Mungu alimuandaa Rais Samia kuwa Rais ndiyo maana amewahi kusema hadharani kuwa yeye hana mpango wa kwenda kugombea Urais wa Zanzibar 2020

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,607
10,020
Ndugu zangu Watanzania,

Nimekaa nikatafakari juu ya Mama yetu huyu mpendwa nikaona kuwa pamoja na kuwa Rais Samia alisema kuwa yeye katika mawazo yake hajawahi kuwaza kugombea Urais wala kuwa Rais wa nchi hii zaidi ya kutamani kufanya kazi katika ndege ,lakini nimekuja kutambua na kugundua kuwa katika ulimwengu wa kiroho Mungu alimuandaa kabisa Mama yetu kipenzi kuwa Rais wa Taifa letu. Ndio maana watanzania waliposema kuwa Rais Samia anakwenda kugombea Urais wa Zanzibar, alikanusha hadharani na kusema kuwa yeye ni namba mbili na hawezi kwenda kutafuta unamba tatu.

Unajuwa ndugu zangu ni kuwa kuna wakati Mungu anaweza kuwa ana mipango na wewe kukupatia nafasi fulani ya uongozi au majukumu fulani pasipo wewe kujuwa wala kujijua. Na katika kufanya hivyo na kukuandaa huko Mungu anakawaida ya kukupitisha katika mikono ya watu watakao fanikisha mipango ya Mungu juu yako pengine na wao wenyewe pasipo kujuwa.lakini pia Mungu anayo namna ya kuwaficha watu wake aliowaandaa na kuwa na mipango nao ili wasichafuke au kudhurika .lakini pia huwapa ngozi ngumu ya uvumilivu,subira wapitiapo magumu au kushambuliwa.huwapatia mioyo ya utulivu,hekima na busara.

Angalia kuinuliwa kwa Mfalme Daudi,angalia alikotolewa porini alikokuwa akichunga kondoo na hatimaye kupakwa mafuta.angalia Mungu alivyomlinda dhidi ya hila za Sauli aliyetaka kumuuwa.angalia namna Daudi alivyokuwa mtulivu katika vita yake ya kukimbia dhidi ya Sauli katika kuepuka kuuwawa, na namna ambavyo Mungu alikuwa akimsemesha na kumuongoza pamoja na kumuelekeza mahali pa kwenda kujificha au kuishi au kukaa au kupita ili kuukwepa mkono wa Sauli.

Ni dhahiri Rais Samia Ni mpango wa Mungu Mwenyewe kumuinua katika kuliongoza Taifa letu.ndio maana mnaona anaongoza nchi pasipo papala wala hofu wala uoga wala kuteteleka wala kuyumbishwa wala kuonyesha udhaifu.ndio maana mnaona yupo imara katika vishindo vya aina yoyote ile.ndio maana mnaona kinywa chake ni kinywa cha kiuongozi kinachojuwa wakati gani kizungumze na wakati gani afumbe kinywa chake. Ni mama anayeongoza nchi utafikiri alikuwa amejiandaa nusu karne nzima kuutaka Urais.

Funzo hapa ni kuwa unaweza ukautafuta Urais kwa jasho na Damu na bado ukaukosa.unaweza ukatembea kwa waganga wa kienyeji,ukatoa watu kafara,ukaua watu unaoona ni kikwazo kwako na bado ukaukosa Urais. Unaweza ukamwaga pesa kwa watu mbalimbali unaoona wana ushawishi na wanaweza kukuvusha lakini ukajikuta huupati Urais. unaweza wachafua wengine,kuwapaka matope ,kuwagombanisha na watu,kuwaliza na kuwabubujisha watu machozi wasio na hatia,kuuwa watu unaoona ni vikwazo,kutesa watu lakini bado ukaukosa Urais.

Kikubwa ni kujinyenyekeza kwa Mungu na kumuomba akupatie jibu juu ya ndoto zako.siyo kila mtu anaweza kuwa Rais.unaweza ukajiona una stahili kuwa Rais lakini Mungu akakuona wewe unastahili kuishia kuwa waziri tu au mbunge au balozi tu nje ya nchi yetu. Mungu ni Mungu tu.hii ndio maana Mungu husema yeye anautizama moyo wa Mtu na siyo muonekano wake wa nje. Mwanadamu unaweza ukafanya maovu mengi sana gizani kwa lengo la kuutafuta Urais halafu Mungu akakukwamisha kwa kuwa yeye anaona yale yote unayoyafanya ukiwa gizani huko ambayo wengine sisi hatuyaoni lakini yapo hadharani machoni pa Mungu.

Mnao utafuta Urais kwa jasho na Damu nawashaurini tu kuwa acheni kufanya hivyo,jikiteni kuchapa kazi na kumsaidia Rais wetu kuwatumikia watanzania,kusiwepo hujuma za aina yoyote ile wala hila za aina yoyote ile. maana unaweza muhujumu Mama yetu kipenzi halafu ukajikuta kuwa anakuja inuliwa mtu mwingine kabisa ambaye wala hakutarajiwa wala kuwahi kuwazwa kuwa anaweza kuwa Rais wetu. Hii ndio maana ya Kauli ya kuwa uongozi unatoka kwa Mungu Mwenyewe na kwamba amelaaniwa mtu yule amtegemeaye Mwanadamu. Kama umepangwa kuwa wewe ndiye basi hakuna awezaye kukukwamisha ,lakini kama wewe siyo uliyeandaliwa na Mungu basi utahangaika na kutumia kila njia lakini utaishia kuusikia tu Urais.

Rais Samia Ni Mpango wa Mungu na chaguo la Mungu Mwenyewe kuliongoza Taifa letu ,ameinuliwa kwa mkono wake na siyo mkono wa mwanadamu wala mapenzi ya mwandamu bali ni kwa Mapenzi na kusudi lake Mungu Mwenyewe.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.

Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili kama Rais wetu na Amiri Jeshi Mkuu wetu.

IMG-20240315-WA0027.jpg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimekaa nikatafakari juu ya Mama yetu huyu mpendwa nikaona kuwa pamoja na kuwa Rais Samia alisema kuwa yeye katika mawazo yake hajawahi kuwaza kugombea Urais wala kuwa Rais wa nchi hii zaidi ya kutamani kufanya kazi katika


Naomba umwambie Mungu wako hatutaki wizi wa kura na tuna omba tume huru. Lakini mwambie tunaomba katiba mpya na awaite wote watakao kataa hayo matakwa ya wananchi
 
Naomba umwambie Mungu wako hatutaki wizi wa kura na tuna omba tume huru. Lakini mwambie tunaomba katiba mpya na awaite wote watakao kataa hayo matakwa ya wananchi
Mungu amemuinua Rais Samia kutuongoza na kuwapatia Watanzania haja za mioyo yao.usijali maana Rais wetu ni Mama Msikivu na mwenye upendo wa dhati na uzalendo kwa Taifa letu.
 
Mungu amemuinua Rais Samia kutuongoza na kuwaotia Watanzania haja za mioyo yao.usijali maana Rais wetu ni Mama Msikivu na mwenye upendo wa dhati na uzalendo kwa Taifa letu.


Inabidi tumuombe Mungu maana sheria zinazopita na majina mazuri kama " Tume huru" wakati sio huru. Rushwa imezidi sana. Mungu amuombe Mama atupe haki au amwite kama mtangulia wake mpendwa wetu aliyemtangulia tupate viongozi ambao kweli wana nia ya kubadilisha nchi
 
Inabidi tumuombe Mungu maana sheria zinazopita na majina mazuri kama " Tume huru" wakati sio huru. Rushwa imezidi sana. Mungu amuombe Mama atupe haki au amwite kama mtangulia wake mpendwa wetu aliyemtangulia tupate viongozi ambao kweli wana nia ya kubadilisha nchi
Rais Samia analindwa na mkono wa Mungu.wenye chuki binafsi aina yako mtaendelea kuona aibu kubwa sana kwa namna anavyoendelea kuwainua watanzania kiuchumi na Taifa kwa ujumla. Kwa sasa Tanzania chini ya Rais Samia ni miongoni mwa nchi kumi za Afrika zenye uchumi mkubwa.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimekaa nikatafakari juu ya Mama yetu huyu mpendwa nikaona kuwa pamoja na kuwa Rais Samia alisema kuwa yeye katika mawazo yake hajawahi kuwaza kugombea Urais wala kuwa Rais wa nchi hii zaidi ya kutamani kufanya kazi katika
Wewe kama sio Mwehu ni KICHAA
 
Back
Top Bottom