Mungu mkuu, Mfalme Suleiman na Ars Goetia (mapepo 72 ya kuzimu)

Mizimu ilitake advantage ya kuabudiwa na watu zamani kwa sababu hawakujua wanachokiabudu.
Mizimu ni wakuu wa falme za Giza wanaosimamia jamii,ukoo,kabila,taifa au familia fulani kwa kuishape ishi kulingana na matakwa ya mizimu
Usichokijua hata dini zimeshepiwa, Na katika dini zenye nguvu mizimu ni mojawapo.Ns ndio maana walokole na waislamu hukesha kuzipiga vita.Unapozungumzia mizimu usisahau mila
 
Utangulizi na Angalizo: Kuna mengi hatujayafahamu bado na kama tukiyafahamu bila maandalizi yanaweza kutuyumbisha kiimani kama tusipokuwa werevu lakini pia yanaweza kutupa maarifa mapya ambayo tulifichwa ama hatukupata kufundishwa!

---------------------------------

Kuna swali nimeulizwa mara nyingi hapa JF kama ni kila utajiri lazima uhusiane na nguvu za giza!!?
Jibu langu siku zote limekuwa hili Si kila utajiri ni lazima uambatane na nguvu za giza la hasha! Lakini kuulinda huo utajiri ama kuuongeza ni lazima kwa asilimia 100 nguvu za giza zihusike! Utajiri moja kwa moja huvutia nguvu za giza ni kama sumaku mbili zinazoshabihiana!

Mfalme Suleiman anayetajwa kama mtu tajiri zaidi kuwahi kutokea duniani (kuna Mansa Musa pia) Simulizi zinasema alipata kuongea na Mungu (nadhani kupitia tahajudi) ama vinginevyo! Na kwenye mazungumzo yao inaelekea Mungu alipendezwa na mwenendo wa maisha wa mfalme Suleiman hivyo akamuuliza angetaka nini toka kwake Mungu

Kwa mawazo ya wengi na kwa haraka watu wangetaja utajiri, mali na umaarufu, lakini kwa mshangao mkubwa Mfalme Suleiman hakutaja vyote hivyo bali alimuomba Mungu ampe hekima!

Unajua ni kwanini hakuomba mali/utajiri au umaarufu bali aliomba hekima?

Kwa nafasi yake ya ufalme hakupungukiwa na vyote hivyo, pengine changamoto kubwa ilikuwa ni kuhitaji hekima kwenye himaya kubwa aliyokuwa anaiongoza!

Mwenyezi Mungu akamkubalia ombi lake lakini pia kwa sababu za wazi kabisa akamuongezea na utajiri wa kufa mtu.. Na kumuacha afurahie maisha yake.. Kwahiyo akawa na ziada ya hekima na utajiri usiopimika! Na shughuli ikaanzia hapo!

Sijui ni kukengeuka ama ni unabii lakini Mfalme Suleiman pengine akaingiwa na hofu ya kupoteza utajiri wake aliotunukiwa bila jasho..! Kwenye kitabu cha The lasser key of Solomon (Ufunguo mdogo wa Suleiman) anatajwa kumiliki mapepo 72 ya kuzimu maarufu kama Ars Goetia. Haya mapepo 72 ya kuzimu yalikuwa na nguvu kubwa kiroho na kimwili na yalikuwa yamegawanyika katika sekta mbalimbali kuanzia ulinzi na usalama, elimu, umaarufu, vita, visasi, malipizi, mapenzi, uhai, libido nknk.. Ndani ya haya mapepo 72 kila moja lilikuwa na taasisi yake kamili yenye maroho ya kila aina..! Madude yote haya yalimilikiwa na Mfalme Suleiman kutokana na utajiri wake!

Mapepo haya 72 ya Ars Goetia pia yanatufumbua fumbo kubwa tulilokosa majibu yake kwa muda mrefu kuhusu Mfalme Suleiman kumiliki wanawake 1000, 700 wake wa ndoa na 300 wakiwa ni masuria (nyumba ndogo/michepuko) na wote hao akiwapelekea moto daily na bila kuchoka!

Huyu mzee ndio alituachia haya mapepo ya ngono yanayotutesa sasa hivi maana kwa nguvu za kawaida za binadamu asingeweza kunyandua daily tena sometimes mpaka mara 5 kwa siku kuzidi dozi ya ugonjwa ya kutwa mara 3


Lakini hapa pia tunafundishwa nini?
Pen ye Mungu shetani hakosi,yuko pembeni
Penye kila baraka kuna laana
Penye kila utajiri kuna nguvu za giza
Mungu hutoa yaliyo mema na kuondoka zake, shetani huyafanyia featuring na kuitawala roho iliyobatikiwa

Mungu akishakubariki keshamaliza, upungufu wa ukamilifu wa kibinadamu humchochea mtu kupitia mapepo yale ya Goetia ya kuzimu kutimiza hamu zake za kimwili na ndio hapo shetani huchukua umiliki

Jukumu la Mungu ni kutimiza wajibu wa kubariki na kugawa vipawa.. Baada ya hapo hatahangaika nawe tena! Kwakuwa anatambua fika utatuka urukavyo lakini mwisho wa siku utakata moto! Uliumbwa kwa mavumbi na mavumbini utarejea! Hutaishi milele

Mfalme Suleiman pamoja na kumiliki mapepo 72 yenye nguvu sana hayakuweza kumsaidia kumpa uhai wa milele!

Zaidi soma
Post in thread 'Kila baraka ina laana ndani yake' Kila baraka ina laana ndani yake


Nakala ya asili ya Goetia
Hii si,kweli.
Wapo waliobarikiwa na hakuna laana. Na wapo wenye utajiri mkubwa pasipo ku mix na mambo ya kishetani

Zingatia.

BARAKA ZA MUNGU HAZINA MAJUTO.
 
Kutambika ni Nini
Kukutanisha ukoo fulani ili kukamilisha mila, desturi, kuwakumbuka waliokufa zamani.Ili kujulisha kizazi kipya asili yao.Kukagua, kuombea na kupalilia makaburi.kuandaa chakula na pombe za kiasili kisha kucheza ngoma na burudani za jadi.
Na kukumbushana mambo mbali mbali ya kiukoo na mipangilio mbalimbali.
 
Samigina, pepo nambari 4 katika Ufunguo Mdogo wa Sulemani. Huwa nasikia watu wakiuliza "nimwite demu gani kufanya x?" X akimaanisha chochote wanachotafuta. Hilo linaweza kuwa chochote kutoka kwa upendo au pesa, au ustadi wa muziki, hadi ulinzi, kuondolewa kwa laana, n.k. Kwa hivyo ni vizuri kuorodhesha mashetani wote unaowajua katika grimoire yako binafsi na kile wanachoweza kufanya. Roho hii inafanya nini? Anafundisha sayansi huria na anatoa hesabu ya roho zilizokufa zilizokufa katika dhambi. Sayansi huria ni nini? Zinafafanuliwa kuwa lolote kati ya masomo saba ya kimapokeo ya kitaaluma: sarufi, mantiki, balagha, hesabu, muziki, jiometri, na unajimu. Hivyo basi, pepo ambaye anaweza kukufundisha jinsi ya kucheza muziki na kumvutia msichana unayempenda! Anaweza pia kuleta bibi yako aliyekufa ili uweze kuzungumza naye, hiyo ni sehemu ya necromancy "inatoa akaunti ya roho zilizokufa ambazo zilikufa katika dhambi."
FB_IMG_1688352031125.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samigina, pepo nambari 4 katika Ufunguo Mdogo wa Sulemani. Huwa nasikia watu wakiuliza "nimwite demu gani kufanya x?" X akimaanisha chochote wanachotafuta. Hilo linaweza kuwa chochote kutoka kwa upendo au pesa, au ustadi wa muziki, hadi ulinzi, kuondolewa kwa laana, n.k. Kwa hivyo ni vizuri kuorodhesha mashetani wote unaowajua katika grimoire yako binafsi na kile wanachoweza kufanya. Roho hii inafanya nini? Anafundisha sayansi huria na anatoa hesabu ya roho zilizokufa zilizokufa katika dhambi. Sayansi huria ni nini? Zinafafanuliwa kuwa lolote kati ya masomo saba ya kimapokeo ya kitaaluma: sarufi, mantiki, balagha, hesabu, muziki, jiometri, na unajimu. Hivyo basi, pepo ambaye anaweza kukufundisha jinsi ya kucheza muziki na kumvutia msichana unayempenda! Anaweza pia kuleta bibi yako aliyekufa ili uweze kuzungumza naye, hiyo ni sehemu ya necromancy "inatoa akaunti ya roho zilizokufa ambazo zilikufa katika dhambi."
View attachment 2676805

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimesoma mara nyingi niwezavyo lakini sijaelewa
 
Ndugu mshana,

Upo utajiri fake na utajiri Original.

Utajiri fake hutoka Kwa Shetani, hivyo tunguri, kafara lazima zihusike.

Utajiri original hutoka Kwa Mungu, na Mungu hakupi utajiri orijino asikupe maelekezo, utajiri orijino huendana na ZAKA na IBADA Kwa Mungu.

Wanaoyumba ni wale waliojaliwa Utajiri na Mungu bila kuomba, walifanya juhudi katika KAZI, na kutajirika, wapatapo mashambulizi ya kipepo Huwa wanaoyumba sababu hawajui chanzo Cha utajiri wao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom