Mume wangu anatembea na mdogo wangu

Kwa kuwa umesema kuwa mdogo wako ni mcharuko (malaya)

Ni wazi kuwa alimfanyia mumeo vtuko vya ushawishi ambavyo ni nadra wanaume kuvikwepa kwa sababu wanaume ni dhaifu.....

Endelea kuuguza maumivu yakiisha rudi kwa mumeo ila mdogo wako mrudishe kwao
 
Wanaume Usimpelekee Asali, hataiacja, Siyo kosa la mmeo ni lako
Kaaa hapo kwa Dadako
Maumivu Yakiisha Rudi Kwako
Ila Kuwa makini pia, mme wa dadako asijekutaka na ww
Umeua Mkali... Kweli Tupu Anaezaliwa Nae Kiboga... Mbona Clinton Alimla Monica Lewinsky Lakini Mama Hillary Akatulia? Tena Majuu Watu Ambao Hawatakag Shobo Na Vyeo Au Hela? Waiiiii Sembuse Wabongo Eti Tuna Wivu?

Mimi Mke Wangu Nishamwambia Aende Kutafuta Anachotaka Lakini Arudi Maskani Mapema Kama Ataona Shoo Ni Ya Kizembeee... Period! Unashindana Na Kumrizisha Mwanamke?
1. Kucha Kapewa Bure, Kaweka BANDIA?
2. Nywele Kapewa Kaweka Bandia?.
3. Matako Nayo Mchina, Wengine Wanavaa Majalada Ili Aonekane Ana Chura? C Kila Mwanaume Anapenda Chura!
4. Kope Kakwangua Kachora Michoro Gani Sijui!
5. Nywele Kila Mtu Anazo, Lakini Mwanamke Atavaa Wig, Badala Ya Kufuga Zake!


.... Waiiiiiii! Mwanamke Rudi Home Bhana Usinchefue Mie Utaliwa Kiboga Na Mikunguru Mingine, Kumbuka Wanaume Ni Wachache, Tena Waliopo Hawaoi...
 
(Hichi ni kisa cha rafiki yangu wa karibu saana)



Habarini za usiku mkali wanajamvi its time for DAKU,

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa Miaka 28 na nimeolewa. Mume wangu ana miaka 42. MUNGU amenibariki na watoto Wawili Mapacha wa Kike wenye umri wa miaka minne.

Ndoa yangu ni ya miaka mitano ila naona hamna Ndoa tena baada ya kugundua kuwa Mume wangu amekuwa akinisaliti na mdogo wangu wa mwisho mwenye umri wa miaka 20.

Mdogo wangu huyo wa mwisho alikuwa akiwasumbua sana wazazi huko nyumbani. Ni mtu wa kutoroka nyumbani usiku kwenda kwa wanaume tofauti tofauti na kumbi za starehe pamoja na kutembea na waume za watu.

Nilivyoona anazidi kuwafedhehesha wazazi wangu na ukizingatia umri wao umeenda sana, nikaamua kumchukua huko Mkoani na kumleta hapa Dar es salaam ili nimsimamie vizuri mimi mwenyewe.

Ambacho sikujua ni kwamba, kumleta hapa Kwangu ilikuwa ni kosa kubwa mno katika mustakabali wa Ndoa yangu. Kwanini sikujua kwamba Mume wangu angejivua ufahamu na kuanza kutembea na mdogo wangu?

Sasa hivi nimeamini kabisa kwamba baadhi ya wanaume hufikiria kwa kutumia nanihii zao tu na wala sio ubongo maana haiwezekani kabisa na haiingii akilini kwa mume wangu kunifanyia vile kwa sababu sikuwahi hata siku moja kutomridhisha pale aliponihitaji.

Niliyajua yote hayo siku fulani ambapo nilikuwa nimetoka kazini na kumkuta mdogo wangu akigaragara chini huku akitokwa na damu sehemu zake za siri.

Nilishtuka mno na kumuuliza amepatwa na jambo gani lakini hakunipa jibu la kueleweka. Niliingiwa na hofu mno na kuamua kukodi tax na kumkimbiza hospitali. L popakini tulipofika hali yake ilikuwa mbaya mno na kupelekea kupelekwa chumba cha Wagonjwa mahututi (ICU).

Nilimpigia simu Mume wangu aje hospitalini lakini alinipa sababu ambazo zisizo na msingi za kutokuja. Sikuelewa ni nini kilichokua kikiendelea.

Nikampigia simu Kaka yetu Mkubwa na Dada yangu ambao wao wanaishi hapa hapa Mjini na wakaja haraka hospitalini.

Baada kama saa moja Daktari alitoka ICU na kutuita ofisini kwake. Akatueleza kuwa Mdogo wangu alikuwa akijaribu kutoa Mimba hivyo mirija ya falopian imeharibiwa vibaya kutokana na utoaji huo wa Mimba na inavyoonesha ametoa mimba mara kadhaa.

Nilishangaa mno, inawazekanaje wakati nilimbana asiwe na uhuru kama aliokuwa nao wakati yupo kwa wazazi.

Baadaye tukaenda kumtazama wodini. Alivyotuona tu alianza kulia huku akituomba Msamaha. Kaka yangu akamwambia akae kimya na atueleze ni nani alimpa Mimba na kwanini atoe bila kuniambia.

Ndipo nilipopata Mshtuko mkubwa katika maisha yangu, baada ya kunieleza kuwa Mume wangu ndiye aliyempa Mimba na asubuhi ile alimpeleka kwa daktari kutoa Mimba. Na akakiri kuwa amekuwa akitembea nae tokea amefika pale nyumbani kwangu.

Ndipo nilipogundua kwanini nilipompigia simu aje hospitali aligoma na kutoa sababu zisizo na mashiko.

Kwakweli nilihisi Dunia inaniangukia. Nilivyorudi nyumbani na kumbananisha Mume wangu alikiri ni kweli alikuwa akitembea nae na ni mdogo wangu ndiye aliyemshawishi na akawa akiniomba msamaha.

Sikuwa na papara, nikaanza kukusanya mabegi yangu huku nikitokwa na machozi. Sio siri niliumia mno kwa kusalitiwa. Nilijiona sina thamani tena na nimeachwa uchi!!

Niliwabeba wanangu na kwenda kwa dada yangu ambako niko huko kwa mwezi sasa nikijaribu kujitibu maumivu na fedheha niliyoipata.

Mume wangu amekuwa akituma watu mbalimbali akiomba nimsamehe na kunibembeleza nirudi nyumbani lakini moyo umekataa kabisa. Nimekuwa nikimwambia amuoe tu mdogo wangu na waendelee na maisha.

Baadhi ya watu wamekuwa wakinieleza kuwa nimsamehe kwa ajili ya watoto lakini sioni kabisa sababu ya kuendelea kuishi nae. Namchukia na upendo haupo hata lepe.

Naomba ushauri, maamuzi niliyofanya ni sahihi? na nifanyaje kuondokana na maumivu nayoyapata kila siku kila nikumbukapo yaliyonikuta?
__________________________
Tatizo lenu wachaga mkishaolewa mnajisahau Sana.
 
Back
Top Bottom