule mjeda au na yeye ndo alikuwa kwenye plan ya masadist!!!!!!
 
Back
Top Bottom