Mume ampa talaka 3 mkewe na kaamua kumsweka ndani

As Salafiyyu91

JF-Expert Member
Jan 11, 2014
2,537
2,526
Siku ya leo nilienda kula katika mgahawa fulani hivi nikamkuta mhudumu moja akionekana macho mekundu kwa kilio, nikamuuliza kulikoni dada mbona upo katika hali hiyo? Akaanza kuniambia yeye aliwahi kuzaa na mwanaume mtoto mmoja hapo siku za nyuma na mtoto huyo anaishi kwa huyo mme wake wa zamani sasa tangu majuzi mtoto amekuwa akiumwa akapelekwa hospitali jana kaenda kumuona mtoto anaendelea vizuri na leo asubuhi alipiga simu akaambiwa mtoto wake anaendelea vizuri tu.

Mnamo majira ya saa 7 mchana wa leo akapigiwa simu na mke wasasa wa mumewe akimpa taarifa kuwa mtoto wake amefariki maskini dada wa watu amelia sana mpaka macho yamekuwa mekundu.

Akaanza kuwa taarifa ndugu na jamaa wa karibu wakamwambia vipi umewasiliana na mzazi mwenzio akasema hapana akaamua kumpigia simu majira ya saa 8 ya mchana wa leo akimuulizia hali ya huko nyumbani salama mzazi mwenzie akamjibu huku salama na sasa hivi natoka hospitali nilimleta mtoto amalizie kuchoma sindano sasa niko njiani kwenye gari narudi nyumbani dada wawatu akashangaa! Akamwambia mtoto ukonae hapo akajibu ndio akampa simu akazungumza nae mara dada akaanza kulia kusikia sauti ya mtoto wake kumbe mtoto wake ni mzima

Akaulizwa mbona unalia kuna nini akamjibu mkeo leo kanipigia simu kaniambia mtoto amefariki jamaa akampigia simu mke wake hawakuelewana kwasababu jamaa alikuwa barabarani alafu anaendesha gari.

Baada ya kufika nyumbani jamaa kamuuliza mke wake kwanini ameamua kumfanyia hivyo mzazi mwenzie? Akawa hana majibu.

Jamaa akawa amekasirika sana kwa kitendo hicho amegombana na mkewe na ameamua kumuacha mkewe kwa kumpa talaka tatu kwa mpigo na kumchukua na kumpeleka police hivi sasa yupo ndani kitacho jiri ntawajuza zaidi.

Ndugu wanajumvi katika mkasa huu nani wakulaumiwa?

Je uwamuzi uliochukuliwa na mwanaume huyu ni sahihi?

Akina mama mnaoishi na watoto wa kambo pateni somo kwa mwenzenu yamemkuta.

Nawasilisha!
 
huo ndio urijali!ingawa adhabu imevuka kiwango.angemuonya ht kwa talaka rejea.ila ukienda mbele na kurudi nyuma tamshi alilotoa halikuwa zuri mtu unaweza kuhisi labda amempa sumu mtoto au ana nia mbaya na mtoto
 
Alafu huyo dada alichokuwa analingia kwasababu eti amezaa nae watoto wengi na mke wa zaman alizaa nae mtoto mmoja tu sasa yeye hataki kuishi na mtoto wa kambo coz watoto wake yeye ni wengi!!!
 
daaaah kumuweza kweli yaaani

sasa ingekuwa mm ningempiga mpk nimpande alalaf kwa hasira namtia mdudu wa skio
 
Hizo chuki hizo... ndio zimemponza huyo dada.. japokuwa adhab ni kubwa.. lakin jamaa amesimama kama mwanaume na kufanya maamuzi. Tabia kama hiz hazivumiliki
 
Siku ya leo nilienda kula katika mgahawa fulani hivi nikamkuta mhudumu moja akionekana macho mekundu kwa kilio, nikamuuliza kulikoni dada mbona upo katika hali hiyo? Akaanza kuniambia yeye aliwahi kuzaa na mwanaume mtoto mmoja hapo siku za nyuma na mtoto huyo anaishi kwa huyo mme wake wa zamani sasa tangu majuzi mtoto amekuwa akiumwa akapelekwa hospitali jana kaenda kumuona mtoto anaendelea vizuri na leo asubuhi alipiga simu akaambiwa mtoto wake anaendelea vizuri tu.

Mnamo majira ya saa 7 mchana wa leo akapigiwa simu na mke wasasa wa mumewe akimpa taarifa kuwa mtoto wake amefariki maskini dada wa watu amelia sana mpaka macho yamekuwa mekundu.

Akaanza kuwa taarifa ndugu na jamaa wa karibu wakamwambia vipi umewasiliana na mzazi mwenzio akasema hapana akaamua kumpigia simu majira ya saa 8 ya mchana wa leo akimuulizia hali ya huko nyumbani salama mzazi mwenzie akamjibu huku salama na sasa hivi natoka hospitali nilimleta mtoto amalizie kuchoma sindano sasa niko njiani kwenye gari narudi nyumbani dada wawatu akashangaa! Akamwambia mtoto ukonae hapo akajibu ndio akampa simu akazungumza nae mara dada akaanza kulia kusikia sauti ya mtoto wake kumbe mtoto wake ni mzima

Akaulizwa mbona unalia kuna nini akamjibu mkeo leo kanipigia simu kaniambia mtoto amefariki jamaa akampigia simu mke wake hawakuelewana kwasababu jamaa alikuwa barabarani alafu anaendesha gari.

Baada ya kufika nyumbani jamaa kamuuliza mke wake kwanini ameamua kumfanyia hivyo mzazi mwenzie? Akawa hana majibu.

Jamaa akawa amekasirika sana kwa kitendo hicho amegombana na mkewe na ameamua kumuacha mkewe kwa kumpa talaka tatu kwa mpigo na kumchukua na kumpeleka police hivi sasa yupo ndani kitacho jiri ntawajuza zaidi.

Ndugu wanajumvi katika mkasa huu nani wakulaumiwa?

Je uwamuzi uliochukuliwa na mwanaume huyu ni sahihi?

Akina mama mnaoishi na watoto wa kambo pateni somo kwa mwenzenu yamemkuta.

Nawasilisha!
Mkewe kwa nn udanganye jmani tena akae huko kbs. Sipendi Kweli wanawake wenye roho mbaya.
 
Back
Top Bottom