Blue G
JF-Expert Member
- Jun 20, 2012
- 5,339
- 3,670
Kulipiza kisasi sio maisha yanayotakiwa kati ya wanandoa,kwa sababu ukiamua kulipa kisasi utaiharibu ndoa yako mwenyewe na utakuwa unaitafuta aibu yako mwenyewe kwa sababu mara nyingi mwanamke aliyeolewa akiwa kicheche inakuwa gumzo mtaani na aibu kubwa kwani kila kona utaongelewa wewe tu,tofauti na wanaume ambao wao hata wawe wahuni kiasi gani huonekana kama ni kawaida sana.Cha kufanya jaribu kuwahusisha watu walio na miaka mingi kwenye ndoa,washenga wenu wa ndoa au hata wazazi na uwaeleze wasiwasi ulionao juu ya huyo mmeo waangalie watawasaidiaje,baada ya hapo ukiona tabia haibadiliki na ukijua chanzo ni nyumba ndogo unaweza kuachana naye kama waweza, kuokoa watoto wenu kwani siku hizi magonjwa ni mengi,na pi hata mwanzilishi wa ndoa yaani Mungu katk maandiko yake ameruhusu ndoa kuisha ikiwa mmoja si mwaminifu.