Mume wangu ana michepuko hamsini kidogo

Mume wangu ana michepuko hamsini kidogo

moniccca

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2015
Posts
2,383
Reaction score
3,287
Habari za weekend wakuu,

Nimekuwa na wakati mgumu kwa muda mrefu bila kufurahia ndoa yangu tangu nimeolewa. Ni hivi mume wangu amekuwa ni mtu wa michepuko isiyo na idadi kibaya zaidi hakuna beki tatu atakakuja asiye tembea nae hata awe mbaya kiasi gani. Kilichonifanya nilete uzi huu humu kwa lengo la kupata ushauri.

Ni kuwa asubuhi niliamka vyema na kwakuwa ni weekend nilimuuliza ana ratiba gani akajibu hana ratiba yeyote atakuwepo tu nyumbani.Ilipofika saa nne tukapata mgeni ambaye ni Jirani, ni baba mtu mzima sana alikuja kumuonya mume wangu ache tabia ya kutembea na mkewe.

Wakati naendelea kutafakari hilo nikapokea ujumbe kwenye simu yangu kutoka kwa mwanamke aliyejitambulisha kama mpenzi wa mume wangu na anamuulizia kama yupo, nilimwambia akakana kabisa. Baada ya muda kidogo akapokea simu ambayo hakutaka nisikie akaenda kuongelea nje ya geti alipomaliza tu akaniaga nikamzuia asiondoke lakini akaondoka kibabe.

Binfsi sioni maana ya kufuga malaya kama huyo, anakula vyangu, hela anatumia zangu anaishi kwenye nyumba yangu halafu anifanye mie kama spare tyre?

Naombeni ushauri kuna haja ya kuendelea na mtu kama hayu? Nilidhani kumpa gari ndo kunamfanya aweweseke hivyo nikaamua kuliuza gari lake mwze wa tano lakini bado hakomi.

Nipeni dawa nimkomeshe.
 
Pole, nafikir unasubiria ukimw, huyo mumewe hakueshimu, hakuthamini na kunguru hafugiki ila ukichukua hx Ata kabla hajaoa alikua Malaya huyo, nikusii uwambie wazaz , wamshaur, viongoz wako wa din, ndugu, marafik, asipobadilika ndio ubebe beg lako, Lakin wanaume mjifunze na nying, Yan mke pesa zake wala, magar, afu upo kwake, house girl unapitia, folen Za kutosha jaman na Hao wanawake wanamoyo, y mtu humtaki umfanyie makusud hivyo mwambie ckutaki aanze maisha yake, ila wanawake jifunzeni mwanaume akifikia hatua hiyo huna aja yakuomba ushaur uku, unatakiwa ujiulize unaitaji kuishi bado au kufa na ukimw, fanya mamuz magumu kwa faida yako na kwa faida ya watoto wako kama mmezaa nae, pili tambua tabia ya mwanaume habadiliki Ata cku moja, Malaya kabla ya ndoa Ata bada ya ndoa ataendelea
 
ww ulimpendea huohuo umalaya saiv hutaki tena lol,embu kumbuka vzr kipindi cha mahusiano
 
Nakushauri tulia tu Utunze Mali za Watoto wenu,,Bila shaka atakuwa Anahela ndio maana Mpo wengi
 
Pole, nafikir unasubiria ukimw, huyo mumewe hakueshimu, hakuthamini na kunguru hafugiki ila ukichukua hx Ata kabla hajaoa alikua Malaya huyo, nikusii uwambie wazaz , wamshaur, viongoz wako wa din, ndugu, marafik, asipobadilika ndio ubebe beg lako, Lakin wanaume mjifunze na nying, Yan mke pesa zake wala, magar, afu upo kwake, house girl unapitia, folen Za kutosha jaman na Hao wanawake wanamoyo, y mtu humtaki umfanyie makusud hivyo mwambie ckutaki aanze maisha yake, ila wanawake jifunzeni mwanaume akifikia hatua hiyo huna aja yakuomba ushaur uku, unatakiwa ujiulize unaitaji kuishi bado au kufa na ukimw, fanya mamuz magumu kwa faida yako na kwa faida ya watoto wako kama mmezaa nae, pili tambua tabia ya mwanaume habadiliki Ata cku moja, Malaya kabla ya ndoa Ata bada ya ndoa ataendelea
Asante kwa ushauri wako
 
Nawewe chepukia kwangu ili tuuane zetu vizuri kisha twende mbinguni
 
Nakushauri tulia tu Utunze Mali za Watoto wenu,,Bila shaka atakuwa Anahela ndio maana Mpo wengi
Uzuri sijazaa nae na hata hela hana ananiibia kwenye biashara zangu tu
 
Kaa chini muongee usikute kuna manjonjo umepunguza
 
Muache Dada yan kitendo cha kumpa hela mwanaume Mmmh m siwez fanya yako dia huyo achana nae
 
Back
Top Bottom