Ni jambo linalotia matumaini kwamba hali duni inayolikabili taifa la Tanzania hatimaye imewagusa hata watu wa mataifa ya nje; si Ulaya Magharibi au Marekani pekee bali hata katika nchi za kiafrika na baadhi ya majirani zetu; hata kama baadhi yao hawsemi chochote hadharani kwa sababu zinazojulikana.
Kwa yale mataifa ambayo tayari wametoa misimamo yao kuhusu hali ya kisiasa hapa nchini kwetu, wengi wameonyesha kusikitishwa na hali ya ukandamizaji unaofanywa na watawala ambao wameshika madaraka bila ridhaa ya wananchi na hadi kutumia silaha kuua wananchi wao.
Juhudi za hadaa zinazotumika ili kuwasafisha hawa watawala, kazi hiyo inazidi kuwa ngumu kwao.
Juhudi hizo ni pamoja na kuwaajili kampuni maalum za kuwatetea katika baadhi ya nchi wafadhili. kama Marekani na Ulaya.
Kwa mfano, kampuni ya kimarekani (lobbyst) iliyopewa kazi ya kushawishi wawakilishi wa maseneta wa Marekani, kampuni ambayo walikubaliana malipo ya dola 45,000 kila mwezi kwa miezi sita.
Kutokana na taarifa za hivi karibuni toka huko Marekani, ni wazi kuwa kazi ya 'lobbyists' hao haikuzaa matunda bora yaliyotegemewa kama inavyoelezwa na mswada unaotengenezwa na maseneta wawili ili uwasilishwe kwenye seneti ya nchi hiyo..
Katika baadhi ya maprendekezo ya mswada huo ni kuwataja viongozi wote wanaojulikana kuhusika na mauaji/utekaji na mambo ya ukandamizaji kwa waTanzania; na hatimaye kuweka vikwazo vya kiuchumi.
Pamoja na kuwa na shukrani kwa nia hiyo nzuri ya kuwabana viongozi waovu; njia hiyo si suluhisho lenye msaada wa haraka kwa waTanzania wanaotafuta kujinasua toka kwenye hii hali mbovu haraka iwezekanavyo.
Vikwazo vya kiuchumi huchukua muda, na mara nyingi wanaoumizwa ni wananchi wenyewe; huku watawala waovu hao wakiendelea na uovu wao.
Msaada unaohitajika kwa waTanzania ni kuwawezesha wafanye wenyewe kazi hii muhimu ya kujiondoa kwenye manyanyaso ya hawa watawala.
Kwa kuwa uwepo wao madarakani unategemea ukandamizaji na mitutu ya bunduki kuua wote wanaojaribu kukataa kunyanyaswa, msaada mzuri zaidi na wa thamani kubwa ni kuhakikisjha kuwa hawaruhusiwi kuitumia mitutu ya bunduki tena bila ya wao kudhurika.
WaTanzania wakipewa msaada huo, kazi ya kurekebisha nchi yetu itakuwa rahisi kwetu wenyewe na njia za kuwawajibisha hawa waovu zitapatikana kwa haki, bila ya uonevu kwa yeyote.
Kwa hiyo, ombi kuu la waTanzania kwa mataifa yanayotaka kusaidia juhudi zetu, ni kuwanyima fursa ya kutumia bunduki wakati waTanzania wakitafuta njia za kurekebisha uongozi wa taifa lao.