Mume avaa nguo za Kike kwenda kufumania

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,298
33,083
SOO.jpg




Na Gladness Mallya
Mwanaume mmoja Adam Hashim (24) mkazi wa Mbezi Makonde jijini Dar es Salaam, amejikuta matatani kufuatia kutinga nguo za Bibie kwa lengo la kwenda kumfumania mkewe (hakujulikana jina).

Tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika Kituo cha Daladala cha Mbezi Shule, Dar ambapo mwanaume huyo alivaa khanga, hijabu huku usoni akiwa amejifunga kininja kwa lengo la kufuatilia nyendo za mkewe ili akamfumanie.

Hata hivyo, mume huyo ambaye ni dereva wa bodaboda maeneo hayo, hakufanikiwa kumtia mtegoni mkewe kwani kabla hajapanda gari kwenda kwenye tukio, mtu mmoja alimtilia shaka kwa kumsalimia lakini hakuitika hivyo ‘msamaria mwema’ huyo akawaita askari waliokuwa doria na kumkamata.

Safari ya fumanizi iliishia hapo, mwanaume huyo alipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Wazo Hill, kilichopo Tegeta, Dar.

Akisimulia mkasa huo kwa maafande kituoni hapo, Adam alisema kwamba, aliamua kufanya hivyo kutokana na wivu kwani kila alipotoka kazini alikuwa na tabia ya kumsikiliza mkewe dirishani ili kujua anazungumza na nani kwenye simu.
Akasema kuwa, siku ya kwanza alimsikia akiomba vocha ya shilingi 500, naye akaikuta hiyo namba kwenye simu ya mkewe akaikariri.

Siku iliyofuata, Adam anasema alisimama tena dirishani, akamsikia mkewe akimwambia huyo jamaa wataonana kesho yake ili wamalizane na kwamba atamdanganya mumewe kwamba anakwenda kutafuta kazi.

“Baada ya kusikia hivyo niliingia ndani, lakini sikumuuliza kitu, kesho yake kweli akaniaga anakwenda kutafuta kazi,” alisema Adam.

Akasema alimruhusu mkewe kisha yeye akaenda kuazima nguo (hijabu na khanga) kwa shemeji yake na kuzitinga na kwenda kujibanza mahali.

Adam anasema mkewe alipotoka, alimfuatilia kwa nyuma mpaka kwenye kituo cha daladala ambapo alipanda gari na yeye alipotaka kupanda ndipo alishtukiwa hivyo fumanizi lake likadunda kwani mkewe aliondoka yeye akakamatwa na polisi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema watakwenda kumfanyia uchunguzi wa akili Adam ili kujua kama ipo sawa kwani wengi wanaofanya hivyo akili zao zinakuwa na matatizo. :clap2::tea::first:





227183_165222686870827_100001492890808_404453_720403_n.jpg
 
duh! hiyo kali ya mwaka, inaelekea alikuwa
anajishtukia yy mwenyewe ndio maana akagundulika
kirahisi.
 
kwa hiyo mkwewe alifanikisha ufirauni wake na alipo rudi jioni akakuta mumewe yupo polisi. Historia inonyesha huyo mwanamke ni cheep sana yani vocha ya miatano tu kesho yake anaenda wakamalizane?
 
hiyo kaliiii na siajabuuuu jioni akaamua kwenda kumalizia utamu wa mchanaaaaa tena hadiii moning.kweli utamuuu wa njiwa kupata ubavuu jamaa kaambulia kupunyua manyoyaaaaaaa
 
kwa hiyo mkwewe alifanikisha ufirauni wake na alipo rudi jioni akakuta mumewe yupo polisi. Historia inonyesha huyo mwanamke ni cheep sana yani vocha ya miatano tu kesho yake anaenda wakamalizane?
Zitakuwa zimetoka mia 5 nyingi tu kabla mume hajazistukia,huyu jamaa kweli akapimwe akili alitakiwa kuomba wenzake wa bodaboda mmoja amfatilie mkewe na kuletewa taarifa.
 
Back
Top Bottom