Mungu hana msaada wowote katika maisha yangu

Mungu hana msaada wowote katika maisha yangu

K
Tatizo kubwa linaanzia hapo unapo fikiria kwamba mungu nikiumbe👈
Ondoa fikra hii kichwani nahii imewafanya watu wengi kua tegemezi na ombaomba wakidhani mungu nikiumbe amestarehe sehemu anawasikiliza wao wakiomba?
Inabidi ubadili fikra zako na utambue kwamba mungu yuko ndani mwako wewe hapo.
Hivyo kumuomba nj'e nawewe nipigo la kufeli kwahatua yakwanza.
Kumbe ni kweli Mungu hasikii maombi?
 
Hivi unatesekaje, tuanzie hapo kwanza! acha kutafuta miujiza, fanya kazi acha uvivu
Ujinga wako unamlalamikia Mungu
Yesu mwana wa Mungu aliteseka tena kuuawa, Ayubu mtu mkamilifu na mnyenyekevu aliteseka,Samsoni alitobolewa macho na ni mtu wa karibu na Mungu
wewe una exceptional gani
Musa nabii aliteseka, akawekwa mtoni, akakimbia toka ikulu akaenda kuchunga
Je wewe uhusiano wako na Mungu upoje
Kiufupi watu wa karibu na Mungu kuna namna anawapitisha kwenye changamoto
Ibahim aliambiwa amtoe mtoto wake wa pekee kwa kumchinja sadaka
Yakobo alichumga miaka 14 ili kuwapata wake zake. wewe ushawahi kuchunga
Huwezi kuelewa. Asante
 
Mungu ni Mwenye Rehema! Kilio chako kimemfikia mbinguni! Usikate tamaa amekusikia atakupa yote unayohitaji.
 
Mikosi, Kila kitu kibaya Mimi. Dhambi zangu hazijai hata kikombe lakini niliyoyapitia ni magumu kuliko umri wangu.

Lakini ukitazama wengine kwenye matendo maovu yote huwakosi, Ila wamejaa neema tele. Kila kitu kizuri kwao.

Ninapoelekea naenda kutokumwamini huyu kiumbe wa kuitwa Mungu. Maana kama kweli yupo ni mtesaji na mnyanyasaji kweli.
NIMEMALIZA.
Supu ya Kitimoto
 
Mikosi, Kila kitu kibaya Mimi. Dhambi zangu hazijai hata kikombe lakini niliyoyapitia ni magumu kuliko umri wangu.

Lakini ukitazama wengine kwenye matendo maovu yote huwakosi, Ila wamejaa neema tele. Kila kitu kizuri kwao.

Ninapoelekea naenda kutokumwamini huyu kiumbe wa kuitwa Mungu. Maana kama kweli yupo ni mtesaji na mnyanyasaji kweli.
NIMEMALIZA.
Daah..pole sana ndugu..naona ni jinsi gani ulivyokata tamàa na maisha..Mungu hufanya njia pasipo na njia..muujiza wako unakuja
 
Ha
Mwanangu wewe hata usimuamini tu, yeye atabaki kuaminiwa na wengine wengiii tu.

Kama umeona Mungu hata msaada fanya hivi

Nenda kaombe kwa kutumia jina la shetani,

Mwambie bwana shetani nisaidie mambo yangu kwakua Mungu nae muamini hana msaada wowote kwangu
Hakuna kitu sijajaribu kukiabudu hapa duniani,: Mizimu, Shetani, Mungu, Miungu, Majini, Jua, Mwezi nk.
Ili tu nipate kile ninachokitaka lakini wapi. Mpaka nikahisi labda kuna formula nakosea wakati wa maombi.

HUENDA MIUJIZA HAIPO
 
Mkuu shida ni wewe mwenyewe fikra zako juu ya mazingira yanayokuzunguka ndio zinachukua asilimia kubwa ya hali unayopitia.

Sasa kama unataka mabadiliko kwanza kabisa, Kamwe usimlaumu/usifikilie kua watu au Mungu ndio wamesababishia hali hiyo.

Amini kwamba hali iwayo yoyote ile unayopitia wewe ndio chanzo na hakuna mtu yeyote ataibadilisha kama wewe mwenyewe hautataka kubadilika.

Kwanini ni kwasababu wewe binafsi umepewa uwezo wa kuamua/ wakuchagua na ukiamua na kuchukua jitihada kwa Akili yako, mali zako na nguvu zako zote... Hilo jambo uliloamua litafanikiwa tu(kwa lugha nyingine ni unakua na IMANI) na yeyote aombaye kwa imani basi aamini amekwisha pokea)

Yaani binadamu yeyote yule (wewe) Ni sehemu ya Mungu/una Uungu ndani yako na nguvu unazo. Kiufupi wewe ni Mungu na kwa ujumla wetu watu wote tunaunda mtandao wa MUNGU. Sasa kama sisi ni miungu kwanini wengi wetu hatuna maajabu(nguvu) Ni KWASABABU hatujiamini(hatuna IMANI) hatujajiunganisha na mtandao wa MUNGU. Sasa kwanini umlaumu au ufikilie mbona kina fulani wako hivi mimi siko ilhali uwezo huo na wewe unao.

Sasa mimi nakushauri badilisha kabisa fikra zako uwe unajiwazia mambo mema ya baraka, mafanikio, huku ukiongeza Akili nguvu na mali zako zote(Uwekezaji) katika malengo ulio jiwekea katika utaftaji wako na ili nafsi yako ione uko serious*** nakushauri badili kabisa mazingira nenda sehemu ambako hujulikani na hauna msaada wowote kwako then ishi vizuri na watu.
Kwa mantiki hiyo Mungu haongozi maisha ya ulimwengu?
 
Ukishaanza kusema anaweza akawepo maana yake umekubali anaweza asiwepo. Hapo umeweka conjecture.

Unathibitishaje Mungu yupo?
jibu lakusema yupo ama hayupo linatakiwa liwe limethibitishwa kwa kufanya chunguzi ulimwengu mzima sasa wewe mpk unasema hayupo umeshafanya hivyo...??

NB; sifungamani pande yoyote sijui kama yupo au hayupo!.
 
Mungu hayupo mkuu. Jipange mwenyewe kuishi na wengine tu.

Tusaidiane wenyewe, kwa sababu Mungu hayupo, hivyo hawezi kutusaidia.

Ukielewa hili, utajibu maswali mengi sana.
Naweza kukubaliana na wewe nimemuomba Mungu sana lakini wapi. Na huenda wanaonishutumu hawajafikia kiwango hicho cha maombi yangu.
 
jibu lakusema yupo ama hayupo linatakiwa liwe limethibitishwa kwa kufanya chunguzi ulimwengu mzima sasa wewe mpk unasema hayupo umeshafanya hivyo...??

NB; sifungamani pande yoyote sijui kama yupo au hayupo!.
Basi una mashaka ya uwepo wake kama Mimi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom