Mungai amlipua Lowassa kwa propaganda anazofanya

Mungai amlipua Lowassa kwa propaganda anazofanya

Status
Not open for further replies.
Anachosema Mungai ni upotoshwaji wa watu kumsifia lowassa kuwa ujenzi wa shule za kata ndiye aliyeziansha na kuzijenga pia kuwa UDO ni wazo la kikwete. Hajisifu kama alifanya vizuri kama waziri kwenye elimu, ila alihuska kufungua baadhi ya shule za kata wakati huo lowasa ni waziri wa maji na kikwete waziri wa mambo ya nje. sasa kumshabulia kuwa aliharibu michezo shuleni, nadhani havina uhusiano na mada yenyewe, labda nia yake iwe kuwaondoa wachangia kwenye mada ya msingi, ili kuendelea kuficha upotoshaji na uongo huo kwa kusetili mtu fulani
 
Wazo na msukumo ulitoka kwa nani kama si yeye.Mungai akili yake hakuwa nayo wakati akiwa waziri wa elimu labda kama aliyemuazima kamrudishia.

Aliondoa elimu ya michezo shuleni akavuruga masomo ya sayansi labda kwa makusudi kwa vile anaaminika ni Mkenya.Ndipo alipokabidhiwa dhamana Mama Sita akasema pale bungeni aliyefuta michezo mashuleni hana akili.Sasa leo anakuja na hekaya za abunuwasi akafie mbali kama Nepi alivyosema..... wanasubiri kufa.

Ma CCM yanazodoana
 
Alichosema Mungai pamoja na mapungufu yake ni kweli, kama tuna kumbukumbu nzuri Kikwete alivyoingia alisema shule zipo tayari sasa ni mda wa kutafuta walimu, ndo vijana wa form six walifundishwa kwa wiki sita wakaenda kufundisha( aka Voda fasta)...

Sawa kabisa mkuu! hata mimi nilitaka kujibu hivyo
.Yaani watanzania sisi ni wepesi wa kusahsahau sana.Kikwete alipoingia madarakani 2005 ailikuta shule ziko tayari Lowasa akiwa PM ndo hivyo wakatangaza crash program, hili halina ubishi, kama kuna mtu anabisha basi hana kumbukumbu.
 
Sawa kabisa mkuu! hata mimi nilitaka kujibu hivyo
.Yaani watanzania sisi ni wepesi wa kusahsahau sana.Kikwete alipoingia madarakani 2005 ailikuta shule ziko tayari Lowasa akiwa PM ndo hivyo wakatangaza crash program, hili halina ubishi, kama kuna mtu anabisha basi hana kumbukumbu.

watu wanaubongo wa funza ndo maana wanajifanya wamesahau, ile crush program ilichukua vijana wengi kituo kimoja wapo pale mwanza ilikwa Butimba, vijana wengi waliokuwa hawana uhakika wa kuendelea na chuo, issue ilikuwa unaenda kufundisha kwa miaka mitatu au miwili then unaenda kuchukua degree ukiwa na uhakika wa mkopo....matokeo bila shaka kila mtu anayajua.
 
Hivi Shetani anaweza kufukuza Jini?

Akifanya hivyo ufalme wake utafitinika. Ukiona watu wa chama kimoja wanafitiniana, basi ujue ufalme wao umefitinika. Baada ya hayo Mungai akubali alivyoua elimu kwa kuunganisha combination na kuondoa michezo shuleni jambo ambalo athari zake mbaya bado hazijaondoka.
 
mungai alituharibia elimu,lakini hivi sasa ameamua kuwa mkweli na kumpa lowasa za uso
 
team ya lowasa imechanganyikiwa,na hii ni dozi ndogo tu,subiri ukawa waingie ikulu mtakufa njaa
 
Haaaa,,,,naanza kwa kucheka tena sana hivi huyu mungai kwanza hana jipya kama mnakumbuka ndugu watu walivyofutiwa mitihani yao,,,daah alafu leo waja kutueleza nini hivi hujui watu wana machungu?kwanza umevuruga mitaala na kuleta ya ajabu ajabu yani wewe bora ukae kimya tuu kwa hili umechemka
 
Mungai kwanza mkimbizi huyo asituletee upuuz ktk nchi yetu,kwanza naasira nae sana alinivurugia kipaji changu alipofuta umitashumta na umiseta junga sana hilo jamaa akapige kura kenya kwao hapa tanzania Rais ni Lowassa 2015 hataki arudi kwao kenya.
 
Aliyewahi kuwa waziri wa elimu na utamaduni ktk serikali ya Benjamin W. Mkapa ndugu joseph Mungai amesema shule za sekondari za kata hazikujengwa na Lowassa.

Joseph Mungai amesema sijawahi kuona tangu nizaliwe kuona baadhi ya watu wanamawazo ya mgando na akili za kusahau lini Lowassa alijenga shule za kata? Mimi ndiye nilikuwa waziri wa elimu na utamaduni kwa miaka nanne.

Shule za kata zilijengwa na nguvu za wananchi wenyewe serikali ya awamu ya 3 chini ya mkapa ndio ilihamazisha kila kata kuwe na shule ya sekondari ya kata.

Nikiwa waziri wa elimu wakati huo niliteua kikosi kazi kila mkoa wakuu wa mikoa niliwaagiza kuhamazisha wananchi kila kata kujenga shule ya kata ndio maana baadhi ya shule hizo ziliitwa majina ya wakuu wa mikoa.

Wakati mkapa hajamaliza muda wake wa uongozi alifungua shule za kata nyingi sana nchi nzima na zingine aliziwekea mawe ya msingi akiwepo waziri mkuu sumaye naye alifungua shule hizo nikiwepo mimi nilifungua sana hizo shule nikiwa waziri mwenye dhamana.

Wakati kikwete anaingia madarakani alizikuta shule za sekondari za kata zikiendelea kujengwa nchi nzima kwa nguvu za wananchi wenyewe kwa kujitolea.

Leo hii Lowasaa anawadanganya wananchi alijenga shule za kata anawatuma vibaraka waseme yeye ndiye aliyejenga shule hizo wakati tulioshiriki ujenzi wa shule tupo tukaye kimya siwezi kukaa kimya.

Watanzania kuweni macho sana na wasaka urais wa maendeleo yote serikali ndio inayafanya kwa kodi za wananchi.

Kuna watu kwenye mitandao ya kijamii wanatumika kumsafisha Lowassa kibaka mchafu mwenye matongo tongo ya kila aina ya uchafu mwl. Nyerere aliwahi kusema kipofu mwenye kichwa kikubwa ndani ya kichwa chake hakuna akili mtu huyo hawezi kuona uchafu na wizi wa Lowassa.

Wapo baadhi ya watu wanasema Lowassa alijenga chuo kikuu cha Dodoma chuo gani Lowassa alijenga?

Wakati wa ujenzi wa chuo kikuu Dodoma mimi na waziri wa elimu ya juu Piyus Ng'wandu tuliitwa na Rais mkapa IKULU tuliambiwa kutafuta eneo la ujenzi wa chuo kikuu Dodoma kesho yake tulienda Dodoma tulikutana wanakijiji wa maeneo hayo kilipo jengwa chuo hicho.

Wananchi walikubali kuyaachia maeneo yao kila mwananchi alilipwa hela na serikali ujenzi wa chuo hicho ulianza kufyeka sehemu za mistu serikali ilisimamisha kwanza ujenzi ili upite uchaguzi mkuu ndio ulimweka kikwete madarakani.

Bajeti iliyokuwa imepangwa kwenye ujenzi wa chuo hicho pesa zilitumika kujenga nyumba ya Rais mkapa muda wake wa uongozi ulikuwa karibu kuisha pia zilitumika kumalizia ujenzi wa ukumbi wa BUNGE Lowassa akiwa waziri wa maji na mifugo.

Yaani huu ni uongo usioweza kuvumilika kwanini mnamchafua Lowassa kwa kiwango hiki, Wote ni mashahidi kuwa eneo LA chuo kikuu Dodoma lilikua ni eneo LA ccm ambalo iliamua kuwapa serikali, sasa Leo inakuaje uje kutwambia kuwa serikali ilienda kunegotiate na wananchi?? Munghai mwenyewe anayajua madudu makubwa aliyoyafanya katika wizara , tunachokitambua sisi ni kwamba Lowassa ndiye mkombozi wa Elimu ya Tanzania na tunamtaka awe rais wa nchi yetu ya Tanzania 2015-2025
 
sasa mbona ccm mlimpa uwaziri,kweli nyie wendawazimu
Duh mimi mwendawazimu tena?Uliwahi kuniona nikiwa ktk Ushirika wa sisiemu?Ni lini ktk historia uliwahi kusikia sisiemu wako makini.kwani Jenerali Ulimwengu naye si aliwahi kuwa mkuu wa wilaya baadaye kaanza kuikosoa serikali sikivu wakasema siyo raiya?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom