Poleni wanajamvi,leo nimekuja na mjadala hapa wa mzazi wa kiume kutopenda uzao wake wa kwanza uwe wa Kike na hii kasumba ipo kwa wanaume weng sana ukubali ukatae jibu ni ndio,hata pindi mke anapokua mjamzito mwanaume ataanza utabiri wa mtoto wa kiume tena na kumpa jina kabisa na si wa kike.
Sasa mimi najiulizaga kwanini mtoto wa kiume anapewa nafasi kubwa sana kuliko wa Kike?
Kama wewe ungependa mtoto wako wa kike awe ndo first born?
Hebu tujadili tubadilishe hii kasumba.
weye hutaki kuwazalia wanaume wenzie wajao wake kama wewe walivyokuzalia mke? usiwe na ubaguzi huo mkuu, halafu mungu watu kama wewe wabaguzi ndio anawaleteaga wale wale usiowataka
mfumo unamafanya mwanamme kupenda uzao wake wa kwanza uwe wa kiume kwa kuwa hamna utamaduni wa mtoto wa kike kuridhi
Sio wanaume wote wenye iyo akili. Wengi siku hizi wameshaelewa kuwa wao ndio wana uwezo Wa kufanya Mtoto awe Wa kike au kiume. Tena wengi ninaowafahamu wanawafurahia sana watoto wa kike
haya bana mungu akupe sawasawa na hitaji lako.Eee! Unaniombea mabaya DEMBA eee?
...
Jaman! Mi thio mbagudhi! Nimesema tu itakua bonge la dissaptment! Thi unajua tena ukitegemea kitu afu ukikose!
...
Thina maana ya kuwakataa or kuwachukia Mtoto wa kike and/or mama watoto!
...
but nikiambiwa nichague.......!
Hakuna ukweli wowote ila wazazi tunapenda kuwa na watoto wa jinsia mchanganyikoPoleni wanajamvi,leo nimekuja na mjadala hapa wa mzazi wa kiume kutopenda uzao wake wa kwanza uwe wa Kike na hii kasumba ipo kwa wanaume weng sana ukubali ukatae jibu ni ndio,hata pindi mke anapokua mjamzito mwanaume ataanza utabiri wa mtoto wa kiume tena na kumpa jina kabisa na si wa kike.
Sasa mimi najiulizaga kwanini mtoto wa kiume anapewa nafasi kubwa sana kuliko wa Kike?
Kama wewe ungependa mtoto wako wa kike awe ndo first born?
Hebu tujadili tubadilishe hii kasumba.
Kwangu mimi majibu yote A,B,C ni sawa tu
Apate mtoto sawa
Apate wa kike sawa
Wa kiume sawa
Asipoza sawa
Hivi kwani umeoa ili iweje?
ndoa ya kweli / pete ya heshima ni mtoto;
mtoto wa kiume ni wa hapo hapo daima lakini wa kike ni wa kwenda kwa mume wake tu.
mtoto wa kwanza akiwa wa kiume ana percent ya kuokoa jahazi,then wakifuata wa kike poa tu!!
Mie napenda sana mtoto wa jinsia aliyopendezwa nayo muumba mwenyewe. Na wote nitawapa haki sawa kuanzia elimu na upendo kama baba.... hayo ya me au ke ni yupi bora ni kutokuonyesha heshima kwa mungu muumba na laweza leta laana.
mtoto wa kwanza akiwa wa kiume ana percent ya kuokoa jahazi,then wakifuata wa kike poa tu!!
kweli elimu kwa hawa wanaume inahitajika,hawajui tu kwamba wao ndio chanzo cha mtoto kuzaliwa ke au me!!!!!