Mume na kuhudumia familia

Mume na kuhudumia familia

Hold other factors constant, jukumu la kuhudumia familia ni la mwanaume na endapo ataachiwa mwanamke basi ndoa hiyo haiwezi kuwa na afya
 
Miaka 16 ina-qualify kweli kwenye ndoa zilizodumu? Sidhani. Kama ni futbol, hata kipindi cha kwanza hakijaisha.

Anyway, as a man, there's only one formula to getting along with us; DO NOT HURT A MAN'S PRIDE. And since we ain't all cut from the same piece of cloth, we don't share the same pride. So some may find theirs in providing, others may not. Just study the brotha
Sikuwezi!! miaka 16 si kudumu? Hata ndoa za miaka 5 wanazishirikisha kwenye hizo makala. Ndoa zinavunjika kabla ya anniversary ya pili. Kipindi tulicho nacho mkifikisha miaka 16 ni mafanikio makubwa.
 
1. Kama kweli, mume ana kipato kizuri tu cha kuwezesha, akimruhusu mke wake awe ndiye mlishi wa nyumbani, huyo mwanamume nasema; Anatatizo kuubwa. Aliyetuumba tangu mwanzo alitutaka, Mwanamume atoke jasho ili mkewe ale. Itakuwa ni aibu iso kifani mke wangu anipakulie wali nyama na mchuzi mzito, halafu nikae mezani na watoto wangu tule tujilambe mikono. Najiuliza swali, nitamwambia aksante mama kwa chakula au nitatoka ka hotelini??
Hiyo nyama najua kafanyaje mpaka akainunua?? Nasema; Haikuji... Haiingii akilini. Mtoto asiposema aksante mama kwa chakula, ki kwetu anastahili vibao vya kumtosha. Sasa, miye ntalambwa fimbo au?? Haijiiiii.
2. Ukweli ni kwamba, hata ukifika pale buchani kununua nyama ya kupeleka home, wale wamama waliokaa pale hukuheshimu. Muuza bucha naye hukuita; Mzee nanihii nikate kilo ngapi. Hizo zote hukufanya ujisikie. Sasa, nikifika home, nkakuta nyama choma imeandaliwa kwa week end, nami sikuinunua, ntakulaje? Mama hastahili.
3. Mke kuwa na kipato chake, nitamkalisha chini, na kumsomesha hadi aujue wajibu wake. Kwa kuwa anataka kufanya kazi ofisini kwa sababu ya kisomo chake, sio vibaya. Lakini, akumbuke kuwa siku alipoondoka kwao, akaja kukaa kwangu, hata jina alibadilisha. Huyu ndiye mtoto wangu wa kwanza. Akaitwa binti MIMI yaani Mrs. MIMI. Kama mtoto wangu wa kwanza, jukumu lake ni kunitii, kuniheshimu. Ili jina langu limpendeze, kamshahara kake, akalete mezani tukapangie tufanye maendeleo. Najua wengi mtanipinga, lakini, kumbukeni kuwa kwenye mirathi anataka awe ndiye msimamizi wa mali (zangu) na wakati huo anadai tulichuma naye. Kama mshahara wake anautumbulia porini kusiko julikana, itakuwa ni dhambi kuthubutu kusema ati tulichuma naye. UAMINIFU ndio msingi wa haya yote. Mzee ukiisha ficha kipato na kuanzisha vijumba vijumba huko na huko, na beeer kwa wingi kwenye mabaa, hustahili hata kumuuliza anapata ngapi.
asante kwa mchango wako ila siamini huo umri wa ndoa 40+ na idadi ya watoto na wa mwisho yuko chuo kikuu! kama kweli basi hongera sana na Mungu aendelee kuwaimarisha.
 
asante kwa mchango wako ila siamini huo umri wa ndoa 40+ na idadi ya watoto na wa mwisho yuko chuo kikuu! kama kweli basi hongera sana na Mungu aendelee kuwaimarisha.

NANDERA;
Utomaso umetoka wapi?? Umesikia nagombea cheo humu JF useme najitutumua kisiasa?? Wanasiasa ndo hudanganya watu; Oh! Mkinichagua ntawajengea gorofa etc etc.
Hunijui, sikujui, sina haja ya kukudanganya miye. Yaani kwako ni sifa kujigamba kuwa ulishafiwa na watoto3?? Ama kweli, tomaso wako wengi.
 
Kw
Sis yani Sijaelewa ilkuwaje mama ndo akawa mhudumiaji mkuu. Mme yupo stable tu kiuchumi na mwanamke akaamua kusimamia show nzima ya familia au mke amemmzidi kipato mume au ilkuwaje?

Sijaolewa yet, ila kwa jinsi navyofahamu, ili ndoa yenu iende kwa amani na heshima iwepo zaidi, mwanaume inabidi awe ndo the ultimate breadwinner na ahakikishe yeye ndo msimamizi mkuu na mhudumiaji mkuu wa familia. Mke abaki kuwa ni msaidizi kumpiga tafu mumewe hapa na pale. but kwenye cases kama mume hana kazi, yupo masomoni, anaumwa etc, mke hana budi kuwa ndo mtafutaji mkuu wa familia , ila itakuwa ni busara mwanaume ndo akisimamia mambo ya finance asimuachie mkewe ndo aongoze hii financial area. (Tusiongelee wale wanaume wenye uwezo lakini hawahudumii familia zao, wao hela zao zinaweka heshima kwenye vitu virefu na kwa michepuko).

Kwa Waafrika, kikawaida ilikuwa mke unaolewa kwa ajili ya kuangalia familia na kulea watoto. Mke kufanya kazi nafikiri ilitakiwa iwe ni "interest" ya mke tu, sio kwa sababu ya kuchangia majukumu ya kifamilia. Tatizo kubwa linalotusumbua hapa ni "Utegemezi". Wakaka wengi wanaoa bado wakiwa hawajafikia kilele cha mafanikio yao, bado wanakuwa na uwezo wa kawaida tu kiuchumi. Issue inaanza pale ambapo mtu anaoa, but still majukumu ya familia yake na wazazi na ndugu kadhaa, yanamwangalia mtu huyu huyu mmoja. Huyu mtu aprovide kwa ajili ya familia yake (malazi, mavazi, chakula), alipe ada, mwanafamilia hajaugua, bado hajatuma hela kwa wazazi wake, kuna mtoto wa dada anahitaji msaada wake, bado kuna wakwe nao awakumbuke mmh . For sure inabaki kuwa ni mzigo kwa huyu mtu mmoja, na yakimzidi hatutochelewa kusikia amedondoka ghafla kwa presha. So mke pamoja na majukumu yote ya kifamilia, anajikuta na yeye anahitajika kuchangia baadhi ya majukumu ( na sio kuwa mhudumiaji mkuu wa familia), let A man be the man

Ila ikitokea mtu kaolewa na Reginald Mengi type, jeshi la mtu mmoja linajiweza, basi mke atafanya kazi kwa ajili ya interest zake tu binafsi. Inaleta raha na ni heshima kubwa sana mwanaume kuhudumia familia yake. Unless kuja special cases ambazo ni nje ya uwezo wenu, basi please hudumieni tu familia zenu
Kwenyemiti hakuna wajenzi, umemaliza dada
 
Wanawake wamekuwa shida sana siku hizi. Unakuta mtu yupo hapa JF anaponda kweli role ya mumewe ila kwakwe kainstall mahouse girl wawili wawili na house boy juu. Asilimia zaidi ya 70 ya wanawake wa siku hizi hawajui role yao kama wake lakini wanavyonyoosha midomo hapa kwenye role ya waume wao.
Hiyo comment yako hakuna atakayeiona!!
 
NANDERA;
Utomaso umetoka wapi?? Umesikia nagombea cheo humu JF useme najitutumua kisiasa?? Wanasiasa ndo hudanganya watu; Oh! Mkinichagua ntawajengea gorofa etc etc.
Hunijui, sikujui, sina haja ya kukudanganya miye. Yaani kwako ni sifa kujigamba kuwa ulishafiwa na watoto3?? Ama kweli, tomaso wako wengi.
mmh.... labda nina usingizi. hata sielewi. kwangu ni sifa kujigamba kama nilishafiwa na watoto?? watoto gani?
NANDERA;
Utomaso umetoka wapi?? Umesikia nagombea cheo humu JF useme najitutumua kisiasa?? Wanasiasa ndo hudanganya watu; Oh! Mkinichagua ntawajengea gorofa etc etc.
 
i swear ninanunua na ninaendelea kununua glass, sahani na vikombe tu.. vingine havinihusu yaani hata asipoacha pesa ya kutosha nazi, wali nazi ataula kwa mama ntilie tu.
wacha mwanaume aumie ajue maana ya uanaume wake.
Haleluyaaaaaaa!![emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106]
 
kuna hii habari ya maisha ya sasa ni kusaidiana'; inatumiwa vibaya mno na wanaume na ndiyo mwanzo wa shida nyingi za mahusiano
Tena shida kubwa, mwanaume lazima abaki kuwa mwanaume, akishindwa basi afanye tu maamuzi magumu kama ya akina nanihiii.
 
si ndo tunatafuta suluhisho? pengine wanawake wakikaa nyumbani mambo yataenda vizuri. Au wakishapata mishahara wawape waume zao?
DDC Mlimani Park walikuwa na wimbo mmoja una mashairi yanasema...

"Usitumie peesa, kqma fimbo baba, mambo ya pesa yataka makubaliano, hapo ndipo pesa huwa na thamani".

Kuna wengine ukiwapa pesa ndo kwanza wanakudharau kwamba huna usanii.

Ni mambo ya makubaliano tu.

Ndiyo maana ushauri wa jumla jumla hauna maana kama wenyewe hawaukubali.
 
Back
Top Bottom