masatujr1985
JF-Expert Member
- Oct 27, 2011
- 1,980
- 788
Wengine wanafanya hivyo ili watoto wao wazoee kuwaita baba zao daddy coz wanackia vile mama zao wanavyowaita. Usikomae sana na sweetie ukashangaa siku mtoto anamuita baba sweetie. Ama 'we fulani!' then mtoto naye anamuita 'we fulani(jina la mume)'
Linahitaji utafiti. Katika kujifunza lugha hasa Kwa watoto wa chini ya miaka 2 Ni dhahiri wanahitaji kutambua watu wa karibu Kwa utambulisho wanaousikia toka Kwa wanafamilia. Hili la kumuita mmeo:baba/ mkeo:mama sina uhakika kama Ni Kwa ajili hiyo maana mtoto Anahitaji tu kusaidiwa katika kujifunza maneno na hasa majina. Mfano: kumtambulisha baba kama baba, na kumwambia baba anakuja/baba yule (mfano tu) mtoto hujenga picha ya baba kirahisi na kujenga tabia na uelewa kuhusu baba. Vivyo hivyo Kwa mama. Nadhani hii Ni katika tu kufanya mapenzi yawe kisasa zaidi na kuweka vikolombwezo. Na hasa hasa Kwa wanawake wa mjini (kama ishara ya mapenzi).
Swali la kujiuliza, kule vijijini ama Kwa wazee wetu mbona hatukukua tunasikia mama anamuita mme wake baba, ama baba anamuita mke wake mama lakini tulitambua huyu Ni baba na huyu Ni mama?
Wenye kutaka kutetea hili katika mlengo wa lugha basi wasome mawazo ya mtu anaitwa Nom Chomsky.
Hili liko kimahaba zaidi.