Mume wangu nataka mtoto

thebogo055

Member
Jun 22, 2020
19
176
Alisikika mke wangu baada ya maongezi mafupi.. nikamuuliza kulikoni unataka mtoto ghafla hivyo? Akaniambia nimetoka home mama akaniuliza vipI tayarI tumboni.. pia mashangazi wakaanza kuniambia mhh umeishi na mumeo mpaka sasa haujashika mimba vipi kuna tatizo!?

Hayo ni maneno ya ndugu wa mke wangu baada ya kutoka kwao kwenye shughuli ya sendoff ya dada yake. Nikafikiria nikaona jinsi jamii inavyo pressurise mabinti kupata watoto ingali bado hawajajipanga kimaisha..

Huwezi kumwambia mwanao unataka mjukuu wakati ndio kwanza yupo kwenye ndoa ya miezi mitatu...

Watoto wapo tu kwanza tujenge maisha atleast hata mwaka mmoja au zaidi ndio tuanze kufikiria kuongeza familia ili hata huyo mjukuu akija akute mazingira mazuri.
...
 
Zaeni mtoto fasta. Kwanza maisha yanajengwaje? Maisha ni pale ulipozaliwa ndio yameshajengwa hivyo. Kuna umuhimu sana wa kuzaa mapema binafsi mie na mtoto wangu wa kwanza tumepishana miaka 20 tu. Imagine when i was 40 he was 20. Sasa hivi anafanya kazi nimeanza kula posho zake ujanani kabisa
 
Pia karama haipangiwi bali hufanya sawa na msukumo wa ndani mkuu
Alisikika mke wangu baada ya maongezi mafupi.. nikamuuliza kulikoni unataka mtoto ghafla hivyo!??

Akaniambia nimetoka home mama akaniuliza vip tayar tumboni.. pia mashangazi wakaanza kuniambia mhh umeish na mumeo mpaka sasa haujashika mimba vip kuna tatizo!??

Hayo ni maneno ya ndugu wa mke wangu baada ya kutoka kwao kwenye shughuli ya sendoff ya dada yake...

Nikafikiria nikaona jins jamii inavyo pressurise mabinti kupata watoto ingali bado hawajajipanga kimaisha..

Huwezi kumwambia mwanao unataka mjukuu wakat ndo kwanza yupo kwenye ndoa ya miezi mitatu...

Watoto wapo tu kwanza tujenge maisha atleast hata mwaka mmoja au zaidi ndio tuanze kufikiria kuongeza familia ili hata huyo mjukuu akija akute mazingira mazuri
...
unawajibu kupitia hapa
 
Mkuu naona unaleta porojo tu, Kama suala LA kujipanga ulitakiwa kujipanga kabla huajoa aisee, ukishaoa ni vyema ukapata hata mtoto mmoja tu huku ukiendelea kujipanga na kuandaa maisha ya wanao , mkishirikiana na mkeo ,
Angalia tu asije akkatokea aliyejipanga akamjaza mimba mkeo maana mpaka hapo mna mawazo tofauti tayari
 
Nipo na mke wangu mwaka wa pili huu hatuna mtoto hiyo pressure tunayopata si ndogo,
Yaan mpaka mnakosa raha, lakini si kwamba hatutaki mtoto tunataka sana ila Mungu nae ana kudra zake
Poleni,
 
Ndugu wa mwanamke wanazingua ila wewe imezingua zaidi mjomba.

Et unajipanga kua na maisha mazuri ya familia wakati familia yenyewe huna

Piga mzigo kabla wajuba hawajakuwahi na kukuacha ulelee famia isiyo yako..

Chelewa chelewa ukute mwana sio wako (wahenga's voice)
 
Back
Top Bottom