Mungu na ulimwengu

Kiukweli ukiniambia kabla ya MUNGU kulikwepo na nini siwezi kukujibu na kitu kigumu sana ambacho kimewasumbua watu wengi sana hasa wanasayansi.

Yani origin ya MUNGU bado ni ishu nzito sana ambao sishani kama itakaa ipatikane.
MUNGU mwenyewe ni roho na roho ni kitu kisichoonekana wala kushikika sasa sijui tunafanyaje kwa kweli.
 
Kila mwanadamu kaumbwa kwa mfano wa Mungu,matendo na matukio ya kila mmoja Ni kipimo Cha uwezo wa fikra zetu Cha msingi IMANI ikitazamwa saana kwa vitendo Kuna mabadiliko ya fikra
 
Mimi naamini , kuna viumbe vyenye akili sawa , au zaidi ya sisi.
Pia naamini Mungu hatumiliki sisi tu , naamini kuna viumbe vingine mfano wa sisi vipo kwenye solar system nyingine kabisa.

Biblia inasema" akili za binadamu na za Mungu sawa na Mbingu na ardhi"


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo katikati ya galaxy usikute ndo kijiwe cha Mungu, ni akili za usiku tu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
A soul...! Once created can never be destroyed
To my opinion, a human's soul is never created but relocated as part of God's soul, having been there in His possession from eternity.

Huwa nafikiria hivi kwa sababu ile pumzi ya uhai anayoitoa Mungu na kumpulizia binadamu, ndiyo roho, na hiyo pumzi amekuwa nayo Mungu tangu milele.
Hata miili ya binadamu nayo pia huwa haumbi, huwa ana-modify kwa sababu kuumba tayari alishaumba huko nyuma, aliumba udongo, ambao ndiyo huwa anautumia kutengenezea mwili wa binadamu. Uumbaji Mungu alifanya huko nyuma kabla ya Adam na Hawa, na alichofanya katika kipindi wakati Adam na Hawa anawaleta duniani, siyo uumbaji, bali ukarabati ili kila kitu kiwe kama alivyotamani kiwe kwa ajili ya utukufu na mapenzi yake mwenyewe. Huu ni mtizamo wangu binafsi na hauna kiini kutoka kwenye maandiko yoyote matakatifu, bali ni kulingana na ufahamu wangu mimi mwenyewe tu basi
 
Binadamu ana mwanzo ila mwisho hana. Binadamu kufa siyo mwisho wa maisha yake, bali ni mwanzo wa maisha mengine mapya kwenye ulimwenngu mwingine. Na kama maisha ya binadamu hayana mwisho, kwa watu ambao akili yao ya maisha ni nzuri sana katika kupima maisha kwa kutumia probability (kumbuka kuwa probability ya uhalisia katika maisha ya kila siku haihitaji mtu kujua hesabu za probability ile tuliyofundishwa darasani, inahitaji mtu kuwa tu na common sensei), basi ni wazi kabisa kuwa probability ya kuishi maisha mazuri baadaye kutokana na kutenda mema sasa, ni kubwa zaidi kuliko ile ya kuishi maisha mazuri baadaye wakati hukiwa unatenda mabaya sasa. Probability ya kuishi maisha mazuri baadaye wakati ulikuwa unatenda mabaya ni ndogo mno kwa sababu hata katika misha haya ya sasa tuliyonayo hapa duniani, bado facts zinathibitisha hivyo, kwamba mabaya hayalipi isipokuwa mazuri.
 
Katika Mambo aliyotyficha MUngu moja wapo Ni mauti au kifo kwa kila mwanadamu,kwa maana laiti wanadam tungejua siku ya kufa kwetu yangekua yanatokea maafa zaidi kwa kila kifo Cha binadamu mmoja
 
A soul...! Once created can never be destroyed
A soul can be destroyed by the creater who created it.Remember before the existance of that soul there was no soul.So the one who brought it to existance can certainly destroy it.atlist that is what i know.Lakini ningependa kujua ni kwa nini roho haiwezi kuhilikiwa.Mshana jr
 
Mungu hayupo na dhana nzima ya "origin" inatokana na udogo wa mawazo yetu.

Kimsingi, time haipo, time ni kivuli kinachotegemea vitu vingine kama space na motion. Ukiondoa space na motion time nayo inaondoka, ukiweza kwenda at the speed of light, time inasimama, kwako wewe unaweza kutoka sehemu moja ya ulimwengu mpaka sehemu nyingine bila time kupita, hata oawe mbali vipi.

To photons, the univerae is timeless. Time does not move.

Ukisoma quantum physics, quantum entanglement na Einstein's Relativity utaona hayo.

Dhana nzima ya "ili hiki kifanyike, inabidi hiki kianze" -cause and effect, ina msingi katika time, kwa sababu bila time hakuna cha kwanza na kinachofuatia.

Na kama time si kitu cha msingi, cause and effect si kitu cha msingi.

Kwenye quantum physics kuna effects zinazotokea kabla ya causes na causes zinazotokea baada ya effects. Yaani katika quantum physics inawezekana wewe ukawa umemzaa baba yako mzazi.

Alice in Wonderland style.

Mambo mengi bado hayajaeleweka vizuri, ila ulimwengu huu tuliouzoea ni mdogo sana ukilinganisha na ukweli.

Hata habari za Mungu ni za maajabu ya kitoto ukilinganisha na ukweli halisi.

Hakuna Mungu, habari za chanzo zinategemea muda na muda si kitu cha msingi, hivyo habari za chanzo si za msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakupinga kwenye dhana ya Mungu hayupo. Mungu yupo. K Ila kwenye maswala ya time unaweza isimamisha kama ukitembea na speed ya light nakuunga mkono kabisa. Nilishai kusoma kitabu fulani. Icho kitabu kinasema kama ukiweza kutembea na speed ya light basi unaweza rudisha wakati nyuma ukaishi hata enz za yesu huko na mitume. Sayansi ni pana sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawezi kutoka nje ya sayari yake sababj haiwezekani na haitokuja kutokea.

Pili ni viumbe gani wenye akili kuliko binadamu ?

Ni kwa Sababu akili yako imeishia hapo .
 
nani alijaribu kusafiri hivyo au ni nadharia??
 
Thibitisha Mungu yupo.
 
Hesabu zinazokuwezesha wewe kuposti kwenye internet hapa JF ndizo zinazoelezea nadharia hizo.

Sasa kama unabishia hizo nadharia, bishia kwamba ume post hapa JF pia.
☕☕☕☕☕☕
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…