MZALENDOWAKWELIKWELI
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 330
- 210
Kwa yeyote mwenye fikra pevu kwa sehemu atakuwa ameng'amua jibu sahihi la dereva lori mzuri ni yupi.....
Dereva asiyejua ni wapi anapeleka watu wake ni dereva ambaye badala ya kusonga mbele atafunga breki kisha aachie usukani ageuke nyuma aanze kusikiliza wasiokuwa tayari kuona gari inafika iendako.....dereva wa namna hii ni dereva ambaye hakujiandaa, hajui wapi anakwenda na wapi anataka kufika.
Dereva anayejua wapi anakwenda hawezi kukubali kupoteza muda kuanza kusimama na kuachia usukani tena katika mazingira ambayo njia ya kufika tuendako ina miiba, milima na mabonde....ningeshangaa kama nisingeskia makelele ya abiria walalamikaji.....
Kwakweli ikifika mahali ikathibitika pasipo shaka kuwa dereva hajasikiliza kelele za kumkwamisha kufika anakoamini ni salama, dereva huyo ni SHUJAA..... Kwanini? Salama anayopeleka abiria wake ni salama anayoijua vizuri kuliko mtu mwingine.....ni salama ambayo akiifika hakubahatisha..... Ushauri wangu ni kumpa nafasi, kumtia moyo dereva huyu wa zamu......
Ni nani anayependa kuzongwa hata robo ya kule atakakokwenda, tena alishapaelezea vizuri tukapaelewa na kumpa usukani wenyewe....leo tumshike mashati apoteze mwelekeo.....nani atakubali.....
Mazuri ya kufanya yanaweza kuwa yako mengi....ni kweli lakini nani asiyekubali huwezi kuyafanya yote???? Mtaka yote hukosa yote.... Tujenge siasa mpya zitakazoigwa na wengine duniani.....Siasa za kupimana kwa matokeo....Siasa za kupeana nafasi.....Siasa za kusaidiana kuziba mashimo gari ipite na sio kuchimba mashimo.....hizi hata wewe unayesoma usingezikubali.....
Kama kweli tunaitalia mema nchi yetu.....twendeni tuunge mkono wanaojenga hoja AGENDA KWA AGENDA.....
Tulianza agenda ya vyeti feki hakuna hata mmoja aliyemnyooshea kidole kiongozi yeyote kwamba ana vyeti feki....Agenda ikapita.....
Tulipoanza agenda ya madawati hakuna hata mmoja aliyepost popote pale wanafunzi wanakaa chini ili madawati yapelekwe.....uone tulivyo wanafiki......
Tulipokuja agenda ya madawa ya kulevya....duuu wanaibuka watu kuchangia....tunapoanza kuwasikiliza kwa makini hoja zinakuwa si za agenda iliyoko mezani bali agenda tofauti.....agenda ambayo tulishajadili na hawakuchangia chochote.....
Usipokuwa smart ni rahisi kutoka nje ya mstari coz mtoa hoja huitoa kwa ustadi mkubwa na usahihi wa uliomakinika.....LAKINI LAKINI kwa wakati usio sahihi hata kidogo..... kwa style ya kukufanya upige breki urudi nyuma kwa ishu ambayo muda wake ulishapita......au si muda wake sahihi ama kukukwamisha agenda iliyoko mezani isihitimishwe vyema.....swali ni je mtu huyu tumbumilie?
Dereva anayeweza kung'amua hili na kukiruka kihunzi hiki si mwingine ni dereva MAKINI TU.....
DEREVA WA AINA HII NI WA KUMLINDA NA KUMUOMBEA....NI DEREVA AMBAYE HATA UKILALA USINGIZI NAKUHAKIKISHIA LAZIMA UFIKE SALAMA KWA UWEZA WA MUNGU....
TUBADILIKE. TUBADILIKE. TUBADILIKE.