SOCIOLOGISTTZ
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 2,615
- 929
Chadema inazidi kupasua anga kila mahali
molemo umetia chumvi nyingi. wiliam mungai aisambaratishe ccm sasa wakati chaguzi za vitongoji na mitaa chadema wamesambaratishwa...mbona unatugeuza watoto wa pinokyo? ungetuambia kuwa wenyeviti wa ccm wamejiuzulu na kurudisha kadi tungekuamini lakini hili la kuchoma kadi mbona hata mimi naweza kuchukua kadi moja ya chadema nikaidurufu zikawa mia au mia mbili halafu nikasimama nazo jukwaani kuwaonyesha kisha nikazichoma..ungetutupia na picha za hao mamia ya wana ccm wanaohama tungekuamini, vinginevyo hatudanganyiki
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimekiweka pagumu chama cha Mapinduzi katika jimbo la Mufindi Kaskazini.
William Mungai mtoto wa waziri wa muda mrefu wa Elimu Tanzania Joseph Mungai ndiye anayeongoza 'mazishi' ya chama cha baba yake hapa Mufindi.
William Mungai tangu ajiunge na CHADEMA zaidi ya mwaka mmoja uliopita amekuwa akiongoza operesheni kadhaa kuimarisha CHADEMA na kuchoma moto hadharani kadi za maelfu ya wanaCCM wanaokihama chama hicho.
Mungai amekuwa akiwaeleza wananchi wa Mufindi mateso makubwa wanayopata na huduma mbovu ni kutokana na sera mbovu za CCM na kuwaambia ukombozi pekee uko CHADEMA kutokana na sera nzuri za chama hicho na uongozi thabiti usiyoyumba wa Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa.
William Mungai ambaye kwa sasa ni mjumbe wa mkutano Mkuu Chadema Taifa wiki iliyopita alimualika jimboni humo Makamu Mwenyekiti BAVICHA Taifa Patrick Ole Sosopi kufanya mikutano kadhaa jimboni humo kuimarisha CHADEMA.
Joseph Mungai ambaye ni Baba yake William mbali ya kutumikia serikali kama Waziri kwa muda mrefu pia amekuwa mbunge wa Mufindi Kaskazini kwa miaka 35.
Akihojiwa kwa nini mtoto wake amejiunga CHADEMA huku yeye akiwa ni kada mkongwe wa CCM waziri huyo wa zamani amesema kamwe hawezi kumuingilia mtoto wake kwani ni kijana mkubwa mwenye maamuzi yake na amesema anamtakia kila la kheri katika harakati zake.
Ukipima hivyo siku zote tafriri yenye uhasilia zaidi si km unayofikiria..tafsiri sahihi zaidi itakuwa ni kwamba CDM NI CHAMA CHA KISASA NDIO MAANA KINAVUTIA WATU WA SASA HIVI NA BAADAE.Pia ujue CCM inapoteza kila mahali ..hata issue ya umeme waliyokuwa wakichukua sifa km mvua eti wanapeleka umeme vijijini wakati wao ndio kikwazo.Yaani wanaiba hela na hii inaonyesha kuwa si wazo lao kupeleka umeme na ushahidi upo ,kwanini mataifa makubwa yanaona kuwa dunia nzima inahitaji kupata umeme ama wa solar ,maji etc ila ili baade waunganishwe na mawasiliano ili kujenga mitandao ya kuwafikia watu wote wa dunia.CCM ni wapumbavu sana kuelewa chocote hata kile wanachokipigia upatu au kutafutia sifa.Kwa kijana kujiunga na cdm sio jambo la kushangaza kamwe! Chadema ni chama kinachoendana na vijana, kwa hiyo ni jambo la kawaida.
Hapo kwenye red angalia usije sababisha wazee wanaotaka kujiunga na waliomo kwenye chama wakaamua kuacha/kuondoka kwa kuhofia kuwa hiki ni chama cha vijana.Kwa kijana kujiunga na cdm sio jambo la kushangaza kamwe! Chadema ni chama kinachoendana na vijana, kwa hiyo ni jambo la kawaida.
Swali:Compare and conrast Big Willy with 'folly Willy' (Le Mutuz).
Hali ya Mufindi iko 50% kila upande...boat hii itazama endapo Mahamoud Mgimwa atarejeshwa kama mgombea baaada kushindanishwa na wana CCM wenzake hii 2015....iwe jimbo jipya tarajiwa la Mafinga au Kusini...
Mgimwa anasemekana kufanya kosa moja...hakuvunja kambi na hasa sasa anaonekana hana tofauti na Mtangulizi wake tena Mtangulizi wake ni bora mara mia.
Kuna issue ya kukopesha bodaboda vijana kwa riba kubwa nako kumemvunjia kuaminika..though ilikuwa ni nia njema lakini sasa inatumika kumuumiza..ujio wa vibali vya uvunaji mbao Saohill nao unamgharimu sanaaa huyu kaka yetu. Hapa kwenye vibali kumeleta siasa mnoo
Huyu ni Mbunge ambaye analaumiwa hana makazi yake mwenyewe jimboni licha ya kuhudumu kwa miaka mitano lakini kushiriki sana siasa za UVCCM mkoani Iringa, Mahamoud ni wa Iringa mjini zaidi ya Mufindi. Mufindi ni kwa mamake zaidi, Iringa ni ngumu kumtoutisha wa Kilolo,Mufindi na hata Kalenga, ila ndio siasa zenyewe
Ana malezi ya wazee wa nchi , hasa ukaribu wake na Makamu wa Rais ndio silaha yake tangu UVCCM....na sasa, na ndicho kilichomuinua 2010, hoja ya kiufundi ni wepesi wake yeye kujiwekea himaya pasipo kumuegemea Mkulu yeyote 2015....akiicheza vema yuko salama. Kuna tetesi kuwa anampiga zengwe mwenziwe Kigora ili angolewe na Mama mmoja wa CCM Mufindi, hili halitamuacha salama Mgimwa...nashauri ajiondoe ktk move hiyo tena hadharani.
Kwa sasa ana wapinzani wakuu watatu hivi wenye koo zenye mashiko wilayani Mufindi...Mwanadiplomasia Chumi , ambaye kwa sasa wapambe wa Mgimwa wanamtangaza kuwa yuko nje ya nchi kikazi...Dr. Kalinga Tacaids na Bwana mmoja aliyepambana 2005-10 yuko pale Viwanda...watatu hawa wakijitosa Mgimwa atakuwa hayupo Bungeni tena.....ndio. maana namshauri atumie hekima za Muvina Vangimembe Lukuvi. Kuna invisible prospect for both kwa Mgimwa na kidogo kule kwa Lukuvi...huyu Invisible toka Ludilo akitia mguu hatapona Mgimwa wala Chadema yeyote Mufindi Kusini. He is the strongest prospect....huyu itategemea nani ni Rais ajaye finito.
Ni kweli CCM imeshinda mitaa na vijiji...lakini leadership ina mchanganyiko wa vyama na ushindi wenyewe ni %00.2, hili ukiongea na makada wenyewe pale mjini wanakiri ushindi wa margin ndogo mnoo na kuiimarisha itataka mgombea safi kwa nafasi ya Ubunge.
William Mungai....anahitaji siasa za kweli na msukumo wa kweli toka kwa Chadema Hq...kunahitajika a dedicated move ya kumtofautisha William Mungai na Joseph Mungai...kwa mjini Mafinga hilo linajionyesha kuwa habebwi na kivuli cha babake ila kwa vijijini inahitajika msasa wa kweli kumrutubisha.
Mgimwa anaweza aka survive endapo hawa watatu watamuunga Mkono kwa kutompinga kwa sababu kwa sasa Mh. Mgimwa ni Muvina...bado ana ujana kwa mbali lakini pia Lukuvi is nearing who else will acquire the Uvina? Wakimpinga Mvina huyu halafu akaibuka kidedea kura za maoni basi CCM haitarudi salama kwenye general election Mufindi ikiwa Mh.Mgimwa ndie mgombea wao. Suluhu wamalizane nje ya kura ya maoni waje kama timu
CCM has alot to do when it comes Mufindi lakini pia CHADEMA has a big task ahead to lure all ant Mgimwa na those Jose's loyal guardians. Agenda ya CCM iwe ni chama kumlinda Mgimwa....ila wakishindana Itakuwa mwanani?! Ndi Mgayisida......hatutaoka salama.
CCM Hoyeeeeee
Mkuu nimesoma uchambuzi wako unaonekana unaijua vizuri siasa ya Mufindi na vitongoji vyake, mm binafsi nipo karibu na huyu bwana wa viwanda na biashara (Mr Kigahe). Huyu bwana anajitahidi sana kuwa karibu na wapiga kura hasa wale wa kawaida.
Kuna huyu bwna Chumi wa wizara ya mambo ya nje ana ushawishi lakini tatizo anatumia hela zaidi na anajivunia support kutoka TISS.
Dk Kalinga wa Tacaids huyo simfahamu kabisa. But whois this invisible? Na kwanini awe tishio, ana nguvu gani na kwanini awe invisible?
Kwa upande wa Mahmood uwezekano wa kurudi bungeni kupitia Mufindi ni mdogo sana!
Mkuu huu siyo usultani au kwa kuwa mtoto kaswitch chama basi usultani unaisha? Huku ni kuchezea shere tu lakini inabaki kuwa ukoo wa Mungai ndio unaitawala Ufindi!
Mungai siyo jina la Kenya hilo? Huyo kafikaje TanzaniaChama cha Demokrasia na Maendeleo kimekiweka pagumu chama cha Mapinduzi katika jimbo la Mufindi Kaskazini.
William Mungai mtoto wa waziri wa muda mrefu wa Elimu Tanzania Joseph Mungai ndiye anayeongoza 'mazishi' ya chama cha baba yake hapa Mufindi.
William Mungai tangu ajiunge na CHADEMA zaidi ya mwaka mmoja uliopita amekuwa akiongoza operesheni kadhaa kuimarisha CHADEMA na kuchoma moto hadharani kadi za maelfu ya wanaCCM wanaokihama chama hicho.
Mungai amekuwa akiwaeleza wananchi wa Mufindi mateso makubwa wanayopata na huduma mbovu ni kutokana na sera mbovu za CCM na kuwaambia ukombozi pekee uko CHADEMA kutokana na sera nzuri za chama hicho na uongozi thabiti usiyoyumba wa Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa.
William Mungai ambaye kwa sasa ni mjumbe wa mkutano Mkuu Chadema Taifa wiki iliyopita alimualika jimboni humo Makamu Mwenyekiti BAVICHA Taifa Patrick Ole Sosopi kufanya mikutano kadhaa jimboni humo kuimarisha CHADEMA.
Joseph Mungai ambaye ni Baba yake William mbali ya kutumikia serikali kama Waziri kwa muda mrefu pia amekuwa mbunge wa Mufindi Kaskazini kwa miaka 35.
Akihojiwa kwa nini mtoto wake amejiunga CHADEMA huku yeye akiwa ni kada mkongwe wa CCM waziri huyo wa zamani amesema kamwe hawezi kumuingilia mtoto wake kwani ni kijana mkubwa mwenye maamuzi yake na amesema anamtakia kila la kheri katika harakati zake.
A
Mungai siyo jina la Kenya hilo? Huyo kafikaje Tanzania
Acha ukabila wewe, kama jina ni la Kenya basi mhusika ni Mtanzania, kama vipi nenda kamwambie akupe jina upeleke huko Kenya ila yy atabaki Mufindi.
Safi sana Mungai Senior, Huwezi kumuamulia kila kitu mtoto wako mwenye mji wake, ana akili yake, ana utashi wake na ana kampenzi yake na hiyo ndiyo demokrasia ya kifamilia. wamesahau tu hao kijana ana mapenzi gani na chama kilichomnyanyasa na kumdharirisha baba yake dakika za mwisho kana kwamba hawamjui. Mtu aliyekitumikia chama kwa uadilifu zaidi ya miaka 30 huwezi kumtreat sawa na kijana aliyejiunga juzi kwa kuangalia maslahi. CCM ya Nyerere na akina Mungai, Siyovelwa, Butiku, Kisumo, Kawawa,Msuya, Mwakawago,Adam sapi,Sokoine, na wengine wengi wa aina hiyo aslani haikuwa na maslahi kwa sababu ulikuwa imefungamanishwa pamoja na Azimio la Arusha. Ndiyo maana wazee wetu wale wengi wao walikufa katika hali ya kawaida. Kumpeleka mahakamani kwa kosa ambalo hata mahakama haikuliona ni udharirishaji.Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimekiweka pagumu chama cha Mapinduzi katika jimbo la Mufindi Kaskazini.
William Mungai mtoto wa waziri wa muda mrefu wa Elimu Tanzania Joseph Mungai ndiye anayeongoza 'mazishi' ya chama cha baba yake hapa Mufindi.
William Mungai tangu ajiunge na CHADEMA zaidi ya mwaka mmoja uliopita amekuwa akiongoza operesheni kadhaa kuimarisha CHADEMA na kuchoma moto hadharani kadi za maelfu ya wanaCCM wanaokihama chama hicho.
Mungai amekuwa akiwaeleza wananchi wa Mufindi mateso makubwa wanayopata na huduma mbovu ni kutokana na sera mbovu za CCM na kuwaambia ukombozi pekee uko CHADEMA kutokana na sera nzuri za chama hicho na uongozi thabiti usiyoyumba wa Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa.
William Mungai ambaye kwa sasa ni mjumbe wa mkutano Mkuu Chadema Taifa wiki iliyopita alimualika jimboni humo Makamu Mwenyekiti BAVICHA Taifa Patrick Ole Sosopi kufanya mikutano kadhaa jimboni humo kuimarisha CHADEMA.
Joseph Mungai ambaye ni Baba yake William mbali ya kutumikia serikali kama Waziri kwa muda mrefu pia amekuwa mbunge wa Mufindi Kaskazini kwa miaka 35.
Akihojiwa kwa nini mtoto wake amejiunga CHADEMA huku yeye akiwa ni kada mkongwe wa CCM waziri huyo wa zamani amesema kamwe hawezi kumuingilia mtoto wake kwani ni kijana mkubwa mwenye maamuzi yake na amesema anamtakia kila la kheri katika harakati zake.
Na unaweza kukuta kwenda CHADEMA kashauriwa na baba yake!Kwa kweli ukiona mpaka watoto wa wanaCCM wakongwe kama Mungai wanaondoka katika chama hicho fahamu kinakaribia kukata roho!