As Salafiyyu91
JF-Expert Member
- Jan 11, 2014
- 2,537
- 2,526
Siku ya leo nilienda kula katika mgahawa fulani hivi nikamkuta mhudumu moja akionekana macho mekundu kwa kilio, nikamuuliza kulikoni dada mbona upo katika hali hiyo? Akaanza kuniambia yeye aliwahi kuzaa na mwanaume mtoto mmoja hapo siku za nyuma na mtoto huyo anaishi kwa huyo mme wake wa zamani sasa tangu majuzi mtoto amekuwa akiumwa akapelekwa hospitali jana kaenda kumuona mtoto anaendelea vizuri na leo asubuhi alipiga simu akaambiwa mtoto wake anaendelea vizuri tu.
Mnamo majira ya saa 7 mchana wa leo akapigiwa simu na mke wasasa wa mumewe akimpa taarifa kuwa mtoto wake amefariki maskini dada wa watu amelia sana mpaka macho yamekuwa mekundu.
Akaanza kuwa taarifa ndugu na jamaa wa karibu wakamwambia vipi umewasiliana na mzazi mwenzio akasema hapana akaamua kumpigia simu majira ya saa 8 ya mchana wa leo akimuulizia hali ya huko nyumbani salama mzazi mwenzie akamjibu huku salama na sasa hivi natoka hospitali nilimleta mtoto amalizie kuchoma sindano sasa niko njiani kwenye gari narudi nyumbani dada wawatu akashangaa! Akamwambia mtoto ukonae hapo akajibu ndio akampa simu akazungumza nae mara dada akaanza kulia kusikia sauti ya mtoto wake kumbe mtoto wake ni mzima
Akaulizwa mbona unalia kuna nini akamjibu mkeo leo kanipigia simu kaniambia mtoto amefariki jamaa akampigia simu mke wake hawakuelewana kwasababu jamaa alikuwa barabarani alafu anaendesha gari.
Baada ya kufika nyumbani jamaa kamuuliza mke wake kwanini ameamua kumfanyia hivyo mzazi mwenzie? Akawa hana majibu.
Jamaa akawa amekasirika sana kwa kitendo hicho amegombana na mkewe na ameamua kumuacha mkewe kwa kumpa talaka tatu kwa mpigo na kumchukua na kumpeleka police hivi sasa yupo ndani kitacho jiri ntawajuza zaidi.
Ndugu wanajumvi katika mkasa huu nani wakulaumiwa?
Je uwamuzi uliochukuliwa na mwanaume huyu ni sahihi?
Akina mama mnaoishi na watoto wa kambo pateni somo kwa mwenzenu yamemkuta.
Nawasilisha!