Mume wangu anataka kuniingilia kinyume na maumbile

Mume wangu anataka kuniingilia kinyume na maumbile

Dada pole...kweli dunia imekua kama v shape....ondoka hapo,,,, atakuharibu huyooo
 
achana nae huyo nenda kapambane na maisha acha uoga tafuta kitu cha kufanya huo ni utumwa,
 
Huyu naye unamwita mume wako.. Hili ni huni tu jambazi na katili la kijinsia, report police lifungwe!
 
Hizi mada Fidel80 anaweza kutoa msaada. Dunia inaongozwa na shetani dalili zote zimepita na sasa dalili zilizoko hata hazikutabiriwa na manabii lakini zinatokea. Kuna mambo hata shetani hashiriki kumshawishi mtu ni mtu mwenyewe amegeuka shetani.

Tufunge macho tuombe.

Eee Mungu baba nakuomba ukapate kumgusa huyo mwanaume fedhuli akapate kushindwa katika jina la Yesu na kama akizidi Mungu naomba umnyanganye hiyo nguvu inayompa kiburi asichaji tena maisha.

Amen
Siku hizi maombi ya kufunga macho yamepitwa na wakati, nani anayetaka simu na pochi yake ziote mbawa bhana...

Kwanza wakati wewe unaongoza maombi mimi nilikuwa macho, nimeshuhudia watu humu wakikulaumu kwa kukataza haya mambo.
 
Ukoje.....siku zooote umekaa kimya wakati kila kituo cha polisi kuna dawati la jinsia na kuna TAWLA;TAMWA na asasi kibao zinazoweza kukuokoa na janga hilo. Halafu bila aibu ati leo unaandika jamvini...iweje wakati ashakuingilia zaidi ya mara moja nawe umekaa kimya????? AMKAAAA CHANGE NI WEWE NI MIMI NI SISI....TWAWEZA....
hii nimeitoa hapa MAISHA , MAPENZI, UREMBO: NISAIDIENI NDUGU ZANGU NAHISI KUCHANGANYIKIWA


sasa naona hii dometic violence imezidi jamani...stori ya Babra, haya huyu naye tena...sijui wanajamvi mnamshaurije?
 
kama hataki kukupa talaka nenda mahakamani ukaombe decree of divorce kwa hicho kitendo mahakama itakupa haraka na pia unaweza ukaenda kumshtaki maana hata sheria yetu (penal code) hairuhusu hilo tendo
 
Nadhan atakuwa alishaondoka jaman hii ilikuwa 2010
 
Aisee huyo mwanaume mwenzetu ametudhalilisha..kimantiki ukifanya hivyo kwa mkewe manake ndoa tena hakuna,.ni talaka tosha na inaonesha ampendi uwezi kuumgeuza mke wako kama unampenda kwa dhati....au mumewe ana matatizo ya akili i don't know what to say but nazani mwanamke akaripoti kwenye vituo husika na mumewe sheria ifate mkondo wake....manyanyaso ya kijinsia haya! Anaweza akaanza kwa joyce kiria email/cm zake ameweka hewani or anybody she think can solve the situation..
 
Sijui Hata Nianzie Wapi Kukushauri,tatizo La Ndoa Zetu Siku Hizi Nyie Wanawake Mnapenda Sana Wanaume Ambao Tayari Wana Nafuu Ya Kimaisha,hamtaki Kuanza Moja Na Wanaume,wewe Hukupata Muda Wa Kumchunguza Hadi Unaolewa? Kifupi Ni Kuwa Huyo Ni Shetani Kabisa,usisubiri Akupe Talaka,ondoka Kwake Haraka Sana Mungu Yupo Hatakuacha,ukizidi Kukaa Kwake Atakuharibu Ibilisi Huyo,nyie Wanawake Tamaa Zinawaponza Sana,ungeolewa Na Maskini Mwenzako Haya Yasingekupata,na Mungu Angewabariki Mkafanikiwa Zaidi.
 
Kumbe haya matukio yapo mengi sana.
Eti na yule dada aliyejaliwa mpododo(Grace) naye analalamika kutaka kuchezewa rafu na mpenzi wake.
 
kama hataki kukupa talaka nenda mahakamani ukaombe decree of divorce kwa hicho kitendo mahakama itakupa haraka na pia unaweza ukaenda kumshtaki maana hata sheria yetu (penal code) hairuhusu hilo tendo

Section 154
 
Asepe tu,talaka makaratasi tu,anateseka kisa kusubiri makaratasi!
 
alimlipue tu kwa wazazi wa pande zote 2, tatizo alishampa sasa dada anaona aibu ingekuwa hajampa ilikuwa amlipue, atulie atapata mume bora mwenye heshima na taadhima
 
Back
Top Bottom