Mungai aja juu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mungai aja juu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bubu Msemaovyo, Nov 25, 2008.

 1. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  2008-11-24 16:48:04
  Na Emmanuel Lengwa, Jijini


  Mbunge wa CCM wa jimbo la Mufindi Kaskazini, Mheshimiwa Joseph James Mungai, ambaye Ijumaa wiki iliyopita alilipukiwa na mkazi mmoja wa Jijini, akimtuhumu kwamba ni fisadi, ameeleza kusikitishwa kwake na kauli hiyo, na akasema madai hayo siyo ya kweli.

  Tuhuma hizo zilielekezwa kwake na Bw. Renatus Mkinga wakati akichangia mada kwenye kipindi cha Kipimajoto, kinachorushwa `live` na kituo cha luninga cha ITV.

  Katika madai yake, Bw. Mkinga alidai kuwa Mhe. Mungai akiwa Wizara ya Elimu na Utamaduni, ulitokea wizi wa fedha zaidi ya shilingi bilioni tatu , mali ya wizara hiyo.

  Akadai kuwa punde tu wizi huo ulipotokea, mfanyakazi mmoja wa Wizara hiyo ambaye Bw. Mkinga hakumtaja jina, aligundua na kutoa taarifa ili hatua zaidi zichukuliwe.

  Bw. Mkinga alizidi kudai kuwa badala ya Waziri Mungai kufuatilia taarifa hizo, alikanusha kuwa hakuna wizi uliotokea na kuchukua hatua ya kumtimua kazi mfanyakazi huyo aliyebaini upotevu wa fedha.

  Hata hivyo Mhe. Mungai leo amenusha madai hayo.
  ``Kamwe sijawahi kutuhumiwa kwa jambo lolote…hilo lililosemwa silijui wala halijawahi kunitokea,`` amesema Mheshimiwa Mungai.

  Amesema wakati akiwa Waziri wa Elimu na Utamaduni, aliiongoza wizara hiyo kwa uadilifu na uzalendo mkubwa kwa maslahi ya taifa na hakuwahi kufanya hujuma ya aina yeyote.

  Kipindi hicho ya Kipimajoto kinachorushwa na ITV kila Ijumaa, wiki iliyopita kilikuwa kikijadili mada ya ``Nini kifanyike kupata suluhu ya migomo ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu``.

  SOURCE: Alasiri


  Hajamalizia maswali mengine na je mfanyakazi aliyefichua siri hii ya wizi alimtimua???...........Mafisadi Bwana....!!!
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Hapo kuna kitu....wakichimba tutajua ukweli...
   
 3. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2008
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,219
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Ni kweli huyo jamaa aliyefichua wizi huo wa bilioni 3 alitilmuliwa kazi kimajungu majungu. Huyu jamaa alikuwa ni kigogo na mzalendo mzuri sana wa pale wizarani. Watu wa pale wizara ya elimu walimpigia debe bovu kwa Kikwete, na jamaa akaandikiwa barua ya kufukuzwa kazi na hao hao wabaya wake, ambao walii forward barua hiyo kwa rais kwa ajili ya approval. Ikawa approved. Lakini kutokana na malamiko ya wazalendo wengine pale wizarani kwamba jamaa kaonewa, ikabidi ile ishu ichunguzwe upya. Ikachunguzwa na kugundua kuwa jamaa kafukuzwa kimakosa (kitu ambacho Kikwete alikiri hadharani mara nyingi sana). Baadaye, Kikwete akaifuta barua hiyo ya kumfukuza kazi jamaa, baada ya kugundua kuwa aliuziwa mbuzi kwenye gunia kwa kumfukuza kwa makosa. Hivyo jamaa akastaafishwa kwa maslahi ya umma na kulipwa mafao yake. Hii habari tulishaijadili sana hapa JF mwaka juzi 2006, ngoja niipekue, nikiikuta nitakuja nayo.
  Huyo bwana aliyemlipua Mungai yuko sahihi, hii soo wakati ikitokea ilikuwa ni wakati wa Mungai.
  Sio uwongo.
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Tuletee hiyo taarifa ili twende pamoja na tujadili kitu ambacho tuna taarifa kamili, kuliko kuwa na vipande vipande vya habari.
   
 5. M

  MpiganajiNambaMoja Member

  #5
  Nov 25, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungai anadai aliongoza wizara ya Elimu kwa unyenyekevu na kwa kuzingatia maslahi ya Taifa. Je kuvuruga mitaala ya Elimu, kwa mfano kuunganisha Fizikia na Chemia ilikuwa kwa maslahi ya Taifa. Kwa nini mwandishi wa hiyo habari asinge mtupi hilo swali pia?
   
 6. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Sawa, sasa tuanzihapo kwenye hayo mabillion yaliopotea....
   
 7. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Uongozi mmbovu haukufanyi kuwa FISADI
   
 8. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2008
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280

  waandishi wetu wengine ndo hivyo tena..hawajiandai kwa mahojiano,, kwa maana ya kuwa hawasomi kwanza kabla ya kwenda huko.....
   
 9. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwa kawaida wahenga wanasema mwizi hata umkute na furushi la wizi bado ukimuliza umeiba atakataa. Sasa sisemi hivi kumshurutisha mh Mungai kuwa nae alifisadi nchi. Nikweli kakataa tuhuma, basi mh. tunaomba maelezo juu ya huyu mfanyakazi mzalendo anaesemwa kuwa alifukuzwa kazi kwa kutoa taarifa za kizalendo. Je ni kweli alifukuzawa na kama ndivyo kwa kosa gani?
   
 10. Kiungani

  Kiungani JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2008
  Joined: Feb 2, 2007
  Messages: 274
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu, naona hapa unachanganya issues. Huyo unayemzungumzia kuwa aliandikiwa barua ya kufukuzwa na baadaye kubadilishwa kuwa ya kustaafishwa, hausiani na whistleblowing ya hiyo bilioni 3.

  Huyo aliyestaafiswa alikuwa ni mtu wa Kapuya na baada ya Mungai kuingia, Kapuya alimkingia kifua jamaa abaki pale pale Elimu kwa wadhifa ule ule. Mungai akaona hiyo ngoma hainogi, kwani naye alitaka kuweka mtu wake pale kulinda masilahi yake. Akampa jamaa wa Kapuya offer ya u-REO Mwanza, jamaa akatema. Akaipeleka issue kwa Lowassa, akapewa go-ahead kuwa anaweza kumpagia kazi nyingine. Kwa kumkomoa akampangia u-DEO kule kwao jamaa Rukwa.
  Jamaa akaenda kwa Kapuya, halafu Magogoni kwa Muungwana, lakini ngoma ikarudishwa kwa EL. Vuta nikuvute, suluhu ikawa jamaa akubali kustaafu na akalipwa haki zake zote, japo alikuwa bado miaka 2 kufikia kustaafu.

  Hiyo ya billion 3 ni nyingine na inesemekana ilianzia wakati wa Kapuya hadi wa Mungai. Mama Six inasemekana alisema yeye hataki kuingilia hiyo issue, ikapoa kwa muda.

  Ila ufisadi wake mwingine Mungai ni wakati akiwa Mambo ya Ndani, alitoa vibali vya kazi na makazi kama njungu kwa jamaa wa Kenya, haswa wa Kikuyu, na hawa jamaa wamejaa Iringa na Mufindi kama wako Nakuru. Kuna mmoja anaitwa Njoroge Mungai (sijui kama ni ndugu yake kabisa au jina tu) ndiye sasa hivi anaendesha ile shule ya Mama Mungai pale Mafinga, naye huyo Njoroge kaajiri nusu ya walimu kutoka Kenya na anawafukuza walimu wa Tanzania kila leo. Huyu Njoroge akisema kitu Mungai anafanya bila pingamizi.

  Njoroge ana rafiki yake mwingine anaitwa Ngakumo lakini inasemekana amerudi Kenya baada ya kupata utajiri wa haraka haraka na usioeleweka.

  Huyu Njoroge na Ngakumo wakishirikiana na yule mdogo wake Mungai kuna kitu cha siri sana wanafanya pale Mufindi. Kwani Mungai anaweza kufika Mafinga usiku usiku, na ataonana na hao watatu tu na kisha anaondoka tena usiku usiku kurudi Iringa kwa yule mke mdogo wa kiburushi. Jimbo limebaki jina tu, wala haonekani kabisa.
   
 11. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kwa wanaojua historia ya Mungai, huyu Mzee mwenyewe asili yake Kenya, sema ndiyo wametoka zamani sana huko.
   
 12. K

  Koba JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ....wengi wao hawana shule wala idea na hiyo kazi ya uandishi zaidi ya kuandika andika porojo za mtaani tuu!
   
 13. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #13
  Nov 26, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Jamani JF huwa hawalali hebu mlioko huko fuatilieni mgundue nini anachokifanya huyu Bwana Mungai. Fisadi wa siku nyingi ambaye kama Nyerere asingefariki kamwe hangekuwa waziri tena kwa alivyo abuse ofisi yake enzi za Nyerere. Ni Mkapa na ubishi wake aliamua kumrudisha madarakani, another abuse of power
   
 14. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #14
  Nov 26, 2008
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,219
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee ana mengi sana mabovu ambayo ameyafanya akiwa waziri wa elimu. Kama mnakumbuka, kuna wakati walibadilisha sana mitaala ya shule za msingi, na dili ilikuwa ni kwamba, alikuwa anakula na wachapishaji wa vitabu, ambao walipewa zile tenda za kuchapa vitabu hivyo.
  Mengi yaja.
   
 15. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #15
  Nov 26, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Joseph Mungai ana sifa za ufisadi kote alikofanya kazi; alipokuwa kilimo hapa majuzi alilazimisha mhindi mmoja anaitwa Mahesh Patel, apunguziwe bei ya kununulia shamba la Kapunga kwa mamilioni ya shillingi na alikuwa anaifuatilia transaction hii mwenyewe pale PSRC!! Iliamuliwa kuwa hilo shamba lingeuzwa kwa bei ya juu lakini huyu bwana aliingilia kati kuwa apunguziwe ingawa mhindi alikwishakubali kulipa bei aliyoambiwa; inasemekana alikatiwa pochi kubwa tu ndio maana ameanza kujenga block of Flats hapo Kawe!! Huyu ni fisadi siku nyingi na asili yake ni mkikuyu kwahiyo sioni ajabu kuwapa vibali wakikuyu wenzie.!!
   
Loading...