Wa kwanza akiwa kidume nitafurahi zaidi ingawa yeyote nitashukuru Mungu tu! Wengi tunafikra kuwa mtoto wa kiume ataendeleza jina la ukoo(la kwangu) maana mwanamke anapoolewa hupoteza jina la kwao na kuchukua la ukweni. Mimi binafsi sijui ni kwasababu gani hasa lakini i think i will be proud to introduce kidume kama firstborn wangu mbele ya ndugu na jamaa zangu.
Lakini kuna tabia nyingine pia nimeiona kuwa mtoto wa kike kwenye familia huwa anakuwa rafiki zaidi wa baba na wakiume rafiki zaidi wa mama sijui hili pia mnalizungumziaje wadau?