Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 10,021
- 20,256
AMINI AHADI ZA MUNGU ZITATOKEA KWAKO
HESABU 23:19, Mungu si mtu, aseme uongo, wala si mwanadamu, ajute, iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza? (Ref: 1Samwel 15:29, Malaki 3:6, Tito 1:2)
1FALME 8:56, Na ahimidiwe Bwana, aliyewapa watu wake Israel kustarehe, vile vile kama yote aliyoyaahidi. Halikukosa kupatikana neno lolote katika ahadi yake njema aliyoahidi kwa mkono wa Musa, mtumishi wake. (Ref; Kumb 12:10, Yoshua 21:45, Yoshua 23:14).
YEREMIA 1:12, Ndipo Bwana akaniambia, umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize. (hii maana yake nini?, anatafuta wapi alisema kitu ili akitimize vilevile kama alivyosema, anaangalia alichokisema ili akitimize, analinda kile alichokisema hadi kitimizwe, yupo nyuma ya chochote alichokisema hadi kitimie).
Labda kama Mungu hakutamka, ila maadamu alikisema, lazima kitatimia chote.
Hebu jiulize, una sababu gani ya kutoamini kile Mungu alichokisema? Ni kwamba unaona Mungu hawezi kufanya au vipi? Hauoni kuwa unaposhindwa kuamini kuwa Mungu atafanya jambo alilolisema unakuwa unamdharau kwamba hana uwezo? Hizo ni dharau, kwanini usiamini kuwa anaweza kufanya? Kwanini unamtilia mashaka?
Basi, kama kuna kitu cha kukitilia mashaka maishani mwako, sio Mungu, unapaswa kutilia mashaka hayo mashaka yako wewe mwenyewe kwasababu huna uhakika kama mashaka yako yana mashiko yeyote, huna uhakika kama Mungu hatafanya hivyo yatilie mashaka mashaka yako mwenyewe. Usiyaamini mashaka yako, lakini usije kuwa na Mashaka na Mungu, yeye sio mtu hata aseme uongo, wala sio mwanadamu hadi ajutie kile alichokisema kwamba kwanini alikisema labda kwasababu hakitatokea.
Jifunze leo, wanadamu huwa wanaahidi vitu vingi ila baadaye wanaanza kujuta kwanini waliahidi kwasababu wanajikuta hawawezi kutimiza, kwa Mungu ni tofauti, yeye sio mwanadamu hadi ajutie kile alichokisema labda kwasababu ameona hataweza kukifanya, HAKUNA alichowahi kukitamka akashindwa kukitimiza. Pia yeye huliangalia Neno lake ili lisikae bure bila kulitimiza. ukiamini kile alichokitamka kuhusiana na hali uliyo nayo, kitatokea hata bila kuwekewa mikono, kwasababu namna pekee ya uhusiano wetu na Mungu ni kwa njia ya IMANI. pasipo imani hakuna aliyewahi kumpendeza Mungu, pasipo imani manake unamtilia mashaka Mungu unaona hana nguvu au kama hataweza au kama aliahidi uongo, na hiyo ni dharau kwake. Mwamini Mungu, soma Neno lake na uliamini.
ISAYA 55: 11 INASEMA, ndivyo litakavyokua Neno langu litokalo katika kinywa changu, halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yote niliyolituma.