Mume amwagiwa maji ya moto na mkewe

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
MUME AMWAGIWA MAJI YA MOTO NA MKEWE

KIZITO Mahamba (50) (pichani), mkazi wa Mwananyamala Mtaa wa Msili B jijini Dar es Salaam, amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala wodi namba 5A baada ya kufanyiwa ukatili wa kutisha na mkewe ambaye amemmwagia maji ya moto mwilini.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii huku akiwa katika hali mbaya wodini alikolazwa, Mahamba alidai kuwa mkewe, Rabina Mkakamba (38) kabla ya kufanya tukio hilo alianza kuonyesha dalili za kumdharau kila alipojerea nyumbani.

“Siku ya tukio ambayo ilikuwa Oktoba 20, mwaka huu, mke wangu hakuwa katika hali ya kawaida maana kila nilichomwagiza kufanya alikataa, nikajiuliza kulikuwa na nini?

“Hayo yote yalipokuwa yakiendelea, jikoni alikuwa anachemsha maji, nikiwa nimelala nilishitukia mke wangu akiingia chumbani na chupa ya chai ambayo alinitupia na maji kuniunguza sehemu kubwa ya mwili wangu, nadhani alitaka kuniunguza usoni.

Baada ya kufanya kitendo hicho alichukua sanduku la nguo zake na fedha zangu na kutoweka huku akiniacha nikigaagaa .

“Nililetwa hapa hospitali na mtoto wa ndugu yangu na ndiye anayenisaidia,” alisema Mahamba.

MUME AMWAGIWA MAJI YA MOTO NA MKEWE

KIZITO Mahamba (50) (pichani), mkazi wa Mwananyamala Mtaa wa Msili B jijini Dar es Salaam, amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala wodi namba 5A baada ya kufanyiwa ukatili wa kutisha na mkewe ambaye amemmwagia maji ya moto mwilini.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii huku akiwa katika hali mbaya wodini alikolazwa, Mahamba alidai kuwa mkewe, Rabina Mkakamba (38) kabla ya kufanya tukio hilo alianza kuonyesha dalili za kumdharau kila alipojerea nyumbani.

"Siku ya tukio ambayo ilikuwa Oktoba 20, mwaka huu, mke wangu hakuwa katika hali ya kawaida maana kila nilichomwagiza kufanya alikataa, nikajiuliza kulikuwa na nini?

"Hayo yote yalipokuwa yakiendelea, jikoni alikuwa anachemsha maji, nikiwa nimelala nilishitukia mke wangu akiingia chumbani na
chupa ya chai ambayo alinitupia na maji kuniunguza sehemu kubwa ya mwili wangu, nadhani alitaka kuniunguza usoni.

Baada ya kufanya kitendo hicho alichukua sanduku la nguo zake na fedha zangu na kutoweka huku akiniacha nikigaagaa .

"Nililetwa hapa hospitali na mtoto wa ndugu yangu na ndiye anayenisaidia," alisema Mahamba.

Pole sana.
inaelekea hiyo chupa ya chai aliyorushiwa ilikua kubwa sana na ilikuwa na mdomo mpana sana, maana maji yalisambaa haraka sana kabla haja-react. Pole zake.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom