Mungu haijui kesho yako

Mungu haijui kesho yako

Mpondoshilla

Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
36
Reaction score
132
Ni ukweli ulio wazi ila ni ngumu kukubalika hasa kwa watu waliokaririshwa imani.

Iko hivi Mungu angekuwa anaijua kesho yako kusingekuwepo na kitu kinachoitwa dhambi, kwa sababu, mfano mtu amechinjwa hapo hakuna dhambi maana tayari mungu alishapanga utachinjwa au huo uovu unaoufanya sasa ungekuwa sio dhambi maana mungu alishapanga.

Njia unayoipitia ndiyo hatima ya maisha yako.

Kuna watu wanamtumikia Mungu mpaka wanazeeka na pia wapo wanamtumikia shetani mpaka wanazeeka.

Pia wapo walikuwa wanamtumikia Mungu ila hawajauona hata ujana.

Maisha ni kama simu tu utachagua uitumieje vile unaitumia ndiyo inakupa majibu unayoyataka wewe.
 
Lengo ni hitimisho la maisha yako ya umilele, Mungu hana hasara hata ukipotea,maana ana viumbe wengine mamilioni kwenye sayari zingine wasio na dhambi, anakupa muongozo kwa faida yako Ili uishi vyema hapa duniani na kesho ahera.
 
Nionavyo binadamu uwa tunatenda na kupita mule mule kulikokwisha pangwa na kujulikana kwa muumba wetu milele na milele huko nyuma.

Haijalishi hayo tunayotenda ni mema au mabaya na tunayopitia ni mepesi au magumu maana yalishapangwa na kubwa zaidi kujulikana na Mungu mwenyewe na hivyo binadamu kutenda au kupitia njia tofauti na hiyo ni ngumu. Tukikataa hili basi tuwe tayari kusema Mungu hana uwezo wa kujua kila kitu.

Na hili la Mungu kutojua kila kitu sitaliamini milele.
 
Sasa kwanini aruhusu mi nizaliwe si angepotezea tu nisiwepo?
 
Nionavyo binadamu uwa tunatenda na kupita mule mule kulikokwisha pangwa na kujulikana kwa muumba wetu milele na milele huko nyuma.

Haijalishi hayo tunayotenda ni mema au mabaya na tunayopitia ni mepesi au magumu maana yalishapangwa na kubwa zaidi kujulikana na Mungu mwenyewe na hivyo binadamu kutenda au kupitia njia tofauti na hiyo ni ngumu. Tukikataa hili basi tuwe tayari kusema Mungu hana uwezo wa kujua kila kitu.

Na hili la Mungu kutojua kila kitu sitaliamini milele.
Sasa kwanini huwa tunamuomba ili abadili maamuzi?
 
Anasema Allaah (Ta'aalaa):

وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ
Na Kwake (Allaah) zipo funguo za ghayb; hakuna azijuaye ila Yeye tu [Al-An’aam 6:59]

Na Anasema (Jalla Jalaaluhu):
قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ ۚ
Sema: “Hakuna aliyoko katika mbingu na ardhi ajuaye ghayb isipokuwa Allaah. [An-Naml 27: 65]
 
ulimuona akisema?
 
Nionavyo binadamu uwa tunatenda na kupita mule mule kulikokwisha pangwa na kujulikana kwa muumba wetu milele na milele huko nyuma.

Haijalishi hayo tunayotenda ni mema au mabaya na tunayopitia ni mepesi au magumu maana yalishapangwa na kubwa zaidi kujulikana na Mungu mwenyewe na hivyo binadamu kutenda au kupitia njia tofauti na hiyo ni ngumu. Tukikataa hili basi tuwe tayari kusema Mungu hana uwezo wa kujua kila kitu.

Na hili la Mungu kutojua kila kitu sitaliamini milele.
Unachosema ni kwamba binadamu hana uchaguzi, hayupo huru zaidi ya kufuata kilichopangwa jambo ambalo si kweli.

Mm nachoona hatufanyi mambo kwa sababu MUNGU amepanga ila MUNGU anajua tutakalofanya kutokana na tabia zetu za maamuzi na tamaa anayoiona ndani yetu.

Kama tu wewe unavyomtambua mwanao wa kiume kiasi kwamba unajua pamoja na kumuonya sana ila nikisafiri nikamuacha atavuta bangi. Wewe kujua kuwa atavuta bangi haimaanishi kuwa ulipanga avute bangi.
 
Ni ukweli ulio wazi ila ni ngumu kukubalika hasa kwa watu waliokaririshwa imani,

Iko hivi Mungu angekuwa anaijua kesho yako kusingekuwepo na kitu kinachoitwa dhambi, kwa sababu, mfano mtu amechinjwa hapo hakuna dhambi maana tayari mungu alishapanga utachinjwa au huo uovu unaoufanya sasa ungekuwa sio dhambi maana mungu alishapanga.

Njia unayoipitia ndiyo hatima ya maisha yako.

Kuna watu wanamtumikia Mungu mpaka wanazeeka na pia wapo wanamtumikia shetani mpaka wanazeeka.

Pia wapo walikuwa wanamtumikia Mungu ila hawajauona hata ujana

Maisha ni kama simu tu utachagua uitumieje vile unaitumia ndiyo inakupa majibu unayoyataka wewe
hoja dhaifu sana. Kesho ya Kila mtu huwa imepangwa na Mungu mwenyew tena Mungu humwazia mema kila mtu ila dhambi ndio hublock baraka bora za kesho ya mtu na kwakua ibilisi yuko against na mema Mungu anayowatakia watu wake. hutumia mlango wa dhambi kama kichocheo cha kublock baraka hizo kwakushawishi wanadamu kujiingiza huko. hakuna baya au zuri linalo mpata mtu kwa mpango wa mungu lile lisilo bora kwa huyo mtu. elewa sio kila jambo baya linalomtokea mtu Mungu anataka limpate
 
"Hakika Allaah Ana elimu ya Saa (Qiyaamah), na Anateremsha mvua na Anajua yale yaliyomo katika tumbo la uzazi, na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani, hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika." 31:34
 
Hapa wachague moja kati ya haya mawili

1.) Mungu kama anaijua kesho yetu maana yake ameshapanga kesho yetu, hivyo dhambi zote mtuhumiwa namba 1 ni yeye.

2.) Kama dhambi ni zetu, maana yake yeye hakupanga sisi tufanye dhambi bali ni uamuzi wetu sisi wenyewe, hivyo haijui kesho yetu.

Chagueni moja hapo
 
Kumbe kila kitu kimeshapangwa..🤣🤣
Basi haina haja ya kuhangaikia sijui kwenda church maana matokeo ni yale yale mwisho wa siku
Yani hata usipoenda jua ndivyo ilivyopangwaaa 😀 😀 usidhani kwamba ukienda sijui kuna mpango utaubadilisha hapana ndo maana unaweza toka kanisani na still ukagongwa na gari ukafa... haubadilishi kitu ila hivyo ndivyo ilivyoandikwa juu ya maisha yako zaidi ukienda Kanisani unatengeneza maisha yako baada ya kifo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom