Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,258
- 20,709
Poleni wanajamvi,leo nimekuja na mjadala hapa wa mzazi wa kiume kutopenda uzao wake wa kwanza uwe wa Kike na hii kasumba ipo kwa wanaume weng sana ukubali ukatae jibu ni ndio,hata pindi mke anapokua mjamzito mwanaume ataanza utabiri wa mtoto wa kiume tena na kumpa jina kabisa na si wa kike.
Sasa mimi najiulizaga kwanini mtoto wa kiume anapewa nafasi kubwa sana kuliko wa Kike?
Kama wewe ungependa mtoto wako wa kike awe ndo first born?
Hebu tujadili tubadilishe hii kasumba.
Kwangu mimi majibu yote A,B,C ni sawa tu
Apate mtoto sawa
Apate wa kike sawa
Wa kiume sawa
Asipoza sawa
Hivi kwani umeoa ili iweje?