"Mungu si Athumani" asili yake ni wapi?

IKARAHANSI

JF-Expert Member
Jul 30, 2019
398
479
Waheshimiwa habari za mihangaiko ya siku!

Ni matumaini yangu kuwa mko powa na wale wenye matatizo ya hapa na pale nawaombea kwa MUNGU awapitishe salama katika hali hiyo.

Nimekuwa nikisikia huu usemi kuwa "MUNGU SI ATHUMANI" tangu nilipoanza kujitambua, sasa ninaamini humu jamvini kuna wajuzi wa historia pia uzoefu wa maisha na ninaomba wanijulishe yafuatayo:-

a. Huyu Athumani alikuwa nani (Kimamlaka au kivyovyote) na alimkosea nini MUNGU?
b. Alitokea taifa gani hapa Duniani?
c. Kwa Nini iwe Athumani na siyo Daudi au Makame?

Ni matumaini yangu kuwa sasa nitapata majibu sahihi kupitia JF.
 
Huyu jamaa. Athuman alikuwa jirani yetu miaka hiyo ya 40s. Alikuwa na mambo mambo mengi sana. Alikuwa na tupesa kidogo.so ikawa akitaka msaidia mtu anaangalia nani ambaye huwa waniva naye...mwingine anampiga chini.kama una dada mkali basi hapo athumani atakusaidia sana ili aje amle dada yako.basi ndo ikawa watu wakipata jambo bila kusaidiwa na athuman ndo wanasema Mungu si athumani yaani hapendelei
 
Mkuu sidhani kama unamsemea Athumani kashingoo ..mzee mmoja aliyekuwa maarufu sana Arusha ..kwa wanaofahamu msikiti wa ngarenaro yeye ndo alitoa eneo na alishiriki kwa asilimia kubwa katika ujenzi...

Alikuwa mtu mwenye wake wasio na idadi na wote aliwatengenezea miji/boma kubwa..Watoto wasiohesabika mpaka Leo kwa sababu ya miji aliyokuwa nao..

Alikuwa mbaguzi kwenye kusaidia watu...aliangalia faida anayoipata baada ya kutoa msaada....hatoi msaada usio na faida kwake....

Baadaye sana wahenga wakifanikiwa wanasema MUNGU SI ATHUMANI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupitia hii methali nilipata wazo kwamba inawezekana hizi methali sio zote za wahenga wetu wa kiafrika, nyingine zitakua zilikuja na mashua na moja kama hii.
Ingekua yetu ingesema "Mungu si maganga" au "Mungu si Mbonde"
 
Waheshimiwa habari za mihangaiko ya siku!!

Ni matumaini yangu kuwa mko powa na wale wenye matatizo ya hapa na pale nawaombea kwa MUNGU awapitishe salama katika hali hiyo.

Nimekuwa nikisikia huu usemi kuwa "MUNGU SI ATHUMANI" tangu nilipoanza kujitambua, sasa ninaamini humu jamvini kuna wajuzi wa historia pia uzoefu wa maisha na ninaomba wanijulishe yafuatayo:-
a. Huyu Athumani alikuwa nani (Kimamlaka au kivyovyote) na alimkosea nini MUNGU?
b. Alitokea taifa gani hapa Duniani?
c. Kwa Nini iwe Athumani na siyo Daudi au Makame?

Ni matumaini yangu kuwa sasa nitapata majibu sahihi kupitia JF.
Athumani alikuwa tapelitapeli, mwongo mwongo, haamini, ahadi zake hazijawahi kutimia
 
Back
Top Bottom