NANDERA
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 2,024
- 2,488
Habari za wikiendi wanaJF,
Leo katika mapumziko yangu nilikuwa nasoma jarida la kila mwezi la Parents. Katika jarida hili huwa kuna makala inayoitwa "Marriages That Last" ambapo huwahoji wanandoa waliodumu kwenye ndoa zao, nia ikiwa ni kuwajenga wengine kwa ku-share changamoto na mafanikio.
Makala ya mwezi huu inahusu ndoa ya baba na mama mchungaji, wako katika miaka yao ya 40, wana watoto wawili wa miaka 12 na 10, na ndoa yao imedumu miaka 16. Wameongea mengi ila leo nitazungumzia moja.
Wanandoa hawa wanasema ndoa yao iliishi kwa kupumulia mashine kwa miaka 9 bila wao kujua mpaka walipohudhuria mafunzo ya ndoa yanayoitwa Ndoa -programu inayoendeshwa na kanisa fulani huko Kenya. Mojawapo ya jambo alijifunza mke ni kuwa katika kipindi hicho cha miaka 9 bila kujua, alikuwa akimnyima mumewe fursa ya kuhudumia familia. Anasema mke "it was only after Ndoa that I realised I was infringing on some of my husband's roles. For instance, I was keen to provide for the family and always made sure there was food in the house. I didn't realise how important it was to let my husband play his role and shine too".
Niliposoma hapa mawazo yangu yakahama. Nikakumbuka ndoa za wazee nilizowahi kuona na ndoa za jamaa na rafiki zangu za sasa. Wanawake hawa ninaowafahamu wengi wako kwenye hili kundi jipya japo la zamani la "married single moms". Hapa nazungumzia wale wanawake wenye waume wenye vipato lakini waume hao hawahudumii familia - hawalipi kodi za nyumba au kugharamia ujenzi, hawanunui chakula, hawalipi ada n.k.
Sasa tukichukua mfano wa huyu mama mchungaji, ina maana kuna wanaume wenye vipato lakini hawahudumii familia kwa sababu wake zao wamejibebesha bila shuruti jukumu hilo na kumbe linawaumiza waume na wake kila mmoja kwa jinsi yake na kuweka ndoa rehani. Sasa maswali yangu ni haya:
1. Hili swala la wanawake kuingilia majukumu ya waume zao lina mchango kiasi gani katika familia zinazohudumiwa na wake hapa Tanzania ilihali waume zao wana vipato?
2. Kama wanaume hujisikia mashujaa/vizuri kwa kuhudumia familia, na kama hizi ni hisia za asili, hawa wanaume wanaonyang'anywa hizi hisia na wake zao huzifidia vipi?
3. Ni mara nyingi tumeona hapa jf wanandoa wa kiume wakilalamika kuwa wake zao wana vipato lakini hawachangii katika kuhudumia familia. Hili nalo liwekwe vizuri.