Mungu ana makudi yake kwa kila jambo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mungu ana makudi yake kwa kila jambo

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by The Listener, May 22, 2012.

 1. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuburudika kwa binadamu ni sehemu ya kila siku ya maisha. Kama zilivyo sehemu nyingine za burudani/mapumziko fukwe za bahari hupendwa na watu wengi. Ilitokea weekend moja ambapo pamoja na watu mbalimbali waliofika kufurahia ufukweni mwa bahari. Ndugu mmoja alikwenda na nduguye ambaye ni mlemavu wa macho/kipofu.

  Mmoja kati ya ya watu wengine wengi waliohudhururia alikuwa Pastor na alijisikia unyonge sana baada ya kuwaona watu wakiburudika majini huku yule kipofu akiwa nje ya maji na akajiuliza eeh Mungu mtu huyu amekukosea nini hata asipate furaha wanayoipata hawa wengine. Akasikia sauti ya chinichini ikimjibu, 'Kila kitu kitokeacho duniani kina sababu yake'. Sauti ile ikaendelea kunena, 'Haujuia hata chembe sababu za mtu huyu kuwa hivi'.

  Mara ghafla yule mtu akapewa uwezo wa kuona na akafurahia sana naye pastor akafurahi sana kwa maombi yake kusikilizwa. Baada ya muda si mrefu yule mponywaji wa upofu akaingia kwenye maji na kuanza kuwakaba watu waliokuwa wakiogelea. Pastor alikasirishwa sana na hali ile kiasi cha kufikia kutaka kumtandika makofi. Akayarejea maneno aliyoyasikia 'kila kitu kitokeacho duniani kina sababu yake'
   
 2. Prof Gamba

  Prof Gamba JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 390
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  enhe!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. Rjohn

  Rjohn JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 599
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Nikwel kabisa
   
Loading...