Mume wangu anataka kuniingilia kinyume na maumbile

Kaizer

Platinum Member
Sep 16, 2008
25,320
17,822
MUME WANGU ANATAKA KUNIINGILIA KINYUME NA MAUMBILE

Habari dada violet, naamini u mzima kabisa, kwa upande wangu mimi si mzima kimwili lakini nahisi kiakili naelekea kuchanganyikiwa, tangu niolewe ni miezi sita sasa, lakini sina amani kabisa ndani ya nyumba yangu, kwakuwa mume wangu anataka kuniingilia kinyume na maumbile, hali ambayo mimi binafsi siipendi na naona ni dhambi kubwa sana. Mume wangu aliponioa hakuniambia kuwa anapenda kufanya kitendo kile, hakusema kabisa, ila nilishangaa siku ile ya ndoa usiku akaanza kuniambia uchafu huo, nilikasirika sana na nilimlilia na kumwambia kama ni ndoa na ife, mimi siwezi kufanya kitendo kile, kwa kipindi cha mwanzo alinielewa kabisa, kadri siku zinavyoenda hali inabadilika kila siku, ugomvi hauishi, matatizo kila kukicha,

Kuna siku ilikuwa usiku sana, aliniamsha kwa hasira na kusema kuwa yeye ameshindwa kulala na hakuta kucha kama sitampa anachokitaka, na kujisifia kuwa mbona wake wa marafiki zake wanawapa waume zao na hawajaharibikiwa? kwanini namimi nisimpe? msimamo wangu ulibaki pale pale,gafla alishuka kitandani na kuchukuwa mkanda wa suruali yake, akaanza kunipiga, niliumia sana, badae niliishiwa nguvu kabisa nikaanguka, alinigeuza na kuniingilia kinyume na maumbile, niliumia sana, nililia sana, na kulipokucha akaniambia taratibu tu utazowea, na kama ukikubali mimi nitakupa kila unachotaka, akaondoka

nililia sana, lakini kitendo kile niliona cha aibu sana kuwashirikisha watu, nikaona nitamdhalilisha mume wangu, niliamua kukaa kimya, ila mwili ulima sana nikatumia dawa za maumivu, aliporudi jioni akataka tena ili nizowee, nilikataa nikamwambia basi niache, nipe taraka yangu niondoke, alichokifanya akanipokonya mtaji wa biashara niliyokuwa nafanya (nina duka la nguo za kike) akachukuwa nguo zote dukani ambazo hadi leo sijui zilipo, akaniambia sikupi taraka, ukitaka uishi kwa amani nipe ninachokitaka, nililia sana, niliamua kumwacha na kuendela na msimamo wangu,

kuna siku niliumwa sana usiku tumbo, akanipeleka hospitali, waliponipima waliniambia nina uvimbe kwenye kizazi inabidi operation, basi tuliporudi nyumbani nikamwambia anipe pesa akasema utakufa, ukitaka pesa yangu nipe ninachokitaka kwanza, nilimgomea, basi tukawa tunaishi hivyo hivyo, hakuna tunachoshirikiana nae, nikipika anasusa kula, nguo anapeleka kwa dobi afue, apasi, kitandani hata shuka alibadilisha kila mtu na shuka lake, nilimsihi anipe taraka niondoke, akakataa, akasema ole wako uvujishe siri hii, nilikaa kwa mwezi tena, kurudi hospitali daktar akasema uvimbe unazidi kukua na maumivu yanaendelea kwa kasi, niliporudi nilimsihi sana akakataaa, niliamua kurudi kwetu, mama alifariki, nipo na baba tu, na baba hana uwezo wa kulipia operation hiyo, kesho yake mume wangu akanifata kwa baba na kutaka nirudi, hadi hapo baba hakua akijuwa lolote, nilirudi kwa mume wangu, lakini hali ikabaki pale pale, kuna siku usiku alinikandamiza kwa nguvu na kuniingilia tena, niliumia na kulia sana, kesho yake akanipa hela ya upasuaji, Mungu alinisaidia nikapona haraka, niliporudi nyumbani hali ni ile ile, ananiuliza hadi leo hujazowea tu? nikamwambia sahau huo uchafu, na kama nitarudia tena nitakuwa kichaa, basi toka siku ile hadi sasa sijui cha kufanya, nawaza nimwambie baba yangu? baba ni mgonjwa mgonjwa maana toka mama afariki mwaka juzi hali ya baba imekuwa si nzuri nahisi na umri nao, naogopa nikimstua anaweza hata kupoteza maisha, kwao amenipiga marufuku kusema. niliwahi kumuita rafiki yake kumuomba aongee na mwenzie, nilishangaa yule baba nae akanilaum mimi akasema kwanini unamkatili mwenzio hivi? mimi mwenyewe mke wangu anafanya hivyo? na tuna raha kabisa, unakosea sana, alipotoka pale akaenda kwa mume wangu kumwambia, jamani nilipigwa siku hiyo kama mwizi, na mapenzi yangu kwake yamepungua sana, talaka hataki kutoa, na hataki niondoke

Naombeni msaada wa mawazo ndugu zangu, naona ninakoelekea ni kuwa mwehu kabisa, sina furaha wala amani kwenye ndoa yangu, naamini nitashauriwa vizuri na ushauri huo nitaufanyia kazi,

asanteni sana

hii nimeitoa hapa http://beautytouchdar.blogspot.com/2010/01/nisaidieni-ndugu-zangu-nahisi.html

sasa naona hii dometic violence imezidi jamani...stori ya Babra, haya huyu naye tena...sijui wanajamvi mnamshaurije?
 
Hizi mada Fidel80 anaweza kutoa msaada. Dunia inaongozwa na shetani dalili zote zimepita na sasa dalili zilizoko hata hazikutabiriwa na manabii lakini zinatokea. Kuna mambo hata shetani hashiriki kumshawishi mtu ni mtu mwenyewe amegeuka shetani.

Tufunge macho tuombe.

Eee Mungu baba nakuomba ukapate kumgusa huyo mwanaume fedhuli akapate kushindwa katika jina la Yesu na kama akizidi Mungu naomba umnyanganye hiyo nguvu inayompa kiburi asichaji tena maisha.

Amen
 
Mhh! Shemeji! Mwambie amrudie Bwana Yesu tu ndio jibu.Mambo mengine ya dunia hii unaweza changanyikiwa.
Wengine wanatamani kuingia kwenye ndoa wakati huohuo wengine wanajuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuta kuingia kwenye ndoa.
Tuombe Mungu tu atunusuru.
 
Jamani kwa nini haondoki?kwani kabla hajaolewa na huyo firauni alikuwa haishi? alikuwa hali na kupumua hata kama ni kwa tabu? why put up with all this nonsense. kisa hela? coz naona ni financial wellbeing ndo inamtesa huyu dada. haoni kama huyo mpuuzi ni muuaji? yani mkewe anaumwa anamnyima pesa ya kujitibu eti kisa hajapewa tigo? and she cal that a husband? si ungetoka hadharani utuambie hata mimi mwanamke mwenzio ningejitolea na kuhamasisha wanawake wenzangu tukuchangie matibabu na hata mtaji ili kumwaibisha huyo firauni.
 
Hizi mada Fidel80 anaweza kutoa msaada. Dunia inaongozwa na shetani dalili zote zimepita na sasa dalili zilizoko hata hazikutabiriwa na manabii lakini zinatokea. Kuna mambo hata shetani hashiriki kumshawishi mtu ni mtu mwenyewe amegeuka shetani.

Tufunge macho tuombe.

Eee Mungu baba nakuomba ukapate kumgusa huyo mwanaume fedhuli akapate kushindwa katika jina la Yesu na kama akizidi Mungu naomba umnyanganye hiyo nguvu inayompa kiburi asichaji tena maisha.

Amen

Amen.
 
Mie nadhani swala zima hapo ni kuwashirikisha wazazi au afanye mamuzi ambayo hatakuja kujutia baadae kuondoka /au !!
 
1.HUYO SIYO MUME BALI NI..SIJUI HATA CHA KUSEMA!

2.Hakuolewa ndoa bali kajiingiza kwenye utumwa wa kisasa - contemporary slavery!

3.Bahati mbaya hajatuambia kama anampenda huyo mume bado au la maana hili nalo ni muhimu kulijua kabla ya kumshauri.Kitendo anachomfanyia ni ukatili uliokithiri maana umo kwenye ndoa na siyo uhusiano wa kihivihivi.

4.Ingekuwa mimi, ningeondoka maana hatakaa afurahie ndoa yake hata kidogo.Bahati mbaya hakuacha contacts zake tungemsaidia hata hayo matibabu yanayomfanya amng'ang'anie huyo shetwani!

5. Kuna mambo ya kuvumilia lakini siyo udhalilishaji wa kiwango hiki.Kitendo cha kuingiliwa kinyume ni kitendo kiovu na hata kiimani imekatazwa.Wanaokiuka basi wawe wamekubaliana wenyewe lakini siyo kulazimishana!
HUYO MWANAUME ALAANIWE NA SIKU YA KIYAMA AWE NI KUNI KATIKA TANURU LA KUUNGUZA WALIOHUKUMIWA JAHANAMU!
 
Jamani kwa nini haondoki?kwani kabla hajaolewa na huyo firauni alikuwa haishi? alikuwa hali na kupumua hata kama ni kwa tabu? why put up with all this nonsense. kisa hela? coz naona ni financial wellbeing ndo inamtesa huyu dada. haoni kama huyo mpuuzi ni muuaji? yani mkewe anaumwa anamnyima pesa ya kujitibu eti kisa hajapewa tigo? and she cal that a husband? si ungetoka hadharani utuambie hata mimi mwanamke mwenzio ningejitolea na kuhamasisha wanawake wenzangu tukuchangie matibabu na hata mtaji ili kumwaibisha huyo firauni.

Nadhani kwa mwendo huu hata ukiondoka au ukitoa talaka,hata Yesu mwenyewe atakubaliana kabisa.Huwezi Ng'ang'ania vitu kama hivo unasema eti niliapa kanisani.
 
Pole sana dada kwa matatizo uliyonayo.
Ulimwengu tulionao hivi sasa, si wakuishi katika hali uliyonayo hata kidogo. Jambo lakwanza unalotakiwa kumfahamisha mumeo ni kwamba, wewe ni binadamu, na unahitaji raha na amani kwa kufanya kitu ambacho kitakufurahisha kwanza wewe na pili yeye, huu si wakati wa utumwa wa mapenzi hata kidogo.

Pia umweleze kwamba kitendo cha yeye kukupiga kwanza ni kinyume cha sheria na pili ni kinyume cha haki za binadamu wakiwemo wanawake. Hivyo basi mfahamishe kuwa akiendeea kukupiga utamfikisha kwenye vyombo vya sheria na kuacha sheria ichukue mkondo wake maramoja.

Kama akiacha kukupiga ila akaendelea kukunyanyasa kwa namna nyingine yoyote, itakuwa nia wakati muafaka wa kuliwasilisha swala hili kwa wazazi wake, na wala hatothubutu kukugusa na akifanya hivyo bila woga umfikishe kwenye vyombo vya sheria.
Wazi wazi waelwze wazazi wake(hasa mama) kuhusu hiyo tabia ya mtoto wao ,na ni jinsi gani inakunyima raha. Bila shaka wazazi watachukua hatua yoyote. Asipobadilika nenda kadai talaka yako mahakamani na utapewa uachane na huyo baladhuli.

Pole sana Dada
 
Utumwa wa kiuchumi ndio tatizo kuu na pia amesubiria tatizo likue ndo alikabili, sasa limeshazaa na kujukuu.

Ndo maana kila siku tunasisitizwa kuwawezesha wanawake wajitegemee. Ukijitegemea utaweza kuyakontroo maisha yako bila kumsubiria mtu yeyote.
 
1.HUYO SIYO MUME BALI NI..SIJUI HATA CHA KUSEMA!

2.Hakuolewa ndoa bali kajiingiza kwenye utumwa wa kisasa - contemporary slavery!

3.Bahati mbaya hajatuambia kama anampenda huyo mume bado au la maana hili nalo ni muhimu kulijua kabla ya kumshauri.Kitendo anachomfanyia ni ukatili uliokithiri maana umo kwenye ndoa na siyo uhusiano wa kihivihivi.

4.Ingekuwa mimi, ningeondoka maana hatakaa afurahie ndoa yake hata kidogo.Bahati mbaya hakuacha contacts zake tungemsaidia hata hayo matibabu yanayomfanya amng'ang'anie huyo shetwani!

5. Kuna mambo ya kuvumilia lakini siyo udhalilishaji wa kiwango hiki.Kitendo cha kuingiliwa kinyume ni kitendo kiovu na hata kiimani imekatazwa.Wanaokiuka basi wawe wamekubaliana wenyewe lakini siyo kulazimishana!
HUYO MWANAUME ALAANIWE NA SIKU YA KIYAMA AWE NI KUNI KATIKA TANURU LA KUUNGUZA WALIOHUKUMIWA JAHANAMU!

well said. ningekua mimi kesho yake ningemuanika ulimwengu wote umjue
 
Jamani kwa nini haondoki?kwani kabla hajaolewa na huyo firauni alikuwa haishi? alikuwa hali na kupumua hata kama ni kwa tabu? why put up with all this nonsense. kisa hela? coz naona ni financial wellbeing ndo inamtesa huyu dada. haoni kama huyo mpuuzi ni muuaji? yani mkewe anaumwa anamnyima pesa ya kujitibu eti kisa hajapewa tigo? and she cal that a husband? si ungetoka hadharani utuambie hata mimi mwanamke mwenzio ningejitolea na kuhamasisha wanawake wenzangu tukuchangie matibabu na hata mtaji ili kumwaibisha huyo firauni.

Asiondoke tu bila kudai talaka, kwani akijataka olewa na binadamu wa kweli huyu Nduli anaweza kuja weka pingamizi!!
 
nitamvumilia mume wangu kwa chochote lakini sio hili jamani, zito sana!!! huyo mama angeondoka tu aendelee na maisha yake.

its not the end of the world!!! na hilo karatasi analomg'ang'ana kulisubiri litamababishia mengi!!!!
 
Yohana 14 : 1-18 .....aliyeniona mimi amemuona baba yangu aliyenipeleka....Filipo akamwambia utoneshe Baba yatutosha,.....Filipo nimekuwa pamoja nanyi hata usinijue?.....(wapo watu wanao kataa Yesu si Mungu ili watende mambo kama hayo kwa wake zao....imeandikwa mambo yote yatapita lakini neno litasimama....
E Mungu baba kwa jina la Yesu aliye hai, wewe ndiye mwenye uwezo wa kumnusuru dada huyu katika hali ile mbaya naagiza malaika zako wa Mbinguni kumwokoa na ufirauni wa mume kwa jina la Yesu, .....ukasema kaeni ndani yangu nami ndani yenu ili muwe salama, ninaamini hatotendewa tena matendo hayo machafu tangu sasa kwa jina la Yesu Ameeni
 
Asiondoke tu bila kudai talaka, kwani akijataka olewa na binadamu wa kweli huyu Nduli anaweza kuja weka pingamizi!!

talaka haiwezi kudaiwa mpaka uwepo ndani ya matrimonial home?????? so unaona ni vizuri aendelee ku-put up na huo ushenzi akingojea karatasi au????
 
alishuka kitandani na kuchukuwa mkanda wa suruali yake, akaanza kunipiga, niliumia sana, badae niliishiwa nguvu kabisa nikaanguka, alinigeuza na kuniingilia kinyume na maumbile
so sorry mama mmmmmh....trust in God alone...He will make a way for you where seem to be no way...
 
Hali hii ni ya kawaida sana katika familia nyingi, si mara ya kwanza kusikia visa vya namna hii katika jamii zetu, ule wakati wa kumtumia mwanamke kama chombo cha starehe umepita, hawa ni mama zetu jamani ni lazima tuwape heshima inayostahili.,huu ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa kweli unaotokana na kuiga tamaduni za watu wa magharibi ambao kwao mchezo huu wa kuruka ukuta si jambo la ajabu sana.

Dada huyu inabidi avunje ukimya, hakuolewa ili akateseke hivyo, alichofuata kwa huyo mume ni maisha ya upendo na amani, sasa kama hivyo vyote vimetoweka hiyo ndoa ina maana gani tena jamani.,lazima awe na moyo wa kijasiri, tena wa kufanya maamuzi mazito vinginevyo ataendelea kuumia kwa kuchelea aibu.
 
Jamani hata kama ni ndoa hapana, huyu dada anahaki ya kutengana na huyo so called Mume "which I dont see" kwa kosa hilo la kinyama.

Dada wewe songa mbele achana na huyo firauni shetani angalia ustarabu wako mapema kabla mambo hajaharibika, alafu good thing hauna mtoto u can fight and struggle na utatoka tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom