Habari wanajamvi,
Kuna rafiki yangu anafanya kazi Iringa na mumewe anafanya kazi Dar. Wana mtoto mmoja.
Toka walipooana (miaka mitatu iliyopita) hawajawahi kuishi pamoja maana mdada alipata kazi one week before marriage, so ikabidi akaripoti kazini na kumuacha mumewe Dar.
Sasa anasema anataka kuacha kazi ili akaishi na mumewe kwani anadai kachoka maisha ya usingle na kulea mwana peke yake.
Je ni sawa kwa maisha ya sasa kuacha kazi? Je, ndoa na familia si muhimu pia? Ameshajaribu kutafuta kazi Dar lakini hajafanikiwa.
Nimemwambia sometimes money is not everything. Wanajamvi mwasemaje maana dunia ya leo wengi wamejikuta wanaishi mbali na wenza wao kwa sababu mbalimbali hasa kazi.
Je, hii arrangement ni health kwa ndoa na familia kwa ujumla ukizingatia vishawishi vya sasa?
Toeni experiences na ushauri wenu.
Asante.