Mungu hana sifa tatu, tu!

Mungu hana sifa tatu, tu!

Wakuu!
Nimeanzisha uzi huu kujaribu kutoa utetezi kinyume na hoja inayopinga uwepo wa Mungu kwa hoja kwamba ulimwengu huu unathibitisha kwamba 'Mungu mwenye upendo wote, uwezo wote na ujuzi wote' hayupo. Kwa wasiofahamu sana hoja hii ni maarufu pengine kuliko hoja zote zinazopinga uwepo wa Mungu, hivi kwamba imekuwa ikikimbiliwa na wengi wasioamini uwepo wa Mungu kama hoja yao ya msingi.

Kwa utambulisho mfupi mimi ninaamini kwamba Mungu yupo, na kwamba pia ninaamini Ukristo ndiyo dini ya kweli pekee. Haya nimeyatamka ili iwe rahisi kuelewa mtazamo wangu kuhusu hili swala, lakini nisingependa iwe msingi wa mjadala, natamani tujadili kulingana na kichwa cha uzi huu.

Ninataka kukiri kwamba ikiwa tunaoamini uwepo wa Mungu tutalazimishwa kuelezea mambo yote yanayotokea katika ulimwengu huu kwa kutumia sifa tatu tu za Mungu (Upendo, Uwezo na Ujuzi) tutababaika kujibu; tutaweza kutoa majibu kwa baadhi ya mambo, lakini si yote. Yamkini hili limejionesha mara kadhaa watu wanapoulizwa hilo swali.

Lakini hoja yangu ni kuwa tatizo liko kwenye swali lenyewe na si kwa wanaojibu. Ikiwa tutataka kujiburudisha tu kwa mdahalo, tunaweza kuweka swali la Mungu mwenye sifa tatu tu lielezee ulimwengu halisi tunaoishi. Lakini ikiwa tutataka kudadisi kwa undani uwepo wa Mungu aliyeuumba na anayeuongoza ulimwengu huu, lazima tutumie mjumuisho wa sifa zake zote (Mungu halisi) kuelezea mjumuisho wa mambo yote ya ulimwengu huu (ulimwengu halisi)

Mungu halisi ana sifa nyingi mbalimbali, na hizi zote zinahusika wakati wowote anapojihusisha na ulimwengu. Baadhi ni hizi Upendo, Uwezo, Ujuzi, Wema, Utakatifu, Utukufu, Hekima, Wivu, Haki, Mamlaka, Uamuzi Binafsi, Uwepo mahali pote, Maarifa na kadhalika.

Mfano: Tukitaka kujiuliza kwa nini Mungu ameumba jua na kuliweka umbali huo alioliweka, na kulazimisha kutumia sifa tatu tu za Mungu kuelezea, hatutapata jibu (la kuridhisha). Lakini tukiruhusu sifa zaidi, ile kujua kuwa ana 'Hekima na Maarifa' vitatupa jibu.

Jambo hili tunapaswa kulitumia tunapoelezea mambo mengine ya ulimwengu huu kama vile kwa nini kuna magonjwa, maafa na kadhalika ilhali Mungu ni mwenye upendo, uwezo na ujuzi wote. Ni kwa sababu hekima, haki, Uamuzi binafsi na kadhalika vinahusika pia.
Sijaziona hizo sifa ambazo unadai kuwa Mungu HANA!
 
Heshima kwako mkuu
Nafikiri naielewa kwa sehemu, kiasi cha kutosha kuelewa mtu anamaanisha nini akiwa anaitumia.

Unaelewa maana ya A n B n C hapo chini?

VDIntersections.png
 
Tatizo la wafia dini hawajui kwamba huyo Mungu anaepewa sifa zote izo alishindwa kuzuia biashara ya utumwa Africa
Watu waliuliwa/kulazimishwa kufuata hizi dini. Lakini bado mnaendelea kumtetea kwamba yupo
*smfh*
Mkuu
Utumwa unajumuishwa kwenye mambo mengine mengi kwa jina moja 'Ubaya'. Halafu wengi wanaopinga uwepo wa Mungu wanasema kwa sababu kuna 'ubaya', basi aidha Mungu
Unaelewa maana ya A n B n C hapo chini?

VDIntersections.png
Naam, nimeielewa hapo.
 
Tatizo la wafia dini hawajui kwamba huyo Mungu anaepewa sifa zote izo alishindwa kuzuia biashara ya utumwa Africa
Watu waliuliwa/kulazimishwa kufuata hizi dini. Lakini bado mnaendelea kumtetea kwamba yupo
*smfh*
Kwahiyo ulitaka waishi milele? Au ilijuaje kwamba vifo vyao havikuwa vya utumwa walitakiwa wafe vifo vingine.
 
Sijaziona hizo sifa ambazo unadai kuwa Mungu HANA!
Mkuu
Kuna sifa tatu za Mungu (Upendo, Uwezo na Ujuzi) ambazo zinatumiwa na baadhi ya watu kwamba zinajipinga/zinapingana na uhalisia wa ulimwengu huu. Ninachomaanisha ni kwamba Mungu ana sifa nyingi zaidi ya hizo, ambazo ni muhimu tunapojaribu kuelezea jambo lolote katika ulimwengu huu.
 
Mkuu
Utumwa unajumuishwa kwenye mambo mengine mengi kwa jina moja 'Ubaya'. Halafu wengi wanaopinga uwepo wa Mungu wanasema kwa sababu kuna 'ubaya', basi aidha Mungu

Naam, nimeielewa hapo.
Nikiwa na kopo la maji safi nusu lita, nikawa na kopo la mkojo wangu nusu lita, nikachanganya maji na mkojo, halafu nikachanganya na Pepsi nusu lita.

Nikawa na lita moja na nusu, mchanganyiko wa maji, mkojo wangu na Pespsi, vimechangamana vizuri.

Halafu nikakwambia kunywa, kwa sababu ndiyo mchanganyiko huo una mkojo wangu, lakini pia una maji safi na Pepsi

Utakunywa huo mchanganyiko wa maji, mkojo wangu na Pepsi?
 
Tatizo la wafia dini hawajui kwamba huyo Mungu anaepewa sifa zote izo alishindwa kuzuia biashara ya utumwa Africa
Watu waliuliwa/kulazimishwa kufuata hizi dini. Lakini bado mnaendelea kumtetea kwamba yupo
*smfh*
Mkuu
Maana ya ulichokiandika hapa ni sawa na kusema kwa sababu mtoto amepigwa na wenzie shuleni, basi itakuwa ni kwa sababu hana baba. Lakini inawezekana akawa na baba, ila hajaenda nae shule.

Ile kwamba inaonekana Mungu hajaingilia kati mambo fulani katika ulimwengu huu, haimaanishi moja kwa moja kwamba hayupo. Inatuhitaji kuzifahamu sifa za Mungu kwa undani, halafu tutaelewa kwa nini ulimwenu upo jinsi ulivyo.
 
Nikiwa na kopo la maji safi nusu lita, nikawa na kopo la mkojo wangu nusu lita, nikachanganya maji na mkojo, halafu nikachanganya na Pepsi nusu lita.

Nikawa na lita moja na nusu, mchanganyiko wa maji, mkojo wangu na Pespsi, vimechangamana vizuri.

Halafu nikakwambia kunywa, kwa sababu ndiyo mchanganyiko huo una mkojo wangu, lakini pia una maji safi na Pepsi

Utakunywa huo mchanganyiko wa maji, mkojo wangu na Pepsi?
Mkuu
Sifahamu unachokimaanisha, lakini uamuzi sahihi kwangu kwa mazingira kama hayo ni kutokunywa.
 
Mkuu
Nitaepuka kunywa kwa sababu mkojo ni kitu kibaya, huwezi kunywa. Na hasa ni kwa sababu 'mchanganyiko' haujaondoa ubaya wa mkojo.
Umejibu vizuri sana.

Kama ambavyomchanganyiko wa kuweka maji na Pepsi hauondoi ubaya wa mkojo, hivyo hivyo, unaposema "Mungu hana sifa tatu tu" sifa zake nyingine haziondoi sifa zake tatu.

Ni hivi.

Sifa yoyote utakayompa Mungu haiwezi kuondoa contradiction ya "the problem of evil" bila kuzaa contradiction nyingine.

Jaribu kufanya "thought experiemnt" hapa umpe Mungu sifa yoyote uone kama itaondoa "the problem of evil" bila kuleta contradiction nyingine.

Sababu hiyo hiyo iliyokufanya ukatae mchanganyiko wenye mkojo, ilitakiwa ikifanye umkatae Mungu mwenye uwezo wa kuzuia maovu ambaye anayaruhusu, kuruhusu maovu ni mkojo nao.

Sasa unachofanya kwa huyo Mungu unasema "Huyu Mungu si mkojo tu, kuna maji na Pepsi vimechanganywa, nakunywa, kwa sababu si mkojo tu"

Mbona pale juu umekataa kunywa maji yaliyochanganywa na mkojo na Pepsi, halafu kwa huyu Mungu unakubali kunywa maji yaliyochanganywa na mkojo na Pepsi?

Umeelewa unapojichanganya?
 
Kwahiyo ulitaka waishi milele? Au ilijuaje kwamba vifo vyao havikuwa vya utumwa walitakiwa wafe vifo vingine.

Hivi huyo Mungu wenu inamana alishindwa kumwinua nabii/mtume katikati ya waAfrika hadi tumjue kupitia watu wa mbali????
Inamana kwa kufanya ivyo hakujua kwamba kutatokea watu ambao hawataamini uwepo wake??
 
Umejibu vizuri sana.

Kama ambavyomchanganyiko wa kuweka maji na Pepsi hauondoi ubaya wa mkojo, hivyo hivyo, unaposema "Mungu hana sifa tatu tu" sifa zake nyingine haziondoi sifa zake tatu.

Ni hivi.

Sifa yoyote utakayompa Mungu haiwezi kuondoa contradiction ya "the problem of evil" bila kuzaa contradiction nyingine.

Jaribu kufanya "thought experiemnt" hapa umpe Mungu sifa yoyote uone kama itaondoa "the problem of evil" bila kuleta contradiction nyingine.

Sababu hiyo hiyo iliyokufanya ukatae mchanganyiko wenye mkojo, ilitakiwa ikifanye umkatae Mungu mwenye uwezo wa kuzuia maovu ambaye anayaruhusu, kuruhusu maovu ni mkojo nao.

Sasa unachofanya kwa huyo Mungu unasema "Huyu Mungu si mkojo tu, kuna maji na Pepsi vimechanganywa, nakunywa, kwa sababu si mkojo tu"

Mbona pale juu umekataa kunywa maji yaliyochanganywa na mkojo na Pepsi, halafu kwa huyu Mungu unakubali kunywa maji yaliyochanganywa na mkojo na Pepsi?

Umeelewa unapojichanganya?
Mkuu Kiranga
Nafikiri ninaona makosa matatu kwa maelezo yako hapo juu. Kwanza, unataka kutuaminisha kwamba kila mchanganyiko wa vitu hubakiza tabia za vitu vilivyochanganywa kama vilipokuwa havijachanganywa. Yaani, kwa sababu umetutolea mfano wa pepsi, maji na mkojo unalazimisha ziwe mfano halisi wa mchanganyo wa sifa za Mungu, ninaona hii si sahihi.

Pili, tunafundishwa na wanakemia kwamba maji (kimiminika) ni mchanganyiko wa Hydrogen na Oksigeni (hivi vyote ni gesi). Yaani, tunaweza kuwa na sifa moja ambayo ikisimama yenyewe huonekana hivi, lakini ikijumuishwa na zingine huonekana tofauti kabisa na ilivyokuwa mwanzo.

Tatu, unatuaminisha kwamba katika sifa za Mungu ipo angalau moja ambayo twaweza kuiita 'mbaya' na kwa hiyo inaharibu sifa zingine za Mungu. Lakini kwa Mungu ninayemzungumza, hakuna sifa yoyote ambayo ni mbaya.
 
Unaelewa sitaki chochote kuhusu imani, nataka ujuzi, na ukishaanza kuandika"unataka kutuaminisha" unaonekana hujanisoma wala kunielewa?

Mungu wako ni muovu au si muovy?

We unajua kuna liquid hydrogen na hydrogen si gesi tu? Kama hujajua kwamba kuna liquid hydrogen, una assume tu kwamba hydrogen ni gesi tu, kuna assumptions nyingine ngapi za mambo common knowledge tu unakosea?

Umeelewa kiini cha point yangu hapo?

Kwamba, kama Mungu muweza yote kuruhusu mabaya yaweze kuwepo duniani ni uovu, sifa nyingine yoyote utakayompa huyo Mungu haiondoi uovu huu bila kuleta conradiction?

Kuruhusu mabaya yaweze kuwepo wakati una uwezo wa kufanya yasiwepo ni kitu kizuri au kibaya?
 
Mimi si mtaalamu wa Kemia, lakini kwa kumbukumbu yangu muunganiko huo hutokea Oksijeni na Hydrogen zikiwa katika haki ya gesi na maji yanakuwa kimiminika. Japokuwa inawezekana kuvibadilisha kuwa gesi, kimiminika ama yabisi.

Mungu si muovu. Na hata ile kuruhusu uovu kuwepo ilhali anaweza kuuzuia SI uovu. Ni kama mwalimu aliyetunga mtihani, akaweka humo chaguzi zenye majibu ya uongo halafu akawaruhusu wanafunzi kuujibu mtihani. Nakuona wewe kama mwanafunzi uliyefeli mtihani na unalaumu mwalimu kwanini aliweka chaguzi za majibu ya uongo, na hapa unamuita mwalimu mwongo.
 
Umesema si mtaalamu, chukua somo la bure leo. Hata hydrogen inaweza kupatikana kama kimiminika, si gesi tu.

Mwalimu anaweka chaguzi kwa sababu hana uwezo wa kuingia kichwani kwako na kukupima unajua nini na hujui nini.

Mungu anayejua kila kitu na kuweza kila kitu anaweka uchaguzi ili iweje?

Kwa nini asingeweka mazuri matupu mabaya yasiwepo?

Angefanya hivyo angepungukiwa nini?
 
Hivi huyo Mungu wenu inamana alishindwa kumwinua nabii/mtume katikati ya waAfrika hadi tumjue kupitia watu wa mbali????
Inamana kwa kufanya ivyo hakujua kwamba kutatokea watu ambao hawataamini uwepo wake??
Mkuu
Jibu la hili swali ni rahisi, jiulize kwa jamii za watu ambao manabii/mitume walitumwa kutoka miongoni mwao Je, wote waliwaamini? Inaonekana kwamba watu hawaamini kwa sababu anayeongea wanamfahamu. Badala yake kuna msemo maarufu kwamba 'Nabii hakubaliki kwao'

Kuamini ni uamuzi wa kukubali jambo kutegemeana na ushahidi uliotolewa kulihusu jambo hilo, kwa mtu anayepuuzia ushahidi unaotolewa hatoamini haijalishi nani anayetoa ushahidi huo.
 
Back
Top Bottom