Mungu ana mpango gani na watanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mungu ana mpango gani na watanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HOMOSAPIEN, Jun 15, 2012.

 1. HOMOSAPIEN

  HOMOSAPIEN JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 719
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Nauliza hivi huu uonevu tunaofanyiwa watanzania utaisha lini?.Hali ngumu ya maisha,bidhaa juu,bado na kodi tena imepanda!bidhaa muhimu zinaonekana ni anasa,mshahara ndiyo hivyo kwa wastani kima cha chini ni kidogo sana.

  Hivi mungu haoni huu uonevu,mbona anawasaidia wengi hata waisraeli kule misri aliwatoa utumwani na kuwapeleka katika nchi ya ahadi.Je sisi watanzania hatuko katika mpango wa mungu?mbona wengine wanafanya maombi yanakubaliwa?vipi viongozi wetu wa dini wanashindwa kuomba maombi ya kweli kujinasua na haya matatizo?badala yake wanatishiwa eti waheshimu sheria au wale walioko madarakani!.siasa za hovyo hovyo kila anayepata nafasi anakula tu tena bila kupangusa mdomo.

  Imefikia wakati sasa wanaweka wanawe marafiki katika nyazifa kubwa kama vile mungu haoni,kama kweli mungu anaona basi tunaomba atende miujiza yake hata leo niko tayari kufunga nac kuomba isifike 2015.

  Nakumbuka rais wa iliyokuwa inaitwa Romania au Yugoslavia jina Chesescu aliuwawa na wananchi wake baada ya wananchi kuchoka na manyanyaso na maisha magumu wakati viongozi wao wanaishi maisha ya kutumbua wakiwadanganya wananchi wao hii ikasababisha mpaka nchi yenyewe ikasambaratika.

  Angalia hapo Misri wananchi wanaandamana wanataka Mubarak ahukumiwe kifo badala ya maisha.

  Viongozi wetu hawajifunzi haya wakafanya marekebisho kidogo au ni mpaka yatokee?.

  Tunaomba yasitokee kwetu tuendelee kuwa wamoja ila yanayojiri sasa yanaweza kutufikisha huko tulikozungumzia hapo juu.
  Karibu watanzania wataamka katika lidi la usingizi wa kusema hewalahewala kila jambo hata liwe baya.
   
 2. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mungu always yupo na wanadamu wake hata wakiwa wabaya vipi. Hata jambazi yupo na Mungu
  Cha muhimu hapa ni sisi wenyewe kujikwamua ktk hili lindi la fikra potofu kuwa ukombozi unaambatana na umwagaji damu kwahiyo tusishabikie.

  na sisiem wanajenga watu hivyo na kuwaaminisha kuwa upinzani = vita = damu!
  Kuna idadi kubwa bado ya watz wanaamini hivyo.

  Thanks to M4C kwa kazi ya kuwaelimisha watz hadi ngazi ya kata ili waondokane na fikra hizi potofu:crazy:. matunda yamekwishaanza onekana.
   
 3. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Sasa zingatia pamoja nami kile kinachosemwa katika Mithali 11:11, "Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki, bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu." Waovu wameongea vibaya kuhusu taifa letu, na nitawaambia Wakristo wengi sana wamefanya hivyo hivyo. Wamesema, "Ah! – hatuna watu bali kundi la wapumbavu tu pale, hawajui wanalolifanya."

  Walipaswa kuwa wanasema, "Namshukuru Mungu, Naamini kwamba Mungu atawapa viongozi wetu pale Dodoma hekima ya kimungu ili waweze kutatua matatizo ya taifa letu."

  Kama Wakristo wangefanya hivyo, wangebadili hali pale Dodoma.
  Baadhi ya Wakristo wameanza kufanya hivyo. Kweli hii imeanza kutokea kwa kiasi fulani. Na Mungu ameanza kutatua baadhi ya matatizo katika serikali ya taifa letu. Mungu ameshaletwa kwenye madhari kwa sababu ya maneno yaliyojaa imani.

  Anza kusema, "Namshukuru Mungu kwa kuwa viongozi wa taifa letu wana hekima ya Mungu." Waombee kila siku. "Baba wape hekima yako ili wafanye mambo ya kitaifa hasa yanayohusu maisha kwa hekima."

  "Maneno ya mwovu huotea damu, bali kinywa cha wanyofu kitawaokoa." (Mitahali 12:6)
  Nini kitawaokoa?

  Kinywa cha wanyofu. Wakovu upo karibu kama mdomo wako. Kinywa kina ulimi ambao hutawala imani na hofu.Maneno huzaa mambo yafanananayo nayo. Tunapaswa kufahamu hili. Tunapoanza kuongea kile alichokisema Mungu Ibilisi atanyamaza na kufungasha virago.Sasa zingatia pamoja nami kile kinachosemwa katika Mithali 11:11, "Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki, bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu."

  Waovu wameongea vibaya kuhusu taifa letu, na nitawaambia Wakristo wengi sana wamefanya hivyo hivyo. Wamesema, "Ah! – hatuna watu bali kundi la wapumbavu tu pale, hawajui wanalolifanya."

  Walipaswa kuwa wanasema, "Namshukuru Mungu, Naamini kwamba Mungu atawapa viongozi wetu pale Dodoma hekima ya kimungu ili waweze kutatua matatizo ya taifa letu."

  Kama Wakristo wangefanya hivyo, wangebadili hali pale Dodoma.
  Baadhi ya Wakristo wameanza kufanya hivyo. Kweli hii imeanza kutokea kwa kiasi fulani. Na Mungu ameanza kutatua baadhi ya matatizo katika serikali ya taifa letu. Mungu ameshaletwa kwenye madhari kwa sababu ya maneno yaliyojaa imani.

  Anza kusema, "Namshukuru Mungu kwa kuwa viongozi wa taifa letu wana hekima ya Mungu." Waombee kila siku. "Baba wape hekima yako ili wafanye mambo ya kitaifa hasa yanayohusu maisha kwa hekima."
  "Maneno ya mwovu huotea damu, bali kinywa cha wanyofu kitawaokoa." (Mitahali 12:6)

  Nini kitawaokoa? Kinywa cha wanyofu. Wakovu upo karibu kama mdomo wako. Kinywa kina ulimi ambao hutawala imani na hofu.
  Maneno huzaa mambo yafanananayo nayo. Tunapaswa kufahamu hili. Tunapoanza kuongea kile alichokisema Mungu Ibilisi atanyamaza na kufungasha virago.
   
 4. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2012
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa! Lazima tuombe hawa viongozi hata kama hatuwapendi!

   
 5. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #5
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  hakuna cha kumsingizia Mungu hapo, ukondoo wetu ndo umaskini wetu, tumezidi kuwa makondoo watanzania, ngoja wenye meno watukamue.
   
 6. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  mungu yupo na haya anayaona..."NI NANI ATAKAYE SIMAMA KUPAJENGA MAHALA PALIPOBOMOKA??" inavyoonekana hakuna walio chukua hatua thabiti kupambana na haya masuala kiroho
   
 7. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mungu anatusubiri mimi na wewe, tumwambie tunataka nini.

  And all things, whatsoever ye shall ask in prayer, believing, ye shall receive. Matthew 21:22

  1 Kings 3:
  11 Then God said to him: "Because you have asked this thing, and have not asked long life for yourself, nor have asked riches for yourself, nor have asked the life of your enemies, but have asked for yourself understanding to discern justice,

  "Keep on asking, and you will receive what you ask for. Keep on seeking, and you will find. Keep on knocking, and the door will be opened to you. Matthew 7:7

  God created man to have dominion over the earth acording to his will.

  Kwa huu ufisadi wa sasa, yaani ni kumuomba Mungu tu.
  Uchawi ndio uliotufikisha hapa.
   
 8. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Mungu katupa akili ili tuitawale dunia. Wanaosababisha haya ni wanadamu na sisi wanadamu kupitia kumuona yeye tunabadilisha haya.
  Kumbuka bila kubisha hodi huwezi funguliwa mlango.
   
 9. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tugonge hodi hadi tufunguliwe, hakuna kulala nje.
   
 10. Mkwai

  Mkwai JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 308
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwetu kuna msemo wa kiluga "omba mungu huku ukikimbia" kwa maana nyepesi ni kwamba unapomuomba mungu lazima uchanganye na vitendo, au uonyeshe jitihada kwa vitendo kwa kile unachokiomba. so maombi peke yake bila kuonyesha jitihada zozote za kuikataa hali tusioitaka tusitegemee miujiza kuibadilisha.
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Eh Wajameni, Kwanini Iwe Mungu? Tulikuwa na J.K.Nyerere; Haturaruana, Hatukuchinjana, Pamoja na kuwa na Makabila kibao, na Dini kibao...

  Wao hao Mubarak - Alikuwa na Ubabe tu watu walijuwa wanauawa kama senene, hawana Makabila, Dini 3

  [h=1]Nicolae Ceausescu yeye alikuwa pia ni utawala wa kuwanyanyasa wananchi wake na kuwanyima uhuru unapotea Jela haurudi tena wengi hadi watoto[/h]
  * Sisi tulikuwa na bahati, lakini ndio kuna baadhi waliona hakuwa rais mzuri. lakini hakumwaga Damu hata kidogo; hata Wapinzani aliwaruhusu kuondoka kuliko kufia jela na kuendeleza upinzani wao nje ya nchi... hiyo ni bora

  TATIZO NI KUWA MWANADAMU HARIDHIKI; HATA UKIMPA CHAI YA MAZIWA KILA ASUBUHI ATAITAFUTIA DOSARI YAKE.
   
 12. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Mungu hana mpango na tanzania wala watanzania anampango na tanganyika na watanganyika
   
Loading...