mume apewa figo na mkewe baada ya kupona anatesa na wanawake wengine

kamusi

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2012
Posts
1,079
Reaction score
753
ni kisa cha kusikitisha ,(kisa cha kweli)

Jamaa mmoja mfanya biashara alikuwa mgonjwa taabani baada ya figo zake kufeli kufanya kazi, ilibidi aende india kwa matibabu zaidi ambapo aliambiwa figo zake zina matatizo makubwa na ili kuokoa maisha yake alitakiwa apatiwe figo nyingine. Mkewe wa ndoa alijitolea figo yake moja na mumewe akawekewa hiyo figo na hali ikaimarika akarudia afya yake. Mume ambaye alikuwa mahututi alipona akaendelea na shughuli zake kama kawaida.

Muda kidogo baada ya kupona mwanaume huyu alisahau yoote mkewe aliyomfanyia na akawa hapatikani nyumbani, hajali mke wake wala watoto n.k baada ya kuchunguza mke akagundua mumewe ana mwanamke mwingine nje ya ndoa ambaye wana mahusiano ya kimapenzi na tayari huyo mwanamke ni mjamzito..

Mume alipoulizwa na mkewe hakuonyesha kujali wala kujutia kitendo chake na bado anaendelea na huyo mwanamke hajamwacha mpaka sasa..kwa kifupi jamaa ni kama kahamia kwa huyo hawara(nyumba ndogo) kwani nyumbani kwa wife anaonekana kwa machale machale(sio full time km zamani)

Mama wa watu(mke wa ndoa) yuko kama amechanganyikiwa hivi na wala haamini macho yake kilichotokea, afya ya huyo mama ameanza kudhoofu na anaumwa mara kwa mara..ghafla tu amepungua mwili na pia amepata ugonjwa wa presha ambapo alilazwa hospitali na sasa ametoka..
Huyu mama( mke) anasimulia kwa masikitiko jinsi alivyohangaika na watoto na kutafuta kipato yeye peke yake kipindi mume wake mgonjwa(aliugua muda mefu kdg) alihudumia familia na pia gharama za matibabu ambazo zilikuwa kubwa yeye ndiye aliyehangaika mpaka mumewe akapelekwa india kwa matibabu..
Kwa bahati wana biashara nzuri inayowaingiza kipato kizuri (kwa usimamizi wa huyu mama) kwani walipooana walikuwa hawana chochote.
kwa kifupi huyu mama amekata tamaa ya kuishi kwani kila mara anaongelea kufa tu, na mumewe wala hajali.. wana watoto 3..
ndugu wamemkalisha huyo mwanaume chini lakini inaonyesha kakolea kwa nyumba ndogo utafikiri karogwa vile..
 
figo ya mkewe aliyopewa na mkewe kumnusuru maisha yake ndio anamlipa kwa nyumba ndogo bila hata huruma!!
dah nitarudi baadae kidogo
 
Duh, mijamaa mingine mikauzu kweli kweli. Huyo mama asimuwaze huyo hayawa.ni maana hawakuzaliwa wote na hawatakufa wote.

Haya mabandiko mengine ya kuharibiana mudi tu, unaweza tukana bure.
 
Sio kwamba .....................'utafikiri karogwa vile'. Huyo kesharogwa kweli
Na mwanamke akigundua kuwa anaiba mume wa mtu,haibi mara moja!!! anapoteza jumla jumla kwa ndumba!11
 
figo ya mkewe aliyopewa na mkewe kumnusuru maisha yake ndio anamlipa kwa nyumba ndogo bila hata huruma!!
dah nitarudi baadae kidogo

hiyo ndio inaitwaga LAANA YA MKE sasa ndio ujue duniani kuna mambo,
 
hii inatufunza ni vema kuwa makini na watu tunaokutana nao ukubwani
 
Ningemtafuta kwa nia moja tu.....arudishe figo yangu...alaaah....
 
sh!t........ mama achukue figo yake tu, maana ianwezekana
 
ua huyo hawara tu maana kama laana kashalaaniwa sana!!!mambo mengine yanaumiza sana
 
Dume La Njiwa Hiloo.,

Hata Aibu na Huruma Halina,Hilo linajali Nyapu tuh
 
hiyo ndio inaitwaga LAANA YA MKE sasa ndio ujue duniani kuna mambo,

Hii ni mbaya mno, kuhangaika kwake ndio kanaswa sasa sijui mkewe akifa kwa presha Mungu atamwacha
Nimejifunza
 
Huyo mama kama anamwamini Mungu aombe sana sbb ndoa nyingi sana zinaingiliwa kishirikina watu wanabaki kulalamika badala yakumshirikisha Mungu. Kama huyo mama atakuwa tayari kwa msaada wakiroho mleta mada ni PM nikupe contact za mtumishi ambaye naamin atakuwa committed ktk kumwombea hadi ndoa yake ifunguliwe!
 
ndivo tulivo tu rahisi kusahau na hatuna shukrani....:..... mama akaze moyo konde afikirie kids akifa nani atalea najua ni ngumu lakini atafute njia sahihi kukabiliana na tatizo alee hao kids.
 
Duh! Hii story ni painful mwambie atulie asimuwaze huyo Mumewe eti tu kwasababu kaokoa maisha yake Atakufa kwa PRESHA mwambie afikirie maisha yake na kama Mumewe kaamua kumdharau basi amrudie mungu wake yeye ndio atamshindia kuliko kushindana na huyo mjaa Laana. Afikirie positive katika maisha yake asikubali kubaki katika Mawazo ya kufikiria huyo mwanaume assume kwamba huyo Mumewe alishakufa so SONGA mbele mama huku ukimkabidhi mungu Maisha yako . Usikubali Mumewe awe kikwazo cha furaha yako vinginevyo utakufa wewe umwache mwenzio akifaidi raha za dunia. TAMBUA KILA MTU DUNIANI ALIKUJA MWENYEWE NA ATAONDOKA MWENYEWE .
 
It is very painful mleta mada naomba um pm yule jamaa ili mama akafanyiwe Maombi kuna nguvu za giza zimetumika kw huyo Mume . Vikao havitasaidia watakaa vya familia mpaka vya kata mume hatarudi . Kwenye ulimwengu wa Roho wa Giza kuna jambo limefanyika co bure fanya haraka huyu mama anahitaji spiritual protection c vingnevyo . Mungu ampe neema ya kumshnda shetani katika majaribu haya
 
Huyo mume na nyumba ndogo yake wana kesi ya kujibu
 
....for better or worse, amstahmilie tu! Sio kwamba alikuwa hajui hiyo tabia ya mumewe.
Ndiyo Maajaliwa yake hayo..

"msukule" per se!

Back
Top Bottom