Mume kumfuata Mke!!!!!!!!!

Nashukuru WANAJAMVI kwa maoni yenu nadhani VIGEZO NA MASHARTI vitazingatiwa!!sasa nitaenda kwa nguvu kwa mkurugenzi anipe uhamisho niufuate usingizi wangu
WAKATABAU
 
fata utamu wako Kaka.......wengine humu hawajaoa tabu tupu hawajui unachopata ..wala unachotarajia
 
Wewe kibaraka wa wazungu. Haki sawa ni kwa watu wasio wastaarabu. Mwanamke anatolewa mahali. Acha ujinga wa kizungu.

Mkuu acha mambo ya kufuata mke, utakuwa mtumwa, wanamatatizo hawa usiwaone2 hivi.

Fanya Kiume acha mambo ya haki sawa yatakupoteza kuwa na msimamo. Ikiwa vipi basi vipi, unamtema wanawake wapo wengi tu tena wenye heshima. Asikuzingue

wewe mwenyewe ni kibaraka wa wazungu kwa kuangalia jina lako tu! Na tutaendelea kuwa vibaraka wa wazungu kama unapenda sana uafrika then go back to ur root hata nguo usivae uvae ngozi na katambuga! Nonsense unaongea tu kwa kuwa huna binti ukiwa unabint hutaongea hivyo!
 
Waswahili bwana! Unaulizwa taratibu na haki za kuhamishwa unajibu habari za mfumo dume! Mfumo dume doesn't work all the time!
Hivi mfano umeoa mwanamke ana kazi inayolipa zaidi ya ya kwako, mnasaidiana maendeleo! Unaweza kweli kumtaka a-sacrifice kazi yake?
Mtoa mada, kila la kheri. Omba uhamisho ufuate mkeo ndugu yangu, wewe mwenyewe ndo unajua uhondo wa ngoma yako. Siku zote mashabiki hujifanya wanajua mpira kuliko wachezaji na kocha wao!
 
MKUU KUNA WENGINE WAMEKWAMBIA MKE AACHE KAZI AKUFUATE ETC ETC!
UKIWAFUATISHA SHAURI YAKO UTAINGIA CHAKA!!

NDOA NI WATU WAWILI, UMESHASEMA UPO HALMASHAURI, HIVYO NI RAHISI KWAKO KUHAMA, ANDIKA BARUA KUOMBA UHAMISHO ELEZA SABABU ZA KUHAMAAMBATANISHA NA CHETI CHA NDOA FUATILIA!!

Mambo ya kwamba wewe ndo mume, mke akufuate blablabla achana nazo, wewe ndo unajua shida mnazokabili kwenye ndoa yako, wewe ndo unajua maisha yako na mkeo ikoje, wewe ndo unajua umuhimu wa ajira ya kila mmoja kwenye ndoa yenu, na ulishatafakari na kuona ni vyema uhame, fanya hivyo hama.

Kuna wengine watashauri mke aache kazi, mipango ya maisha yenu yakiharibika kwa kupungua kipato, au frustration za hapa na pale ni ndoa yako ndio itakayokua na mashakani,
 
hizi ushauri ndugu yangu inabidi kuzichambua sana maana wengine wanachowaza ni mfumo
dume tu, wanasahau ndoa ni wawili wao ndo wanapanga mipango yao, wao ndo wanajua nini wanataka, wenyewe washaona kwa kazi ya mke hawezi hama ila mume anaweza kuhama, badala ya kumpa utaratibu wa kuhama wanashauri mke aache kazi, then what? Wanadhani wenyewe option ya kuacha kazi hawakuiona wala haakuijadili?


Waswahili bwana! Unaulizwa taratibu na haki za kuhamishwa unajibu habari za mfumo dume! Mfumo dume doesn't work all the time!
Hivi mfano umeoa mwanamke ana kazi inayolipa zaidi ya ya kwako, mnasaidiana maendeleo! Unaweza kweli kumtaka a-sacrifice kazi yake?
Mtoa mada, kila la kheri. Omba uhamisho ufuate mkeo ndugu yangu, wewe mwenyewe ndo unajua uhondo wa ngoma yako. Siku zote mashabiki hujifanya wanajua mpira kuliko wachezaji na kocha wao!
 
Kama kazi ya mke ni ya maana zaidi katika jamii kuliko ya mme inakuwa rahisi kuhamishwa mme, mfano mke ni daktari bingwa ilhali mme ni mwalimu wa sekondari. Kaka andika barua ukielezea sababu zako. Tchao!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom