Mume wa Maana Usipokuwa naye tu, Ukimpata...!!!

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,116
Namasteeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! (Mwaka mpya salamu mpya! mambo ya kuchukuchu hotaheeeee!)

Mazungumzo Kabla ya Habari!!!!! (Baada ya BAN)

Wanga wote miniwacheeeee hii 2014, SITAKI SHARI NA MTU! Hamlazimishiwi kusoma hizi thread! Ukiona vipi Jikate! Msione nimetoka BAN mkazani nina Mswalie Mtume sinaaaaaaaaa! Mwendo ule ule NAWACHAMBA WIMA WIMA, Mara million nipigwe BAN DAILY kuliko kuwakopesha! Ukileta za kuleta unachambwa uzuri na UKASHTAKI VIZURI KWA MODES! Thread kibaooo WANGA msiijazie nzi humu!!!!!!!! Sijawaita kwa kadi ya mwaliko humu! Mnituweeeeeeee! Dume zimaaa unachambwa hazarani si bure utakuwa SI RIZIKI!!!!!!!!!!!!!! Na KUCHAMBANANA MIMI UWE NA JF SENIOR EXPERT MEMBER atiiiiiiii au walau umelipia ukapewa Gold Member! New member kuwapa KICK humu iliishia mwaka jana! Mwaka huu watafuta kick! NAWATIA KWENYE DUSTBIN MAZIMAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!! Hio inaitwa .............. NAWAPOTEZEAAAAAA!!!!!!!!!


BACK TO TOPIC
Mwaka jana kati kati bibi dada mmoja, alijibinafsishia na kumtaifisha mume wa mwenzie mchana kweupeeeee!!!! Si kuwa Mume wa mtu waloana, la hasha! Walizaa tu watoto 3 pamoja. Bi dada yuko vizui kumpata yule bwana, akamtolea mahari fasta fasta akafunga nae ndoa lutheran! Makubwaaaaaaaaaa! Wote wachaga wenzangu!

Harusi ilikuwa crash program, hela uliyonayo ndo unatoa maana ilikuwa short notice! Mhhhhhhhhh! Ukistaajabu ya Musa utashangaa ya firauni!!!!!!! Ilileta mkanganyiko, watu wazima kwenda kumsuta na kumchambaa asifanye hilo jaribio la kupindua serikali kuu, mwenzie na watoto wa 3 ataenda wapi goal keeper yule. (Dont get the impression im mocking her because im not) ila ndo hivo tenaaa mtu mzima hatishiwi nyau! Mumeo nimemchukua, wacha nijishebedue mke mwenzangu unijue! We maliza kuku kwa mganga Mumeo mie ndo ninae ndani! IT WAS SAD! Ndumila kuwili hatukukosekana huku tunasema alivofanya shost vibaya kweliii! Huku tunpokea malace wig ya kusimamia na satin za Dubai! Njaa mbaya sanaaa! Na ushoga mjini ni full time job. Japo dhambi ilitubidi kutoa pongezi!

Tukirudi nyuma Bidada alikuwa anafanya kazi na hilo Gumegume, na alikuwa anamjua fika my wife wake maana alikuwa anakuja ofisini kwao, sasa sijui ni yeye ama karogwa ila yaliyomo yalikuwamo.! Huwezi jua maybethe guy had a SITUATION! ambayo si wa nje kuhukumu rahisi, ila nionavyo mie kumuacha mkeo na watoto wa 3 ukaoe mdada mwengine hata hujazaa nae, na usiku unakoroma peacefully si jambo rahisi!!!!!!!!!! We may never find out the truth but it was UNFAIR kwa yule bibie alieachwa! Na hakuachwa nusu, mazimaaa, na watoto kawapeleka kijijini. Bi dada yupo anapika mama lishe mjini hapa! CHOZI LA MNYONGE LALIPWA KWA MUNGU BABA! Japo la samaki lamezwa na bahari. Mungu AMKIRIMIE afungue Hoteli 5 star na apate ampendae, alisamehe na kulsahau gumegume hili. Dua zangu zifike moja kwa moja.

Huku harusi ikafungwa ya kukata na shoka, msizanie coz nimesema short notice mkajua ilichinaaa,weeee! Dhubutu yenu! It turne out ndumila kuwili tulikuwa wengi mno! Fahari ya ndoa mwisho wake honey moon. Sijui laana ama bibi alienda kuroga, yue bwana si akaachishwa kazi!!!!!!!!!? Ashinda kwenye TV! Mhhhhhhhh! N a baada ya ndoa alihamia kwa bi dada eeeeh! Ndo kushinda kwenye DSTV ya bi dada 24/7 hata kama kazi imekuwa bahati mbaya kahangaike basi mwana baba hata ukikosa umejituma sio kulikomoa sofa na Telemundo my heart beats for lola na Delmonte Dynasty. Ndo hivo hatoki wala hajitumi. Bi dada kamvumilia Nusu MWAKA!!!!!!!! Khaaaaaaa! Umlishe, umvishe mtu mzima, pocket money umjue wewe, kodi uzijue wewe, wanae kijijini uwajue wewe Inahuuuuuuuuu????????? Aku babu sitaki mizigo mie! (Ni mie lakini si yeye jamani!)

Ndo hivo hali iko hivo, ukichukulia kiwepesi waweza hisi katiwa zongo na mkewe wazamani aishi tu humo ndani ka mjusi asitikisike! Mbona MAJARIBU! Hataki wazae, haelewekiiiiiiiiii! Shosti kachokaaa! Kakubali AMEBUGI MEEEN! Tukamwambia ng'ang'ania hapo hapo UTUKOME SIE tunaoshika bango hutodumu kwenye hio ndo! Ukibwaga manyanga tunafanya party! We komaa nayo hivo hivoo. Kama huna inspiration ya kuendelea fom the inside, hata hii hatred rom the outside ikuinspre ubakie ndoani manake sahvi YOU ARE DISPEAKABLE kwa ulikwisha tenda ukimtema huyo bwana takuwa DISGUSTING!!!!!!! Usjaribu!

Ndoa umeitaka kwa chati haya hiyo hapo! Ayayaaaa umeolewa utarudi nyumbani kutembea sasa ndo utulize kalio kwa mmeo katika shida na raha! Kakondaje kwa stress? Hana hamu saa 11 ifike arudi kwa Habby! Hahahaaaaaa! Halooooo! Ndoa hiz!!!!!!! Mara aambiwe yeye ndo anamletea huyo bwana Gundu! Tangu kamuoa mmbo hayaendi!!!!!!!! Makubwaaaaaaa!!!!!!!!! Mume fahari na wa maana muone kwa MWENZIO!!!!!!!!!! Akipita kang'aaa , katokelezeaaaaa jasho la mkewe lile, Ukimkuta bar akakuhonga mchemsho utamuona wa maana kumbe husle za mkewe familia isonge, yeye kama yeye bila mkewe MAJANGAAAA! Wake za watu wakikusimulia walivoanza na waume zao na SHUKA 2! Utachokaaa! ukijitia mpana kama pazia la cinema ndo kama hivi yaliyomkuta bi dada.!!!!!!!

Ndo maana nasisitiza KUDOKOA ndo ujanja KUKWANGUA UKOKO NI KUMBEEP MPISH!!!!!!

HERI YA MWAKA MPYAAAAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
huu waraka wa leo kiboko...lakin asante nimejifunza vingi sana kupitia huu ujumbe.kwanza uvumilivu kutoka kwa bi mdada aliye achwa na kukubali kushindwa huku akimuachia mungu.
pili nimeamini malipo ni hapahapa duniani mbinguni mahesabu.
tatu mwanamke kujishughulisha kwa chochote kile sio kukaa nyumbani kusubiri kuletewa.
HERI YA MWAKA MPYA NA KWAKO PIA MKUU...
 
Dah bibie Lara1 ndo napoamin yale maneno ya mjin kuwa unaeza ukawa na mwanaume au mwanamke ambaye nyota yake ipo poa yaan kila unachokifanya ukiwa naye mambo yanakunyookea!na pia waweza ambulia mwanaume au mwanamke ambaye anaweza akawa gundu kwenye mahusiano yenu yaan kila siku ww unakua unapata mikos kama huyu bidada na mumewe. Khaa ful majangaa
 
khaaaaaaaaaaaaaaaaaa, we mtoto ni balaa, ama kweli hii ni 2014, huu memo ndo mara ya kwanza mimi kuusikia! Heri ya mwaka mpya na wewe ila upunguze makali!!!
Ndo maana nasisitiza KUDOKOA ndo ujanja KUKWANGUA UKOKO NI KUMBEEP MPISHI!!!!!!
 
Heri ya mwaka Mpya na kwako pia,Pole na Ban tusha kumbuga swagga zako aise
 
Kwel lara 1 ayo mambo ya nyota kumatch yapo sanaa...kwapua mme wa mtu ujionee kama hujaumbuka...teh ao inzi uliofukuza kwan kuna vidonda humu?????
 
weraaaaa wacha movie iendelee skelewu na ngololo ndo habari ya mjini kati!
bidada alidhani ndoa kupambwa na maznat eee wizi mbaya..onja usogeze hatua...
Happy New Year
 
Unajisikiaje kwenda kumuingilia mwanamke mwenzio lol ona sasa anavoumbuka. Malipo ni hapahapa duniani
 
hiyo ndiyo laana ya kutumia libwata. libwata linaua ubongo wa mwanaume na kuwa kama zezeta , kazi hawezi , maisha hawezi yeye nikula kulala. ndiyo maana alishidwa hatakujua umhimu wa mke mwenye watoto watatu na kumwacha , akaoa mwanamke aliympa libwata na mwisho hata kazi ikamshinda.
 
Yan nlivoona tu heading ya thread nkajua Lara1,welcome back,happy new year!!!
mhhh,pole yake uyo dada mana daah,..kaanza vibaya ajee
 
Aisee! Ndo atulie huyo bidada si alitaka ndoa? Wacha amuhudumie si mumewe wa ndoa?!! lakini zote hizo ni dhambi tu! Umuache mkeo na kids wanahangaika kweli ?
 
me study imenibana mnoooooooo naingia mara moja moja hivi ulipigwa ban kwa sababu ganiiiii anyway heri ya mwaka mpyaaaaaa na itabidi msemo wa igweeeee unirithishe bie bidada

back to the topic

huyo bidada alidhani laaana yatoka kwa wazazi tu eeeeeeh ndo ajue sasa laana ya mkee ni mbaya mnoooo na akimkimbia huyo mume dunia itamzogoajeeeeee si alitamka mwenywe kwa shida na rahaaaaa ndo shida zenyewe hizo ingawa zimewahi kupiga hodi ajifunge kibwebwe kutunza na watoto wa mume pia wakati anavaaaa shela si alijua kuwa bwana ana watoto watatu kashapenda boga na maua yanamhusu
 
Mhhhh! Happy new year pia, bt una mambo wewe, nikadhani mzaramo kumbe mchaga pure! missd u tho!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
...Telemundo my heart beats for lola na Delmonte Dynasty...

Ndo maana nasisitiza KUDOKOA ndo ujanja KUKWANGUA UKOKO NI KUMBEEP MPISH!!!!!!

HERI YA MWAKA MPYAAAAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Heri ya mwaka mpya na kwako!
 
KUDOKOA ndo ujanja KUKWANGUA UKOKO NI KUMBEEP MPISH!!!!!!.......kwi kwi kwi kwi.......yeleeewiiii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom